James Rugemalila afungua kesi Mahakama Kuu

James Rugemalila afungua kesi Mahakama Kuu

Status
Not open for further replies.
Haha bora bwana sheria zetu na wana sheria wetu kina vitu wanavikosa.nice move ruge..!!
 
Hili sakata kweli kizungumkuti. Rais wa nchi alionesha wazi kutokulielewa. Mimi pia nimejitahidi sana kuelewa nimeshindwa. Ni kama vile una hoja ya msingi. Hebu fafanua, Jaji Utamwa alitoa hukumu juu ya shauri gani? Kwa maneno mengine, James alifungua kesi kudai nini ambapo Jaji Utamwa aliamua in his favor? Ni kwa namna gani hukumu ya Jaji Utamwa ili-trigger ulipwaji wa fedha zilizokuwa kwenye account ya escrow? Kama James aliiomba mahakama kufuta/kusimamisha ufilisi wa IPTL na mahakama ikaridhia kupitia hukumu ya Jaji Utamwa?, hukumu hiyo ilipelekeaje kutolewa kwa pesa zilizokuwa kwenye account ya escrow? Ni nini kilimfanya Katibu Mkuu Nishati kuomba mwongozo kwa Mwanasheria Mkuu kuhusu utoaji wa fedha zilizokuwa kwenye account ya escrow? James anasema aliionya serikali kutoilipa PAP fedha zilizokuwa kwenye account ya escrow kwa kuwa PAP si mmiliki halali wa IPTL. Kwa nini serikali iliilipa PAP badala ya IPTL?
Sijui kama nitaweza kujibu maswali yako yote ila kwa kifupi ni kuwa VIP engineering chini ya Ruge ilifunga mashauri ya ufilisi mahakamani kati yake na Mechamar juu ya ufilisi wa IPTL. Kabla shauri halijaisha akaibuka PAP ( wanajua wenyewe walichokubaliana) , Ruge akapeleka hapati ya kutoa hilo shauri ya ufilisi na akamuuzia PAP hisia zake 30%.
Hapo jaji utamwa akatoa hukumu kuwa all affairs of iptl should be handled to PAP.
Sasa kwasababu wezi walishadhamiria kutuibia wakapotosha hiyo hukumu wakasafisha akaunti ya escrow.... Hizo fedha zikagaiwa kwa wezi wote ikiwemo wale wa Ikulu yetu na wengineo na kumlipa Ruge dili lake la hisa 30% tena muhongo akiwa ndiyo dalali.
Sasa leo hii watanzania tunakomaa warudishe fedha zetu anaibuka mshirika wa wizi huu anamshitaki mwizi mwenzake. Huoni hapo kuna kamchezo wa kisanii.?
 
Huyu kamwaga mboga yule anamwaga ugali. Tunasema kama mbwai na iwe mbwai tu...
 
Hii Tegeta Escrow itamchafua Kikwete na kufuatia hotuba yake kwa wanaodaiwa kuwa wazee Wa Dar, huenda akaaibika na kutufanya Watanzania tusahau mema yake yote.

Vv
 
Mkuu, Ruge alishaitahadharisha serikali mapema kabisa kwamba isitoe pesa za Escrow hadi alipwe mauzo yake ya hisa kutoka kwa PAP. Hii dhahama na kashfa zote za Escrow zimemkuta kwa sababu serikali ilifunga masikio na kuamua kumlipa PAP kabla hajawa mmiliki halali wa IPTL. Baada ya PAP kulipwa hela za Escrow, ndipo akamlipa Ruge.

Tatizo la Ruge ni vile kumtumia dalali muhongo kufunga dili na PAP , hapo ndiyo atapoteza credibility.
Pili kitendo cha kuuza hisa zake na hukumu ya utamwa kuoverule kuwa all affairs of iptl should be handled to PAP , baada ya hapo kilichofuatia iptl hakimuhusu Ruge tena.
Hiyo kesi kanyaboya tu , sisi tunahitaji pesa zetu.
 
Maadam huu uzi umefika mpaka page ya saba bila kuondolewa,basi hii habari inaweza kuwa ni ya kweli.

Sasa hapa wa kuwajibika ni Kikwete mwenyewe na ajiuzuru mara moja.
 
Wow ruge mmwaaaa,i just like the way you handle things,oga you are just smart meen!
 
Nchi hii laiti ingekuwa na the so called" Accountability" basi Rugemalira angekuwa Shahidi Muhimu sana kwenye sakata la IPTL! Yeye amewawezesha PLAYERS wote hususan wale waliokuwa mawaziri wa nishati na madini NGELEJA, YONA, J, KARAMAGI na washereheshaji AGs CHENGE, WEREMA et al ... Leo hii anakuja na mkakati wa kulamba Zaidi!!! Grrrrrrrrrrrrr... Wao wanalamba bia kwa kwenda mbele sisi tuna nunua Umeme wa Bei mbaya, maisha magumu...

Rugemalila ni msanii tokea enzi ya utawala wa Marehemu baba wa Taifa wenye kujua historia ya nchi hii watawaeleza Rugemalila alikua vipi hata mwalimu alimvulia kofia na akampa BAN! Sidhani kama Kikwete anamjua vizuri huyu mzee!
3.JPG
 
alichofanya Ruge ni sahihi kwani yeye aliuza hisa tu na si fedha ambazo tayari walishagema na mbia mwenzake! fedha zilizokuwa kwenye acc ya escrow (kwa mujibu wa jk) ni za ruge! sasa kwanini asizidai? serikali inajuwa hili ndio maana ilijidanganya na kinga hewa! ngoja tusubiri maana hili hata Zito alilisema bungeni!

