James Rugemalila afungua kesi Mahakama Kuu

James Rugemalila afungua kesi Mahakama Kuu

Status
Not open for further replies.

lebraza

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
124
Reaction score
114
VIP Engineering imekanusha habari hizi:


TAARIFA KWA UMMA

Kuna uvumi unazagaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii kuwa mmiliki wa VIP Enginering and Marketing Limited, "aliyekuwa anamiliki hisa IPTL Ndugu Rugemalira" amefungua kesi Mahakama Kuu akiidai Serikali jumla ya TShs. 398 bilioni.

VIP Engineering and Marketing Limited inapenda kuufahamisha umma kuwa hizi taarifa si za kweli, hakuna kesi yoyote ambayo imefunguliwa na VIP Engineering and Marketing Limited au Bw. James Rugemalira dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mahakama Kuu ya Tanzania au Mahakama nyingine yoyote.

VIP Engineering and Marketing Limited inaamini uvumi huu unalenga kuleta uchonganishi wa VIP Engineering and Marketing Limited kwa umma ili kukidhi maslahi binafsi ya waanzilishi wa uvumi huo.


VIP ENGINEERING AND MARKETING LIMITED

03 JANUARI, 2015

Email:
vipemltd2@gmail.com

=========

Habari ilikuwa hivi:

Mmiliki wa VIP Enginering, aliyekuwa anamiliki hisa IPTL Ndugu Rugemalira amefungua kesi mahakama kuu akiidai serikali jumla ya Sh. 398 bilion zilizokuwemo/ zinazotakiwa kuwemo katika Escrow Account ya Tegete na zilizolipwa kwa kampuni ya PAP na kuleta mjafala mkubwa bungeni.

Katika madai yake, mwenye hisa hatambui malipo yote yaliyolipwa na serikali kwa kampuni ya PAP kwani kampuni hiyo haikuwa na nyaraka halali kutoka kwa msajili wa makampuni BRELA, Taxe Clearance Certificate kutoka TRA, kuandikishwa Tanzania Investment Center na wala mmliki wake kuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini kutoka idara ya Uamiaji.

Katika hoja yake mdai anasema kuwa ni jukumu la serikali kuwahakiki wawekezaji wa nje ili kuwalinda wawekezaji wa ndani pindi tu wanapoingia ubia na wawekezaji wa nje. Ameendelea kudai kuwa, kwa uzembe huo wa serika kwa kutotimiza uhakiki wake wa kigeni ulisabibisha kampuni yake ya VIP Engineering kuingia ubia na Kampuni Feki na kumsababishia hasara ya sh. Bilion 56 kwani alizimika kuvunja ubia wao na kumfungulia mashitaka mbia mwenza PAP baada ya kugundua ubabahishaji wa uhalali wa kampuni hiyo.

Hivyo ameitaka tena serikali kulipa gharama zote alizotumia kuendesha kesi sh.36.8 bilion.
Aidha amedai kuwa aliwafahamisha serikali kutolipa malipo yoyote yaliyokuwemo kwenye account ya Escrow na endapo serikal ingeona kuna haja ya kufanya hivyo basi ilipe kwa VIP au IPTL account ambayo yeye alikuwa signatory.

Katika uwasilishaji wake mahakamani hapo anadai kutofahamu au kutambua kulipwa kwa PAP. Hivyo serikali inatakiwa kulipa tena madai yote kwa VIP au IPTL. Amewapa serikali siku 14 tu toka 1 Januari,2015 kuwa wamelipa malipo yote.

