Lembeli aichana serikali kuhusu migomo ya walimu na madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lembeli aichana serikali kuhusu migomo ya walimu na madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mtego wa Noti, Aug 13, 2012.

 1. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Akichangia bungeni leo, bila woga amesema seikali inachokifanya siyo sawa kwa kuwanyanyasa walimu kwa kuwapeleka mahakamani na kutojali maisha yao hasa suala la mishahara yao mibovu la laki 2 na nusu. amesema serikali inajifurahisha eti mgomo umeisha na wakati mgomo uko palepale maana walimu mpaka sasa hawafundishi.
  Bila kumung'unya maneno amesema hii nchi siyo ya wakulima na wafanyakazi tena, amesema ni ya wahuni tu!!! pia amesema kama wabunge ambao wana maposho mengi na bado wanalalamika, je, walimu hawana haki ya kudai nyongeza kwenye mishahara yao?
  Amekemea mtindo wa serikali kukimbilia mahakamani kuwashtaki walimu akisema ni sawa na baba anagombana na mke wake na watoto halaf anakimbilia polisi kuwashitaki polisi.
  Amesema serikali isicheze na walimu wala madaktari mana ndio walioiwek madarakani na huenda wakaendelea kugoma mpaka 2015 iwapo mambo yao hayatatekelezwa
  Nawasilisha!
   
 2. M

  MTK JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Well spoken James Lembeli; way to go!
  nimezipenda hizi;
  1. Waziri akisimama hapa atwambie je Tanzania ni nchi ya nani maana inaonekana sio nchi ya wakulima na wafanyakazi tena!!
  2. Serikali kuwashitaki mahakamani walimu ni sawa na baba kugombana na baba kugombana na mke na watoto kisha akakimbilia mahakamani kutafuta suluhu!
  3. Kama sisi wabunge kila siku tunalalama tuongezewe posho iweje walimu wakidai nyongeza wapelekwe mahakamani!? mbona wabunge hawajapelekwa mahakamani!?
  4. walimu, wakulima na madaktari wasibezwe, wasipuuzwe; wasikilizwe maana ni wao waliotufikisha hapa tulipo (mjengoni).
  5. Serikali inatamba eti mambo sasa shwari, walimu na madaktari wamerudi kazini; sio kweli wapo lakini hawafanyi kazi! serikali inajidanganya.

  Kudos James Lembeli; Truth is devine and has no ideology.
   
 3. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Siamini kama kuna magamba wana busara kiasi hiki THUMB UP James!
   
 4. a

  augustino ameri JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  LEMBELI Maneno aliyosema hayana unafiki na yametoka moyoni,WATU WAMECHOKA,UGANDA ENZI ZA IDD AMIN WALICHOKA, NAYE ALITUMIA NGUVU ZA DOLA KUPITA KIASI,MAjesh ya TZ Yalipoingia Uganda wananch walisaidia kuonyesha askali wao walipo wakiita majeshi ya UKOMBOZ.I.watanzania wanaweza kuwaunga mkono wamalawi pia kama njia ya ukomboz.
   
 5. Asumwisye

  Asumwisye Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Well spoken for sure Lembeli, maana bila walimu wengi wetu tusingekuwa hapa tulipo..!
  Madai ya walimu ni ya msingi sana, wanastahili kuongezewa kipato na kuboreshewa makazi na mazingira ya kazi.
   
 6. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Hii kali ya malawi tena!
   
 7. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Walimi wanaweza kuwa na maamuzi ya ajabu 2015. Just imagine kila mwalimu akitafuta wapiga kura 100 vijijini!!!!! Na wa mjini 100! Kitatokea nini!
   
 8. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CCM siyo wa kuwaamini hao mdau!Mwisho wa kuchangia kwake hajasema anaunga mkono hoja 100%?
   
 9. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  naona hajaunga hoja kabisa...nadhani anaweza akawa tofauti na magamba wengine wanaobwabwaja na mwisho wake wanaunga mkono hoja kwa zaidi ya 200%
   
 10. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,926
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Walimu wanahitaji kuishi vizuri including maboresho ya sehemu wanazofanyia kazi ili kuokoa elimu ya nchi yetu ambayo iko mahututi bin taaban.
   
 11. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Lembelli anaujumbe mzito hasa anaposema bila waalimu wabunge wa ccm wasingekuwa hapo maana yake ni kwamba; waalimu walishiriki kwa kiwango kikubwa kuiba kura kwa ajili ya ccm, sasa wanadai kuwa tunawasubiri ccm 2015 nani atawasaidia kuiba kura???
   
Loading...