JK naye ni wa kusikilizwa?
Ruge alipofanya dili na PAP halafu akakubaliana na hukumu ya jaji utamwa kuwa all iptl affairs should be handled to PAP ni kuwa Ruge alishapoteza kila kitu kuhusu iptl.
Kwa kifupi baada ya hapo iptl haitamuhusu tena.
 
huyu Rugemalila ana uhusiano gani na JK mbona ana kiburi sana utafikiri hii nchi na hizo mahakama ni za mjomba yake .

Ukizijua sheria raha sana. unacheza tu na peni na unageuka kuwa bilionea, hakuna kutoa jasho.
 
Haha bora bwana sheria zetu na wana sheria wetu kina vitu wanavikosa.nice move ruge..!!
 
Nchi hii laiti ingekuwa na the so called" Accountability" basi Rugemalira angekuwa Shahidi Muhimu sana kwenye sakata la IPTL! Yeye amewawezesha PLAYERS wote hususan wale waliokuwa mawaziri wa nishati na madini NGELEJA, YONA, J, KARAMAGI na washereheshaji AGs CHENGE, WEREMA et al ... Leo hii anakuja na mkakati wa kulamba Zaidi!!! Grrrrrrrrrrrrr... Wao wanalamba bia kwa kwenda mbele sisi tuna nunua Umeme wa Bei mbaya, maisha magumu...

Mbona hii trela tu, serikali ikijitia kumfilisi kama PAC ilivyoshauri basi yeye ndio ataifilisi serikali.
 
Mmoja wa wanasheria wa ruge ni dada mmoja anaitwa julie em sure sha played a role here shes so smart...!!ruge is just a genius.
 
Sijui kama nitaweza kujibu maswali yako yote ila kwa kifupi ni kuwa VIP engineering chini ya Ruge ilifunga mashauri ya ufilisi mahakamani kati yake na Mechamar juu ya ufilisi wa IPTL. Kabla shauri halijaisha akaibuka PAP ( wanajua wenyewe walichokubaliana) , Ruge akapeleka hapati ya kutoa hilo shauri ya ufilisi na akamuuzia PAP hisia zake 30%.
Hapo jaji utamwa akatoa hukumu kuwa all affairs of iptl should be handled to PAP.
Sasa kwasababu wezi walishadhamiria kutuibia wakapotosha hiyo hukumu wakasafisha akaunti ya escrow.... Hizo fedha zikagaiwa kwa wezi wote ikiwemo wale wa Ikulu yetu na wengineo na kumlipa Ruge dili lake la hisa 30% tena muhongo akiwa ndiyo dalali.
Sasa leo hii watanzania tunakomaa warudishe fedha zetu anaibuka mshirika wa wizi huu anamshitaki mwizi mwenzake. Huoni hapo kuna kamchezo wa kisanii.?

Ni dhahiri kuwa hapa kuna kamchezo. Sasa Ruge alitaka IPTL ifilisiwe. Baadaye akabadili mawazo na kuiomba mahakama ibatilishe zoezi la kuifilisi IPTL. Sasa kwanini Jaji alisema "all affairs of IPTL should be handed to PAP"? badala tu ya kusitisha ufilisi? Kwa nini Jaji aseme "all affairs of IPTL should handed to PAP" ilhali hisa za VIP ni 30% tu?
 
Asije uwawa mzee Ruge. maana mashahidi wote kwenye ile kesi ya ufisadi ya singa singa huyu kule kenya waliuwawa....
 
Muhongo anasubiri nini kuachia ngazi?yeye si ndia aliwakutanisha PAP na VIP?kumbe PAP ni kampuni feki,jamani kweli vingozi wetu wana vichwa vya panzi

Muhongo bado kiporo alikuwa sawa na chakula cha moto kinasubiriwa kupoa.
 
Tatizo la Ruge ni vile kumtumia dalali muhongo kufunga dili na PAP , hapo ndiyo atapoteza credibility.
Pili kitendo cha kuuza hisa zake na hukumu ya utamwa kuoverule kuwa all affairs of iptl should be handled to PAP , baada ya hapo kilichofuatia iptl hakimuhusu Ruge tena.
Hiyo kesi kanyaboya tu , sisi tunahitaji pesa zetu.

Kama hii taarifa ni kweli (maana hata kesi No haijaambatanishwa),then JR ana hoja, tena nzuri tu. Yeye alipatanishwa na serikali kuuza share zake, akaridhia akauza. PESA zikapigwa, akalipwa baadaye. Kama nimeelewa kesi hi vema, malipo aliolipwa, hajui kama ni za ESCROW lakini yeye kesha lipwa na PAP kulingana na makubaliano (ingawa PAP wamemlipa baada ya deal kuiva). Baadaye, anagundua kuwa PAP ni feki. Kumbe kadalalishwa na fake non existant, void company! Ndio msingi wa madai yake kwamba kwa kuwa ni void, kwa hiyo lolote lililofanyika ni kama halipo. Sasa sijui sheria inasemaje kuhusu hili lakini kwa vyovyote vile kama ni kweli, basi mchezo ni mzuri na kuna mengi ndani yake yanaibuka. Na kama ni kweli, basi JR anaweza kuwa nia yake si pesa tu bali kuwaumbua serikali, maana yeye hata kodi alilipa sasa ni kazi kwa serilaki kudhihilisha kuwa yeye ni sehemu ya deal. Sehemu pekee ingawa haimbani ni kwa nini aligawa pesa nyingi kiasi kile tena kwa watu wa serikali na, chama nk. Lakini hakuna sheria inamzuia mtu kutumia mali yake apendavyo labda hadi ihakikishwe nia ya kugawa hivyo ni kununua haki kama hungo n..

Kazi kweli kweli hta kama si JR basi hoja hii ni nzuri hata kutumiwa na wanasheria wanaojitegemea kuibana serikali.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom