Jamhuri: Pinda agongana na bilionea Dar!

Jamhuri: Pinda agongana na bilionea Dar!

Nyerere alipoambiwa serikali yake imewekwa mfukoni alitoa tamko kali.....

Hawa ni watu wa karibu wa huyu mswahilina wetu wa magogoni bwana, kukamatwa hamna wa kuwakamata. Huyu jamaa, huyo mwizi wa UDA na yule wa home shopping.....
 
Kwakuwa habari hii imegusa watu walio karibu na watawala na ni habari mbaya, tusubiri tu kusikia lile "rungu" dhalimu la waziri mwenye dhamana likitumika kwa mara nyingine kuadhibu gazeti hili.
 
kama ni kweli,bac tupo pabaya sana,kwamba mtu anaweza jifanyi lolote awezalo,mungu asaidie haki itendeke,coz inaonekana kama wenye pesa wachacha wanashikilia maisha ya wanyonge wengi.

Ndio maana kuna haja ya kuiondoa ccm madarakani. Kuendelea kuipigia kura na kuishangilia tunajipalia makaa wenyewe.
 
2015 Chadema itakapo chukua nchi kuna watu wengi watakimbia kwenda mafichoni
 
Hii nchi bwana, yani ukiwa na uhakika wa kuwanunulia polisi bia tu ujue umeishika dola, kwanini tunafika huko???? Taifa la utawala bora na washeria tunaishi hivi???"

Huyo gabachori tu anaimiliki haki ya watu ndani ya nchi hii???

Baba huko uliko lala amka ushuhudie Kikwete alichoifanya nchi. Amefanya urais kuwa mrahisi, amefanya watu amiliki utu wa wengine!

Enzi zetu tuliimba ahadi za TANU. Kama kweli CCM ni mtoto wa TANU na ASP, au angalau kama ni chama kilichofuata misingi iliyowekwa na waasisi wake waliotokana na TANU na ASP, basi ahadi zile zingeboreshwa na kuimarishwa ili zifanane na mazingira ya karne ya 21. Kati ya ahadi muhimu sana za TANU kulikuwa na zinazosema:

Kila mtu anastahili heshima.
Cheo ni dhamana, sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu

Ahadi zilikuwa nyingi, lakini hapa tulipo leo hii heshima na utu wa mtu umeendelea kudhalilishwa na vyombo vya dola pamoja na viongozi wa dola wakati wananchi wamekuwa hawana mtetezi. Vyeo vimekuwa si dhamana tena, bali vinatumiwa kudhalilisha wananchi bila kuheshimu utu wao.

Tusipofanya maamuzi ya kuuondoa utawala huu wa kidhalimu madarakani, hakuna atakayepona!
 
mkuu mimi nimeogopa sana!kama huyo jamaa anazo anafanyiwa hivyo je mimi nisiye nazo itakuwaje!!

Hapo ndio angehakikisha mpaka amekutoa Mgolo, maana sisi weusi hatuna hadhi ya kumzidi mbwa wao ndani ya nchi yetu wenyewe. Shame!
 
swala sio mafuta wanabiashara zingine kama mfayakazi ana nyumba nairobi magari mawili viwanja kigamboni pocket money dola lakimoja unahitajika uchunguzi wa kina
 
haki huchelewa tu lakini siku moja lazima ipatikane.
 
Kamanda wa Kanda maalum ndugu Kova amekaa kimya kama hajasikia yeye ni kuokoteza Bendera za CDM na kuzionyesha kila siku huku watu wakatili kama hawa akiwaacha
 
duuh mtumishi unakaa na $100,000 nyumbani?za nini,hapo mwajiri lazima akuone wewe mwizi

Hata angekaa na bilioni,
kupeleka pesa bank ni mchakato, huenda alitegemea kesho yake asbh angepeleka, hata hvyo bado mwajiri hana haki ya mfanyia unyama huo, kila siku polisi wanasisitiza kuacha kujichukulia sheria mkononi lakini baadala ya wao kushughulika na ukiukaji huo wanaanza kutaka pa kupatia pesa ya viroba.....nchi hii fyuuuuuuuu!,,
 
Jeshi la Polisi si la kurekebisha ni la kuvunja.

Mimi nimekuwa na issue nao kama mwezi hivi nikifatilia haki yangu fulani nilichokuwa nakutana nacho kiutendaji na maadili inatisha! Sijui kama mnaelewa tulipofikia!

Siku ukiwa na issue Polisi na hujui mtu ndio utajuta kuitwa Mtanzania.Utachosaidiwa sana na hao wapelelezi ni kuandika maelezo yako na baada ya hapo ni kuzungushwa.
 
Sikubaliani na huu unyama lakini uyu gabachori alikua anamuibia mwajiri wake kabisaa
 
Naomba Mungu sana haya uapite mbali kwangu na kwa ndugu zangu kwani sidhani kama ninauwezo wa kuvumilia udhalilishaji mkubwa kama huu, i rather die fighting....
Ewe Mungu tuepusha na mibalaa ya wenye fedha ila nchi yetu imefika pabaya sana na hakuna anayejali..kwani ukiwa na fedha polisi yote inakunyenyekea na kukuuzia haki
 
Back
Top Bottom