James Lembeli apasua jipu migomo ya walimu na madaktari

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
aitaka serikali ishuhulikie matatizo isikimbilie mahakamani, migomo bado ipo

asema haiwezekani baba kugombana na mama na watoto halafu akawa wa kwanza kukimbilia polisi

Asema ukificha maradhi kifo kitakuumbua, migomo bado inaendelea

Adai nchi hii siyo tena na wakulima na wafanyakazi, ni ya wafanyabiashara, matapeli na wahuni

Awaonya wabunge wanaoponda walimu kugoma kwamba wakirudi majimboni kwao wataongea na nani

Aisuta serikali kwa nini haipeleki wabunge mahakamani kwa kudai posho zaidi
 
Ushahidi mwingine wa mgomo wa madaktari kuwa unaendelea ni maamuzi ya serikali ya Kenya kuwarudisha majeruhi wa ajari ya basi Nairobi haraka sana juzi. wangefia moi wote.
 
Ushahidi mwingine wa mgomo wa madaktari kuwa unaendelea ni maamuzi ya serikali ya Kenya kuwarudisha majeruhi wa ajari ya basi Nairobi haraka sana juzi. wangefia moi wote.

tena usiku kwa ndege ya jeshi.....
 
Lembeli kasema ukweli mtupu! In fact all assential issues are only debated but never resolved
 
Mh inanikumbusha enzi hizo mkipigana au kuparurana, enzi hizooooo, unakimbia kushtaki ili usiadhibiwe mwenzio aipatepate!!!!
 
That is the indication that Health System in this country is actually paralysed. Am personally very scared.
 
Lembeli kasema kweli, ila kwa yale aliyosema anakwenda kinyume na sera ya magamba ya kuwanyamazisha wadai haki kwa kukimbilia mahakamani.
 
zoba na ritz mnasemaje huyo ni ccm mwenzenu mnaona na mbunge wa kuchaguliwa patamu hapo kwi kwi kwi
 
Mgomo wa walimu haujaanza leo, tangu mimi niko primary mgomo ulikuwepo. Haujawahi kuwa official tu, na hii ndio inaua elimu yetu.
 
Huyu ni mbunge wa magamba ila nahisi hana maslah ya moja kwa moja na chama chake maana huwa sikuzote wenzake wakienda kushoto yeye kulia au neutral.

Mtaji wa mbunge ni wapiga kura wake, na waalimu ndio watu muhimu sana walio karibu na wapiga kura wote, tena wanao ushawishi mkubwa katika jamii hasa vijijini.
 
Mtaji wa mbunge ni wapiga kura wake, na waalimu ndio watu muhimu sana walio karibu na wapiga kura wote, tena wanao ushawishi mkubwa katika jamii hasa vijijini.
Kwa lugha nyingine ameshasoma alama za nyakati maana siku hizi issue siyo kukubalika ndani ya chama bali wananchi wako unawatetea kiasi gani, nadhani huyu na Filikunjombe wanatembea hatua sawa sawa! Safi sana
 
Acha aseme ukweli. Mdharau mwiba mguu huota tende. JK alisema kura za walimu sizitaki lakini ngoja uone mziki wake 2015. Walimu wengi 70% wamesaini opposition.
 
Sidhani kama mnaielewa hii serikali vema. Ni genge la watu wanaofanya ujanja kusogeza siku ilimradi wanafanikiwa kula na kupora kwa amani. Siyo nia yao kutatua matatizo yaliyopo iwapo wana uwezo wa kuendelea kututawala huku wakipata kila wanachotaka. Ndiyo maana wafanyakazi wakigoma kudai marupurupu wanakandamizwa halafu wanawaongezea Wabunge ili wasiibane serikali.
 
Lembeli kafunguka! Nilitamani wabunge wote wawe wakweli na kuacha unafiki. Nimewasikia wabunge wawili wanawake ambao wamejinadi kuwa walikuwa waalimu eti wanawaponda wenzao kwa kugoma! Kilichowafanya wakakacha ualimu ni nini kama si kutafuta maslahi? Wameniboa sana maana walikuwa wanachangia kwa unafiki wa hali ya juu kupalilia posho zao za bungeni.
 
Back
Top Bottom