BAADA YA KUKACHA BAJETI Mbunge CCM apasua jipu *Asema hawezi kufunga mdomo hadi kieleweke * | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAADA YA KUKACHA BAJETI Mbunge CCM apasua jipu *Asema hawezi kufunga mdomo hadi kieleweke *

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Jun 25, 2012.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  [h=3]BAADA YA KUKACHA BAJETI Mbunge CCM apasua jipu *Asema hawezi kufunga mdomo hadi kieleweke *Awataka wabunge wote wamuunge mkono [/h]

  Na Benedict Kaguo, Dodoma

  MBUNGE wa Kisesa, Bw. Luhaga Mpina (CCM), amefichua siri iliyomfanya atoke nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma wakati mchakato wa kupiga kura za kupitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/13 ukiendelea.

  Bw. Mpina ndiye mbunge pekee wa CCM, aliyetangaza ndani ya bunge dhamira yake ya kutoiunga mkono bajeti hiyo kutokaana na sababu mbalimbali.


  Miongoni mwa sababu hizo ni kuondolewa sh. trilioni 2.7 ambazo zilipitishwa na wabunge kwa ajili ya Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano uliozinduliwa mwaka 2011 na Rais Jakaya Kikwete.

  Kutokana na msimamo wa Bw. Mpina, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Bw. William Lukuvi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Bw. Stephen Wassira, walitumia nguvu ya ziada kumuomba aungane na wenzake ili kuunga mkono bajeti hiyo.

  Akiguzumza na Majira mjini Dodoma jana, Bw. Mpina alisema kabla ya Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa hajaanza kujibu hoja za wabunge, Bw. Bw. Lukuvi na Bw. Wassira, walimweleza kuwa, hoja yake ya kutaka ongezeko la sh. bilioni 500 imesikika.

  Alisema Mawaziri hao walimweleza kuwa, muswada wa sheria ya fedha mwaka 2012, haujapitishwa hivyo bado ipo nafasi ya kutafuta fedha ili kuongezwa katika mpango huo.

  Alisema wakati Dkt. Mgimwa akijibu hoja za wabunge licha ya kusisitiza muswada huo haujapitishwa, hakusema kama fedha za maendeleo zitaongezwa.

  “Kwa kuwa kanuni za kudumu za Bunge, toleo la mwaka 2007, hazitoi nafasi kwa wabunge kupata ufafanuzi wa zida kuhusu maelezo yaliyotolewa na Waziri, niliamua kutopiga kura.

  “Kimsingi hoja yangu ilikuwa haijajibiwa licha ya kupewa maelezo ya awali na Mawaziri ambayo yalikuwa nje ya kumbukumbu (hansard), msimamo wangu unabaki pale pale,” alisema.

  Aliongeza kuwa, hoja yake ya kutaka fedha za maendeleo ziongezwe kutoka sh. trilioni 2.2 hadi sh. trilioni 2.7 kwa fedha za ndani ili kukidhi mahitaji ziweze kutekeleza miradi mbalimbali, bado hajaifunga wala haijafika mwisho.

  Bw. Mpina alisema, muswada wa sheria ya fedha mwaka 2012, (finance bill of 2012) utawasirishwa na kuidhinishwa na Bunge baada ya kupitia bajeti za Wizara zote.

  Alisema sheria hiyo ndiyo inayoidhinisha mapato na matumizi ya
  vifungu vyote vya fedha hivyo aliwataka wabunge wote bila kujali itikadi za vyama vyao, kuungana, kupunguza na kufuta matumizi yasiyo na tija kuziokoa fedha hizo ili zipelekwa katika miradi ya maendeleo na kutafuta vyanzo vipya vya mapato.

  “Lengo ni kuhakikisha miradi iliyopangwa kutekelezwa mwaka wa fedha 2012/13, iweze kutekelezwa bila visingizio vyovyote, miradi ambayo imeainishwa katika mpango huu ipo ya aina mbili.

  “Ipo inayotekelezwa na Serikali kwa ubia na sekta binafsi na ile inayotekelezwa na Serikali kwa asilimia 100 lakini kutokana na upungufu wa sh. bilioni 500 katika bajeti ya maendeleo, miradi mingi imepata fedha pungufu na mingine kukosa kabisa.

  “Kwa mfano, baadhi ya miradi hiyo ni Tanzania Investment Bank (TIB), imetengewa sh. bilioni 30, badala ya sh. bilioni 125, Tanzania Agricultural Development Bank (TADB), imetengewa sh. bilioni 40 badala ya sh. bilioni 100,” alisema Bw. Mpina.

  Aliongeza kuwa, miradi mingine ni ile ya upembuzi yakinifu na kujenga skimu za umwagiliaji ambayo imetengewa sh. bilioni 7.1 badala ya sh. bilioni 242 na ujenzi na ukarabati wa reli ya kati sh. bilioni 134 badala ya sh. 198.

  Mingine ni viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa nchini kama pamba, korosho, mkonge na mifugo kuachwa bila kutengewa fedha yoyote.

  Miradi mingi ya maji itaendelea kutegemea fedha za nje ambazo haziletwi kwa wakati au kutoletwa kabisa.

  Share on facebook Share on twitter Share on email Share on print More Sharing Services
   
 2. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Kifupi huwezi kufanya harakati ukiwa ndani ya ccm,zaidi wata-mkolimba au kumwakyembe tu!anapaka rangi upepo tu!harakati zina wenyewe chadema huyo ni gamba tu kama magamba mengine!
   
 3. O

  Orche Senior Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Siasa hizo!
   
 4. a

  afwe JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mlitaka aseme nini baada ya kuwa amekaidi chama chake?
   
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,700
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  Huyu simuelewi
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Yeah! Amekaidi chama kwa maslahi ya wananchi wake!
   
 7. m

  mchaichai JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 650
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  namsubiri ule wake
   
 8. Mwanyasi

  Mwanyasi JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 5,761
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Watashindwa tu kama walivoshindwa kwa Mwakyembe.....! Mungu yupo upande wa mwenye haki. Lakini pia wakimuua mtetea wananchi watajiongezea maadui nikiwemo mimi!
   
 9. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Jembe la pili baada ya Simbachawene. Hakuna jambo zuri kwa maisha ya mwanadamu kama kuusimamia ukweli. Tuwape support hawa watu, tunaitaji viongozi kama hawa! May God guide them.
   
Loading...