Nakumbuka tulivyokuwa wadogo tuliishi na mtoto wa kike mwenye tatizo kama hilo ulisemalo Red Giant. Yeye alienda kupigwa sindano za kuzuia matiti kuota/kukua na pia makalio kuwa makubwa na sauti pia ikawa ya kiume. Alipenda sana kucheza na watoto wa kiume na michezo yote ya kiume tulishiriki nae. Hakuwa na rafiki wa kike. Alikuja hama pale tulipokuwa tunakaa ila baadae waliomuona wanasema kwamba aliamua kujiachia katika hali yake ya kawaida ya uwanamke na hivyo matiti yaliota na pia alikuwa na swaga za kike kabisa hadi sauti.
So ni ukweli ukisemacho kipo si abroad tu, hata hapa kwetu Bongo. Tunahitaji kujikubali kwa vile tulivyoumbwa na Mungu kwani hakuna aliyeumbwa mbaya duniani...ukikosa hichi basi ujue umepewa kile na ndiyo maana wazee wetu au wahenga zetu walisema kwamba "Mungu akikupa kilema hakukoseshi mwendo"..hii ina maana ya kwamba kwa vyovyote vile utakavyokuwa basi ujue una cha kufanya maishani mwako na hutakiwi kujuta..shukuru Mungu na jikubali.