Jamani wanaume wasomi mna nini?

Kinachotakiwa huyu mama ajitahidi kuendana na wakati, acheze kulingana na muziki wenyewe! Na aoneshe anaweza akijiona kilaza kweli atakua kilaza sasa kama ana degree atashindwaje kuongea nae baba watoto. Komaa katika shida na raha na mchanganye kwa upendo wa kweli isijekuwa umepunguza mapenzi halafu unakuja kuongea kitu kisichokweli! Kwani mi ninavojua mwanamke akisoma kuzidi mwanaume ndo mwanamke anakuwa na nyodo asikwambie mtu!


Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kwan PHD ndio ubakuwa umesoma degree ngap?

Hamna kitu kibaya kama kumnyanyasa mkeo kwa mambo madogo kama elimu yake kama unampenda kweli na unataka awe level yako ya elimu si umsomeshe

Issue ya kupata hasara kwny biashara ni mambo ya kuongea na kujua tatizo nn anapata hasara bakhresa ije kwa wewe?
 
Binadamu ili awe binadamu anatakiwa apate elimu nyingi sana na iliyo kuu ni ya utambuzi

Kuna kundi kubwa sana la binadamu ambao wameshindwa kabisa kutenganisha ndoa na mambo mengine,kama wewe unajiita msomi halafu unaona mkeo hana maana kwasababu tu hana elimu jua kwamba hiyo elimu uliyonayo bado haijakusaidia kabisa

Ujuzi wa kuifanya ndoa kuwa imara hauletwi na elimu ya darasani bali elimu ya utambuzi zaidi,ngoja niwaulize swali la kijinga,unapokwenda kusomea uhasibu kwa mfano,hivi inawezekanaje uhasibu ukaboresha mahusiano?

Maisha yana mambo mengi sana ya kujifunza na kuelewa,unapokuwa na mtu mzima halafu ukashindwa kujua hayo wewe ni mtoto bado wala hatutajali umesoma mpaka wapi

BACK TO YOU LADIES
Nyie nao mna matatizo yenu kwenye hili,mkishafika sijui huko chuo huwa mnakuwa na mindoto ya ajabu sana,hamtaki kabisa kujifunza nini maana ya ndoa wala ndoa yenye afya,mnataka muolewe na "wasomi" kama nyie mkiamini kuwa "msomi" ana "akili",haya ni ya kujifunza sasa

Unakuta mdada anadai anataka mume,bila kujua anachokitaka ni mume kwa maana ya yule ambae atakuwa nae kwenye maisha ya aina nyingi sana yeye anakomaa "awe na elimu ya kuanzia chuo",khaa unatafuta mtu wa kuajiri kwenye kampuni yako au?

Sisemi elimu haifai lakini ni bora ukajijua kabisa unatafuta kitu gani na sio kujiingiza kutafuta kitu ambacho hukihitaji

Elimu ina faida nyingi sana kwenye maisha ya binadamu hasa kwenye jambo ulilosomea,lakini unapotaka kuleta elimu kwenye ndoa ni sawa na mtu asomee udaktari atake akafanye kazi ya ualimu wa mpira wa miguu!
 
The fact is vere simple,bibie hawezi kutiririka na notes za mzee..
yeye anataka alete habari za lace wigs na salon makeovers za pedicure na manicure wakti
mzee anawaza miformula ya vitabuni tuu...
akae aongee nae tu taratibu...watafikia muafaka tu...
 
ndoa bana......mleta mada umeolewa wewe? zisikie tuu.....
 
Cku zote maisha ya mke na mume yanatakiwa yaanzishwe na watu wawili wenye uwiano unaokaribiana kimtazamo, Socially,Agewise, Spiritually, Education wise na mengine mengi ,Ili mnapoishi muweze kuendana.Mfano labda wewe elimu ndogo kiasi halafu tena ukaoa mke ambaye hata smart phone hawezi kutumia!Ni wazi kuwa mtatofautiana.Suala la kuoa hatuangalii mapenzi tu .Inashauriwa uchumba uchukue muda mrefu kiasi ili kujuana kwa undani.
 

Hili lawezekana
Kuna jamaa mmoja ameachana na mkewe kwasasa anachukua PHD yake chuo flani mkewe alikuwa ni Mwl wa shule ya msingi though sijui chanzo chao kikuu cha kuachAna kwao but nilinote maneno ya jamaa kwamba ANATAKA KITANDA CHAKE KILALIWE NA DEGREE 6
nikawaza tu huenda kuachana kwao kumechangiwa na utofauti wao wa elimu.
 
Queen Horse umenipasua pwaaaaa......

Kumbe rafiki yako kaja kukuambia yoote? Leo atanitambua na tabia yake ya kuanika mambo ya ndani..... Hivi vyuo vya katavinatuharibia wanawake..
 
Last edited by a moderator:


magreat thinkers kama wewe ndio mnaohitajika ktk jamii, well spoken
 
I have masters my wife is std 7 and respect her seriously and she understands it.
 

A cha kabisa,baadhi ya hawa binadamu wana tabia chafu sana ya dharau,roho mbaya na ukatili inapokuja kwenywe masuala ya kuishi na MTU wa mwingine sometimes hata kwa damu Zao wenyewe,you can imagine.PHD na madegree yenyewe bora hata wangekuwa wanakufa nayo
 
Mleta uzi na wewe pia una "dharau" kwa kiasi chako...hivi kozi za kuchechemea ni zipi? Halafu diploma ya ualimu ndio S.I. Unit ya wenye elimu ndogo eee?...just curious!!
Back to the topic, dharau,kujikweza ni tabia ya mtu tu na ni ulimbukeni tu, huyo jamaa hakutarajia kufika alpofika. Watu wana degree zao kadhaa na wakifika nyumbani wanaziacha mlangoni..ndani ni mume wangu,mke wangu full stop!
 
inawezekana huyo jamaa back ground yake ni mbaya wale wa ghetto fabolous wale waliokuwa maisha magumu sana hivyo hali hii huchangia wanakuwa na matatizo ya saikolojia

au kabila letu lile la kujivuna la huku kagera nshomile

Watu wakikulia maisha ya shidA,akipata ni taabu tupu,ubinafsi mwingi na roho mbaya
 
Alafu hii kitu sometimes inasababisha wanaume kuchepuka

Kaoa mwenyewe Mwenye level ya chini( though Mimi siamini kama elimu ya darasani inamfanya mtu ajitambue) then baadaye baada ya kuona mambo hayaendi ndani anatafuta kamchepuko kenye elimu yake kakuziba mapungufu ya mkewe ndo hapo dharau zinapozidi ndani ya ndoa mwisho wa siku anamwona mkewe kilaza badala ya kumpeleka shule ama kumuelimisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…