Rais Kikwete akutana na wahariri; asema madai ya walimu hayatekelezeki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete akutana na wahariri; asema madai ya walimu hayatekelezeki!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Aug 1, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wana JF

  Rais Kikwete leo saa kumi kamili jioni anazungumza na taifa kupitia kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar. Agenda kuu iko mfukoni mwake, lakini swala la mgomo wa walimu huenda likatawala mkutano huo.

  MY Take: JK akumbuke kuna kesi maakamani na hukumu inatolewa kesho. Mkutano wake usije ukaingilia uhuru wa mahakama na kuathiri maamuzi ya kesho.

  Updates:

  Jamani anayefuatilia mkutano huu kwa Radio ama TV atoe updates hapa mara utakapoanza. Mie nitajaribu kutoa updates kama bepari wangu akinipa upenyo kidogo.

  1) Anazungumzia maswala kuhusu uchimbaji na utafutaji gesi asilia na sheria zihusuzo sekta ya gesi

  2. Anaongelea waalimu sasa, kuwa serikali inawajali na inawathamini sana, ila mengi yataongelewa kesho na mahakama

  3) Anasema madai ya walimu ni makubwa na serikali haina uwezo wa kutoa mishahara kiasi hicho

  4) Anasema hawapuuzi walimu ila madai yao ni magumu kutekelezwa. Abeza pia kuipelekea notisi serikali ijumaa wakati jumamosi na jumapili ni siku za mapumziko

  HOTUBA YENYEWE:
  Maswali now;
  Kibanda anauliza; Serikali imejifunza nini kufuatia migomo kuendelea?
  Serikali bado inatuhumiwa kuhusika na utekwaji ulimboka, nini kauli yake??
  MAJIBU; CT SCAN sio sawa na shangingi moja, anayesema hiyo ndio bei ya CT scan aende akapewe pesa ili alete hiyo CT scan.

  Swali la Pili: Bakari Machumu -Citizen; Kuhusu serikali kuwashirikisha wadau wengine katika sekta ya nishati na hasa gesi.

  MAJIBU: Serikali inawashirikisha na inafanya jitihada za kuwa karibu na wote wanaosaidia katika sekta za nishati, gesi na uzalishaji umeme hadi hali itakapokuwa nzuri. Kubinafsisha Tanesco bado si muafaka ila mambo mengine yatafanywa na watawala wajao 2015

  Swali la Tatu: Jesse Kwayu Nipashe; Kukithiri kwa rushwa katika sekta mbalimbali, jitihada gani zimefanywa na serikali maana bado Rushwa inazidi kukithiri ikiwa ni pamoja na wabunge kuanza kuhusishwa na rushwa pia.

  MAJIBU: Rais peke yake hawezi kupambana na rushwa ila mfumo mzima. Serikali imejitahidi kuboresha sheria ya rushwa na kuongeza makosa ya rushwa, PCCB ina ofisi hadi wilayani na ina watumishi wa kutosha, hii ni kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa kupambana na rushwa.

  Swali la Nne: Kuhusu uporaji ardhi, na namna serikali inavyolinda ardhi na hasa katika swala la ushirikiano wa jumuiya ya Afrika mashariki

  MAJIBU: TIC na Serikali za vijiji ndio wanaoweza kugawa ardhi na serikali itaendelea kulinda ardhi inufaishe wazawa.

  PRESS CONFERENCE IMEKWISHA


   
 2. ng'wanankamba

  ng'wanankamba JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 341
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Bora umemtahadharisha mapema asije akasema washauri wake wamempotosha kwa kutomuambia kuwa suala la walimu liko mahakamani asiliongelee. "Fore warned fore armed"
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nadhani aliyemshauri kuitisha hii Press Conference hakumshauri vizuri. Angesubiri kesho mchana baada ya mahakama kutoa maamuzi
   
 4. M

  Mlyafinono Senior Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yupo juu ya sheria analizungumzia tu.Ndo itakuwa ajenda yake kwa leo.
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Nimecheka saaaaana. kweli jamii iko makini...hahahahahahahahahahaha
   
 6. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  kimekuchekesha nini mkuu?
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kwani atasema nin zaidi ya ambao hawataki kufanya kazi na serikali yake waondoke!?
  Kwani madr aliwaambia nini? Ingekuwa na mshauri jk ningemwambia aongee lugha ya kuwaconvice waalimu warudi kufundisha kwa matakwa yao na si kulazimisha kama anavyofanyaga!
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Jinsi Rais anavyopewa tahadhari in advance kuwa jambo liko mahamani hivyo asilizungumzie leo!
   
 9. b

  beyanga Senior Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  atazungumzia serikari kuanzisha mfuko wa futari kabla ya bajeti kuisha
   
 10. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Aulizwe swali: Kufuatia mgomo wa madaktari na sasa waalimu, serikali yake inao mpango gani wa kujiuzulu?
   
 11. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Inabidi tumshauri maana washauri wake wanampotosha nae haoni kama anapotoshwa
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sawasawa mkuu, tuko pamoja...
   
 13. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Ikifika kesho itakuwa amechelewa zaidi kutoa stuff ya mwezi July japo tayari kachelewa.

  Swali la kijinga!!! ni hotuba ya mwanzo wa mwezi au mwisho wa mwezi uliopita???????
   
 14. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Baada ya Tundu Lissu kushindwa kuwataja wala rushwa wa chadema JK wa ukweli kutumbua jipu jion hii.I trust u JK
   
 15. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Inaelekea amewatosa wazee wa Dar es salaam sasa.
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Ni baada au kabla ya kufuturu? Asije haribu funga yake tu kwa kudanganya
   
 17. m

  msenda Member

  #17
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Yote maisha
   
 18. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tayari anayajua mengine si wanaandikaga wao??
   
 19. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Hotuba za Migomo tumezichoka
   
 20. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Mwambie awaeleze watanzania kuwa Rama wa TISS na wenzake kawaficha wapi?
   
Loading...