James Rugemalila afungua kesi Mahakama Kuu

James Rugemalila afungua kesi Mahakama Kuu

Status
Not open for further replies.
Huyu muhaya anakili nyingi sana. Viongozi wetu wanezoea kufanya kazi kwa mazoea sasa ngoja, wapewe somo, kwanza ndio wamesababisha na jina la Rugemalira kuchafuliwa kwa njaa zao za kitoto

Ruge ni kichwa soma hoja zake hapo juu ndio utamuelewa usicheze na mtu aliyekulia kwa kula ndizi utotoni.
 
Ruge anaiua CCM kwa kifo staili ya KANU.....yeye hapotezi kitu......lazima wamfate kwa magoti wasiumbuke......
 
Haya ni matokeo ya kuwa na chama, serekali, na viongozi legelege.
Hadi uchaguzi ujao msishangae hata serikali na nchi nzima ikawa imeuzwa.
 
Ruge anaiua CCM kwa kifo staili ya KANU.....yeye hapotezi kitu......lazima wamfate kwa magoti wasiumbuke......

na hio ndio solution pekee tofauti na hapo magogoni 2015 octoba wameipoteza.
 
Dah! Hivi BOT ilipata nyaraka ya kutodaiwa tena? Authenticity ya ile Nyaraka ikoje kisheria? ... Jamaa anang'ang'ania kunyamazishwa au ni mpango mkakati wa kukwapua fedha za Uchaguzi?... Hii move itakuwa na madhara permanent kwa CCM na Serikali yake! Huu ni Mwaka wa Uchaguzi, hope wanalijua hilo!!!
 
mwaka wa mafanikio huu..ngoja awavuruge kwanza ili tujue yaliyo jificha zaidi....kitafahamika mwaka huu..
 
Muhongo anasubiri nini kuachia ngazi?yeye si ndia aliwakutanisha PAP na VIP?kumbe PAP ni kampuni feki,jamani kweli vingozi wetu wana vichwa vya panzi
 
Tume confirm na baadhi ya mawakili na mahakimu, huu ni uzushi hakua kesi kama hii mahakama za hapa duniani. Labda kama amefungua kesi ahera
 
Ninge mshauri Rugemalira aka draft upya madai yake maana akienda na haya atashindwa case na yata tupiliwa mbali siku ya kwanza! Case hii atashindwa mapema mno?
 
Rugemalila anachokifanya kimepangwa na kikwete na mafisadi kwa pamoja. Kumbuka kikwete na majizi wenziye hawalipi fedha zao za mfukoni. Ni namna ya ku divert attention ya umma kutoka kurejeshwa kwa fedha za escrow, kuwawajibisha wadau wa wizi huo na kuwachukulia hatua za kisheria.

Hasa pale Tanzania inaposhindwa fedha zilizotoka Stanbic Bank ambazo ikulu ya kikwete ni mnufaika kiasi kwamba hataki hata zizungumziwe na yeyewala hana mpango wa kuzitaja.

Kinachofanyika ni kuwafanya waTanzania waone suala hili kkwa mtazamo mwingine kwamba fedha zile zilikuwa za VIP Engineering na si za uma kama kikwete linvyowafanya watanzania wajinga amini.

Na pia ni kumfanya raisi mhuni kikwete anayekamata vijana wanaopeleka ujumbe wa amani kwa taifa kwake na kuyaacha majizi menziye, asichukue hatua kama ilivyopendekezwa na bunge ili wasimuabishe wenziye waliosema wakiwajibika nchi itatikisika. Kwa kisingizio kwamba shauri liko mahakamani na bado linaonyesha utata wa nani mmiliki halali wa fedha zile as if watu wote ni walilpaga GPA 2 kama kikwete.

Lingine ni mpango fisadi wa kukomesha watanzania na wabunge wao wanaokimbilia kutaka kuwajibisha mafisadi kwamba wanalilpeleka taifa kwenye hasara kubwa zaidi ya kulipa billions of money kutokana na maamuzi magumu dhidi ya mafisadi ambao wana mkono mpana kama Pinda alivyowahi kusema.