Katika madai hayo, ili kuyadhitisha ameambatinisha:
1. Report ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za serika inayodhibitisha baadhi ya pesa kulipwa kwa PAP
2. Mkaguzi mkuu kudhibitisha kuwa mlipwaji hajawahi kusajiliwa kama mlipa kodi wala kupewa Taxe clearance certificate.
3. Report ya mdhibi mkuu wa Rushwa kuthibitisha kuwa kampuni iliyolipwa haikusajiliwa BRELLA na wala haikuwa na sifa au uhalali kufanya kazi yoyote ya ugavi dhidi ya Shirika lolote la Uma.
3. Report ya Bunge kama muhimili mwingine wa nchi kupitia kamati yake ya hesabu za serikali na mashirika ya uma kutodhibitisha/kudhibitisha juu uhalali wa PAP, mmiliki wa kampuni ya PAP na utendaji wake wa kazi.
4. Mapendekezo ya kamati ya bunge kwa serikali dhid ya PAP, mali zake na mmiliki wake.
5. Mapendekezo ya bunge kwa serikali yanayodhibitisha kuwa PAP haikuwa halali.
6. Mapendezo ya bunge kwa serikali juu ya watendaji wote walioshilikiana kwa pamoja ya kuilipa kampuni isiyo halali.
7. Baadhi ya magazeti likiwemo gazeti la serikal kudhibitisha mkuu wa nchi kupokea na kuridhia mapendezo hayo.
8. Magazeti pamoja na la serikali kudhibitisha serikali kwa kuwaadhibu watendaji wote waluofanya udhembe wa kulipa kampuni isiyo halali.
9. Mkanda wa video ya Rais wa nchi katika hotuba yake kukili watendaji wake kuilipa kampuni isiyo halali na kawasimamisha kazi kwa uzembe huo.
10. Barua ya Mwanasheria mkuu wa serikali kwa Rais ya kuomba kujiuzuru kwa kufanya uzembe huo wa kulipa kampuni isiyo halali.
11. Barua ya Rais kwa Mwanasheria mkuu kukubali kujiuzuru kwake kwa kutoa ushahuri wa kulipa kampuni isiyo halali.

Kesi hiyo uenda ikaamsha tena hasia za wanachi juu ya malipo ya Escrow account. Ni mtihani mwingine kwa serikali kwani Bunge na wanachi hawako tiyari kuona pesa kama hiyo ikilipwa tena.
 
safi kabisa rugemalira. hili nililisema wiki mbili zilizopita hapa kuwa mmliki halali wa IPTL atakuja muda si mrefu na atadai hela zake.
 
safi sana serikali ya magamba ni wapuuzi yule waziri aliyesema hausiki na mauzo ya kampuni inayomhusu atashiriki kutulipa hapa

kabla ya uchaguzi mkuu

singa singa kama pombe imewalewesha miccm october tunawasukuma bila nguvu kubwa shennzzzz magamba
 
safi sana ruge.wakabe wapumbavu hawa
Nilishasema mmiliki Wa iptl atakuja kudai pesa zake.

Kuna watu watadai alilipwa za escrow.no.alilipwa kuuza hisa za kampuni take hakuwa na haja kujua pesa zimetoka wapi.
 
safi kabisa rugemalira. hili nililisema wiki mbili zilizopita hapa kuwa mmliki halali wa IPTL atakuja muda si mrefu na atadai hela zake. Kwa wale msiofahamu kampuni ya MECHMAR ambaye ndiyo mwenye hisa 70% ya kule Malaysia inamilikiwa na Royal family ya UK, her Majesty the Queen.




ESKRO season two
 
Naomba mwanasheria aje hapa atupe uchambuzi wa kisheria. Naona kama kuna siasa kwenye vinavyoitwa vithibitisho na maelezo hayajakaa kimahakama sawasawa.
 
Kweli we mleta mada kopo tupu lenye makelele mengi hivi unatuona sisi hamnazo kama kijiweni kwenu ama vipi?

Hivi mtu alieuza hisa za kampuni yake na akalipwa kwa kuridhia anaweza vipi fungua kesi mahakamani.
Istoshe hiyo kampuni ya PAP ni kampuni ya mfukoni kama ilivyokuwa RICHMOND baadaye DOWANS wakadai hela yao ya bure.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom