Jamani nakufa mwenzenu kwa stress

Jamani nakufa mwenzenu kwa stress

hapo sijakuelewa, kwani mwanzoni kabla hajalipa mahari hukuziona hizo tabia, alafu hapa inakuwa ngumu mana hatujui vigezo ulivyoweka wewe kuwa hakufai ni vipi, ni malaya, mchafu au ..........? angalia mapungufu na mazuri yapi yamezidi, usije ukamuacha alafu ukaingia kubaya zaidi, shetani umjuaye ni bora kuliko malaika usiemjua, swali lingine, je ulimshirikisha Mungu wakati unatafuta mchumba? kwa imani yeyote uliyonayo muombe Mungu akusaidie kwa akili za binadamu ni ngumu lakini kwa Mungu yote ya yanawezekana, kumbuka mke/mume mwema anatoka kwa Mungu.
 
women always are devils i dont trust women,hawana maana ujingaujinga tu,tamaa mbele.
HATA MEN ALWAYS ARE DEVILS I DONT TRUST MEN,hawana maana pia wana tamaa zilizokithiri!!!!mara ngani mwanaume anaenda kujitambulisha kwa mdada na ana lala mbele???mara ngapi anaaumua mpaka kuoa kumbe ana makandokando yake kibao??????better u take precaution mapema kabla mambo hayajaharibika....!!!
 
una kesi ya kujibu,mpaka amefikia kuleta mahari, mliafikiana afanye hivyo. ktk hili yaonekana mmeshibana, baadaye umegundua jamaa sio. hapa ndipo panapohitajika busara ya khali ya juu. unajua mpaka hapo maamuzi mengine yoyote yasiyohusiana na kufunga ndoa hiyo ni fedheha kwa wazazi pande zote mbili, ndugu na marafiki pamoja na nyinyi wenyewe, hivyo kuepusha hayo yote waeleze wazazi kwa uwazi juu ya maamuzi yako. wakipima na kuafikiana nawe kwa moyo mkunjufu haina madhara ,lkn kama sababu zako si za msingi umelivulia nguo lioge.
 
Mmmmhhh hukumtaka ila kunavitu ulikuwa unapata huku unampa Hope kuwa mtaoana ss ndo hyo yamekufika.
 
Nini cha kufanya pale utakapojikuta katika relationship na mtu ambaye umeona hakufai na mahari ameshakulipia?




Simple tu,rudisha pesa yake,fanya mambo yako naye afanye yake maisha yanaendelea kama kawaida.Kwanini umng'ang'anie as if mlizaliwa pamoja????
 
Ndoa sio kitu cha kujaribu uone ikoje halafu kesho usepe, no! kama umeshaona hakufai waambie wazazi wako mrudishe hiyo mahari, vinginevyo utasuffer maisha yako yote yaliyobaki duniani
 
Wewe acha ukichaa si ulitaka masharobaro, handsome, sasa ndo hakuna rangi utakayoacha kuiona. Hakufai kwa lipi sio riziki?
 
Hueleweki Hakufai kwa lipi?, Hakuna mkamilifu duniani na pia inawezekana umekutana na bwana mapesa, TAMAA MBAYA!
 
Nini cha kufanya pale utakapojikuta katika relationship na mtu ambaye umeona hakufai na mahari ameshakulipia?
Mbona unajitia stress bure,kwani mahari umelipa roho yako au pesa na vitu? sasa kwanini ujilazimishe kama umeona hamtuwezana au hamuwezani kwanini shida na raha zimejaa tele! kama kuna kitu anafanya na hupendi muonye na kama hakuelewi mwabie tabia yako na yangu haiendani basi,na mahari pia unaweza muachia kwani pesa zinatafutwa sio furaha. la unaona mahari yako yatapotea na unataka kununua ----- kwa pesa ukuwashe maisha choice ni yako ndugu.....
 
MUNGU WETU MWEMA, awajalie watoto wetu WAUME NA WAKE WAZURI KADIRI YA MAPENZI YAKE, amen!
 
Back
Top Bottom