Hii kesi Rugemalila anashinda na wanagawana kila kikwete na wezi wenzao kwa kukomesha watanzania wenye kudai haki.

Huu ni mpango wa kikwete na wahuni wenzake.

Lakini kabla fedha zile hazijalipwa, wanatakiwa wawe wamesha zirudisha za mgawo wa wa kwanza. Hii sanaa haikubaliki.

Kwa wale wasioona hadi watoke damu masikioni:-

Tuambieni uzalendo wa Rugemalika uko wapi? Fisadi ni fisadi tuj. Mwizi kama kikwete, ruge, Singa, Lowasa, chenge, na ccm kwa ujumla wake n.k ukiona wanaongea mema ujue ni njia ya kukufanya ujisahau waibe zaidi. Haya mamtu hayawezi kua na uchungu kwa taifa.

Kigugumikzi cha kikwete kimeibuka na mkakati wa ruge!!!!!!!!.


Halfu eti viongozi wa Africa wanaambizana waondoke ICC, upumbavu mtupu. Mtakaokuwa mmebakia, mtaenda ICC mkiwa na sikio moja, wengine pua ziko nusu wengine kweny viti vya miguu mitatu. Ndipo mtakapotambua kwamba Tanzania ina wenyewe. Pu.mbavu kabisa.
 
Tume confirm na baadhi ya mawakili na mahakimu, huu ni uzushi hakua kesi kama hii mahakama za hapa duniani. Labda kama amefungua kesi ahera

hahaha.....labda wanapima joto la umma......
 
acha kukurupuka mkuu
this is a brilliant move that will expose the ccm government.
Ruge hakulipwa hela za escrow.
Ruge alilipwa hela za uuzaji wa hisa katika kampuni yake.
Transactions za escrow zilifanyika mapema hata kabla ya yeye kuuza
zilifanyika kinyemela
go ruge...go tibaijuka
kikwete and ccm has to learn hard way
come to election the escrow issue itabaki kuwa hot

wewe ndiye unakurupuka mkuu

kwani unadhani hizo 30percent alizolipwa vip kutoka iptl ni pesa zipi kama sio hizi za escrow account??
 
Mmiliki wa VIP Enginering, aliyekuwa anamiliki hisa IPTL Ndugu Rugemalira amefungua kesi mahakama kuu akiidai serikali jumla ya Sh. 398 bilion zilizokuwemo/ zinazotakiwa kuwemo katika Escrow Account ya Tegete na zilizolipwa kwa kampuni ya PAP na kuleta mjafala mkubwa bungeni.

Katika madai yake, mwenye hisa hatambui malipo yote yaliyolipwa na serikali kwa kampuni ya PAP kwani kampuni hiyo haikuwa na nyaraka halali kutoka kwa msajili wa makampuni BRELA, Taxe Clearance Certificate kutoka TRA, kuandikishwa Tanzania Investment Center na wala mmliki wake kuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini kutoka idara ya Uamiaji.

Katika hoja yake mdai anasema kuwa ni jukumu la serikali kuwahakiki wawekezaji wa nje ili kuwalinda wawekezaji wa ndani pindi tu wanapoingia ubia na wawekezaji wa nje. Ameendelea kudai kuwa, kwa uzembe huo wa serika kwa kutotimiza uhakiki wake wa kigeni ulisabibisha kampuni yake ya VIP Engineering kuingia ubia na Kampuni Feki na kumsababishia hasara ya sh. Bilion 56 kwani alizimika kuvunja ubia wao na kumfungulia mashitaka mbia mwenza PAP baada ya kugundua ubabahishaji wa uhalali wa kampuni hiyo.

Hivyo ameitaka tena serikali kulipa gharama zote alizotumia kuendesha kesi sh.36.8 bilion.
Aidha amedai kuwa aliwafahamisha serikali kutolipa malipo yoyote yaliyokuwemo kwenye account ya Escrow na endapo serikal ingeona kuna haja ya kufanya hivyo basi ilipe kwa VIP au IPTL account ambayo yeye alikuwa signatory.

Katika uwasilishaji wake mahakamani hapo anadai kutofahamu au kutambua kulipwa kwa PAP. Hivyo serikali inatakiwa kulipa tena madai yote kwa VIP au IPTL. Amewapa serikali siku 14 tu toka 1 Januari,2015 kuwa wamelipa malipo yote.

Katika madai hayo, ili kuyadhitisha ameambatinisha:
1. Report ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za serika inayodhibitisha baadhi ya pesa kulipwa kwa PAP
2. Mkaguzi mkuu kudhibitisha kuwa mlipwaji hajawahi kusajiliwa kama mlipa kodi wala kupewa Taxe clearance certificate.
3. Report ya mdhibi mkuu wa Rushwa kuthibitisha kuwa kampuni iliyolipwa haikusajiliwa BRELLA na wala haikuwa na sifa au uhalali kufanya kazi yoyote ya ugavi dhidi ya Shirika lolote la Uma.
3. Report ya Bunge kama muhimili mwingine wa nchi kupitia kamati yake ya hesabu za serikali na mashirika ya uma kutodhibitisha/kudhibitisha juu uhalali wa PAP, mmiliki wa kampuni ya PAP na utendaji wake wa kazi.
4. Mapendekezo ya kamati ya bunge kwa serikali dhid ya PAP, mali zake na mmiliki wake.
5. Mapendekezo ya bunge kwa serikali yanayodhibitisha kuwa PAP haikuwa halali.
6. Mapendezo ya bunge kwa serikali juu ya watendaji wote walioshilikiana kwa pamoja ya kuilipa kampuni isiyo halali.
7. Baadhi ya magazeti likiwemo gazeti la serikal kudhibitisha mkuu wa nchi kupokea na kuridhia mapendezo hayo.
8. Magazeti pamoja na la serikali kudhibitisha serikali kwa kuwaadhibu watendaji wote waluofanya udhembe wa kulipa kampuni isiyo halali.
9. Mkanda wa video ya Rais wa nchi katika hotuba yake kukili watendaji wake kuilipa kampuni isiyo halali na kawasimamisha kazi kwa uzembe huo.
10. Barua ya Mwanasheria mkuu wa serikali kwa Rais ya kuomba kujiuzuru kwa kufanya uzembe huo wa kulipa kampuni isiyo halali.
11. Barua ya Rais kwa Mwanasheria mkuu kukubali kujiuzuru kwake kwa kutoa ushahuri wa kulipa kampuni isiyo halali.

Kesi hiyo uenda ikaamsha tena hasia za wanachi juu ya malipo ya Escrow account. Ni mtihani mwingine kwa serikali kwani Bunge na wanachi hawako tiyari kuona pesa kama hiyo ikilipwa tena.
I doubt this story because yeye ndiye aliyelazimisha kuwe na indemnity kabla BoT haijalipa fedha hizi kwa PAP. Na nadhani VIP ilithibitisha mahakamnani kuwa PAP ni mmiliki halali wa hisa za Mechmar
 
Muhongo anasubiri nini kuachia ngazi?yeye si ndia aliwakutanisha PAP na VIP?kumbe PAP ni kampuni feki,jamani kweli vingozi wetu wana vichwa vya panzi

hahahahah mama ulukuwa hujui hilo? ni kama richmond vile kampuni iko mfukoni watu wanatembea nayo. mwaka huu ccm mnalo lazima iondoke na mtu hiyo.
 
Acha kukurupuka mkuu
This is a brilliant move that will expose the CCM government.
Ruge hakulipwa hela za ESCROW.
Ruge alilipwa hela za uuzaji wa hisa katika kampuni yake.
Transactions za ESCROW zilifanyika mapema hata kabla ya yeye kuuza
Zilifanyika kinyemela
Go Ruge...Go Tibaijuka
Kikwete and CCM has to learn hard way
Come to election the ESCROW issue itabaki kuwa hot

Ningekuwa Moderator haya maelezo yako ningeyaweka juu kabisa kwenye huu uzi ili watu waelewe nini Mr.Ruge alilipwa.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom