James Rugemalila afungua kesi Mahakama Kuu

James Rugemalila afungua kesi Mahakama Kuu

Status
Not open for further replies.
Mkuu umeongea point sana.

Hawa woote wana case ya kujibu,

Nashangaa wapuuz wanamshangilia RUGEMALIA ETI WANAMWITA SHUJAA KWA KUFUNGUA KESI HII KAMA KWELI IMEFUNGULIWA KESI YENYEWE,

NCHI NGUMU SANA HII

RAIA WENYEWE FIKRA ZETU NDIO KAMA HIVYO TENA
Na kwa namna moja DPP anaweza kufanya kesi hii ikawa mwanzo mzuri wa kumshitaki Ruge mwenyewe kama sehemu ya kundi la matapeli.
Kama PAP ni feki yeye alilipwaje na Kampuni Feki- kupokea Doc.feki eti serikali inajua hakuna uhalali kisheria. Je alichukua hatua kuzihakiki?
Kama aliweza kuwatonya Tanesco kuwa wanaibiwa na IPTL alishindwa nini kuwa PAP ni feki?


Hii issue ingekuwa USA au UK Ruge angekuwa ashaswekwa ndani,Akaunti zake Benki kusimamishwa na labda yuko nje kwa dhamana.
Lakini kwa vile ni Bonga na issue Magogoni wanajua ,anakula bata kwa mirija!
 
Hii ni chai tu!
Huyu Ruge alikuwa na kesi ya ufilisi na Mechamar mahakamani , akaibuka PAP . Ruge akaongea na PAP wakakubaliana akapeleka hati ya kuondoa hiyo kesi. Jaji utamwa akatoa hukumu , Ruge akamuuzia hisia zake PAP.
Sasa hivi Ruge anatoa wapi ujasiri wa kufungua kesi?
Baada ya Ruge kuuzia hisia zake kwa PAP , maana yake hana chake tena IPTL na kwa hizo hizo hisia zake alizomuuzia PAP anakua mmiliki halali wa iptl.
Hamna kitu hapo , wametuibia hela zetu halafu wanatuletea michezo ya maigizo.
Tunataka pesa zetu mlizoiba escrow.

Nazi imekaa kwenye kiti
 
Mmiliki wa VIP Enginering, aliyekuwa anamiliki hisa IPTL Ndugu Rugemalira amefungua kesi mahakama kuu akiidai serikali jumla ya Sh. 398 bilion zilizokuwemo/ zinazotakiwa kuwemo katika Escrow Account ya Tegete na zilizolipwa kwa kampuni ya PAP na kuleta mjafala mkubwa bungeni.

Katika madai yake, mwenye hisa hatambui malipo yote yaliyolipwa na serikali kwa kampuni ya PAP kwani kampuni hiyo haikuwa na nyaraka halali kutoka kwa msajili wa makampuni BRELA, Taxe Clearance Certificate kutoka TRA, kuandikishwa Tanzania Investment Center na wala mmliki wake kuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini kutoka idara ya Uamiaji.

Katika hoja yake mdai anasema kuwa ni jukumu la serikali kuwahakiki wawekezaji wa nje ili kuwalinda wawekezaji wa ndani pindi tu wanapoingia ubia na wawekezaji wa nje. Ameendelea kudai kuwa, kwa uzembe huo wa serika kwa kutotimiza uhakiki wake wa kigeni ulisabibisha kampuni yake ya VIP Engineering kuingia ubia na Kampuni Feki na kumsababishia hasara ya sh. Bilion 56 kwani alizimika kuvunja ubia wao na kumfungulia mashitaka mbia mwenza PAP baada ya kugundua ubabahishaji wa uhalali wa kampuni hiyo.

Hivyo ameitaka tena serikali kulipa gharama zote alizotumia kuendesha kesi sh.36.8 bilion.
Aidha amedai kuwa aliwafahamisha serikali kutolipa malipo yoyote yaliyokuwemo kwenye account ya Escrow na endapo serikal ingeona kuna haja ya kufanya hivyo basi ilipe kwa VIP au IPTL account ambayo yeye alikuwa signatory.

Katika uwasilishaji wake mahakamani hapo anadai kutofahamu au kutambua kulipwa kwa PAP. Hivyo serikali inatakiwa kulipa tena madai yote kwa VIP au IPTL. Amewapa serikali siku 14 tu toka 1 Januari,2015 kuwa wamelipa malipo yote.

Katika madai hayo, ili kuyadhitisha ameambatinisha:
1. Report ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za serika inayodhibitisha baadhi ya pesa kulipwa kwa PAP
2. Mkaguzi mkuu kudhibitisha kuwa mlipwaji hajawahi kusajiliwa kama mlipa kodi wala kupewa Taxe clearance certificate.
3. Report ya mdhibi mkuu wa Rushwa kuthibitisha kuwa kampuni iliyolipwa haikusajiliwa BRELLA na wala haikuwa na sifa au uhalali kufanya kazi yoyote ya ugavi dhidi ya Shirika lolote la Uma.
3. Report ya Bunge kama muhimili mwingine wa nchi kupitia kamati yake ya hesabu za serikali na mashirika ya uma kutodhibitisha/kudhibitisha juu uhalali wa PAP, mmiliki wa kampuni ya PAP na utendaji wake wa kazi.
4. Mapendekezo ya kamati ya bunge kwa serikali dhid ya PAP, mali zake na mmiliki wake.
5. Mapendekezo ya bunge kwa serikali yanayodhibitisha kuwa PAP haikuwa halali.
6. Mapendezo ya bunge kwa serikali juu ya watendaji wote walioshilikiana kwa pamoja ya kuilipa kampuni isiyo halali.
7. Baadhi ya magazeti likiwemo gazeti la serikal kudhibitisha mkuu wa nchi kupokea na kuridhia mapendezo hayo.
8. Magazeti pamoja na la serikali kudhibitisha serikali kwa kuwaadhibu watendaji wote waluofanya udhembe wa kulipa kampuni isiyo halali.
9. Mkanda wa video ya Rais wa nchi katika hotuba yake kukili watendaji wake kuilipa kampuni isiyo halali na kawasimamisha kazi kwa uzembe huo.
10. Barua ya Mwanasheria mkuu wa serikali kwa Rais ya kuomba kujiuzuru kwa kufanya uzembe huo wa kulipa kampuni isiyo halali.
11. Barua ya Rais kwa Mwanasheria mkuu kukubali kujiuzuru kwake kwa kutoa ushahuri wa kulipa kampuni isiyo halali.

Kesi hiyo uenda ikaamsha tena hasia za wanachi juu ya malipo ya Escrow account. Ni mtihani mwingine kwa serikali kwani Bunge na wanachi hawako tiyari kuona pesa kama hiyo ikilipwa tena.
...safi sana....hii kesi pamoja na kwamba inaweza kuwa ya kimagumashi kama njia ya Ruge kujisafisha na wizi wa escrow...kama kweli imefunguliwa mahakama kuu basi mtu pekee anaetakiwa kuitwa mahakamani kujibu tuhuma hizi ni JK...maana yeye ndie amehangaika kwa nguvu zote kuwasafisha PAP....na amekula baadhi ya hela iliyokwapuliwa BOT(toka kwa shaban gurumo na albert marwa)...wa kujibu kesi hii ni JK na si mwingine....msiwafanye watanzania wapumbavu hapa.....
 
Acha kukurupuka mkuu
This is a brilliant move that will expose the CCM government.
Ruge hakulipwa hela za ESCROW.
Ruge alilipwa hela za uuzaji wa hisa katika kampuni yake.
Transactions za ESCROW zilifanyika mapema hata kabla ya yeye kuuza
Zilifanyika kinyemela
Go Ruge...Go Tibaijuka
Kikwete and CCM has to learn hard way
Come to election the ESCROW issue itabaki kuwa hot

Umesomeka;
Lakini unamuziaje mtu usiyemjua mali yako!


Kama atakuja na hoja kuwa hakuuza hisa zake hapo nitamwelewa na kwamba alipewa zawadi na Singa Singa na yeye akagawa zawadi kwa wengine.
Kwa mpango huo hatua ya kwenda mahakamani ni ni nzuri ili kulinda pesa walizochukua na kwamba Singa singa apotee kama Balali alivyopotea.

Bongo raha tupu!

Katika madai yake, mwenye hisa hatambui malipo yote yaliyolipwa na serikali kwa kampuni ya PAP kwani kampuni hiyo haikuwa na nyaraka halali kutoka kwa msajili wa makampuni BRELA, Taxe Clearance Certificate kutoka TRA, kuandikishwa Tanzania Investment Center na wala mmliki wake kuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini kutoka idara ya Uamiaji.
 
Lugemarila arudishe kwanza pesa alizopewa na tapeli mwenzie sethi
 
Hii inaweza kuwa part two ya Movie

Inawezekana kuna watu wameji-mobilze ku-counter attack.

Tatizo kubwa hapa ni kitendo cha Ikulu yetu kuhusishwa na kashfa hii na bado wanawaadhibu watu wengine bila wao kuguswa hata kidogo.

Ni bora utende haki kwa asilimia 100 kuliko vinginevyo,

Hii si habari njema kwa ma-CCM
 
Hicho kiambanisho cha TAKUKURU ndiyo kimemaliza kesi na kumnyima ushindi. Sababu TAKUKURU bado hawajamaliza uchunguzi wao.
 
Hii nimependa sana. Kama naona watu mikojo iketeremka kwenye suruali
 
Na kwa namna moja DPP anaweza kufanya kesi hii ikawa mwanzo mzuri wa kumshitaki Ruge mwenyewe kama sehemu ya kundi la matapeli.
Kama PAP ni feki yeye alilipwaje na Kampuni Feki- kupokea Doc.feki eti serikali inajua hakuna uhalali kisheria. Je alichukua hatua kuzihakiki?
Kama aliweza kuwatonya Tanesco kuwa wanaibiwa na IPTL alishindwa nini kuwa PAP ni feki?


Hii issue ingekuwa USA au UK Ruge angekuwa ashaswekwa ndani,Akaunti zake Benki kusimamishwa na labda yuko nje kwa dhamana.
Lakini kwa vile ni Bonga na issue Magogoni wanajua ,anakula bata kwa mirija!

Mukulu alishasema hahangaiki na watu binafsi,Na huo ndo ulikuwa mwanzo wa kabri cha Ruge.Hata kama ailishalipwa pesa zake lakini kama alikujakugundua kua PAP alikua na nyaraka faki ana haki ya kudai kua aliibiwa,msimamizi wa haya yote alikua serikali,mbaya zaidi jamaa alilipa kodi.Chezea kina change we we!!
 
Si waliwekeana kinga na singasinga; ngoja atakuja alipe madai ya Bro Ruge.
 
Hii ni chai tu!
Huyu Ruge alikuwa na kesi ya ufilisi na Mechamar mahakamani , akaibuka PAP . Ruge akaongea na PAP wakakubaliana akapeleka hati ya kuondoa hiyo kesi. Jaji utamwa akatoa hukumu , Ruge akamuuzia hisia zake PAP.
Sasa hivi Ruge anatoa wapi ujasiri wa kufungua kesi?
Baada ya Ruge kuuzia hisia zake kwa PAP , maana yake hana chake tena IPTL na kwa hizo hizo hisia zake alizomuuzia PAP anakua mmiliki halali wa iptl.
Hamna kitu hapo , wametuibia hela zetu halafu wanatuletea michezo ya maigizo.
Tunataka pesa zetu mlizoiba escrow.

Hili sakata kweli kizungumkuti. Rais wa nchi alionesha wazi kutokulielewa. Mimi pia nimejitahidi sana kuelewa nimeshindwa. Ni kama vile una hoja ya msingi. Hebu fafanua, Jaji Utamwa alitoa hukumu juu ya shauri gani? Kwa maneno mengine, James alifungua kesi kudai nini ambapo Jaji Utamwa aliamua in his favor? Ni kwa namna gani hukumu ya Jaji Utamwa ili-trigger ulipwaji wa fedha zilizokuwa kwenye account ya escrow? Kama James aliiomba mahakama kufuta/kusimamisha ufilisi wa IPTL na mahakama ikaridhia kupitia hukumu ya Jaji Utamwa?, hukumu hiyo ilipelekeaje kutolewa kwa pesa zilizokuwa kwenye account ya escrow? Ni nini kilimfanya Katibu Mkuu Nishati kuomba mwongozo kwa Mwanasheria Mkuu kuhusu utoaji wa fedha zilizokuwa kwenye account ya escrow? James anasema aliionya serikali kutolipa fedha zilizokuwa kwenye account ya escrow na kama aliyepaswa kulipwa ni IPTL au VIP. Kwa nini serikali iliilipa PAP badala ya IPTL? James anasema serikali ilimwingiza mkenge kwa kutofanya uhakiki wa kampuni ya kigeni iitwayo PAP. Je, serikali ilipata kumthibitishia James kuwa PAP ni kampuni halali? Au hili linathibitisha madai kuwa Waziri Mhongo ndiye aliyemtambulisha PAP kwa James?
 
Hata kabla ya kufika huko kwenye uma na sio uma

Ukishasema tu PAP was not a recognized legal person in Tanzania kipindi hili deal linafanyika...then kila kitu kinakuwa void.

Then kila transaction iliyofanyika na PAP ni void....

Cha ajabu Rais wa Tanzania amewatetea hawa PAP....Eti baadaye walipata vibali

Nakubaliane nawe kabisa ngoja JR awtufundishe adabu si tunajifanya wajuaji. Mimi si mwana sheria, lakini nakumbuka "void abnitial". Yaani PAP was not existing at the time all these were taking place. HAIPO sasa utadai nini kama kitu hakipo ni hewa.
 
Ruge wakomeshe hao, si walimkombatia tapeli wakihindi acha waisome namba sasa,
 
Ccm hiyoooo, inapelekwa machinjoni
 
huyu Rugemalila ana uhusiano gani na JK mbona ana kiburi sana utafikiri hii nchi na hizo mahakama ni za mjomba yake .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom