Jamani msiwaseme vibaya watumishi wa Mungu

sasa ebu angalia Kakobe anavyopendeza na suti yake safi na Kitambi juu wakati waumini wake akina mama maskini yaani choka mbaya utadhani hawajapata msosi siku 3 hivi!
 
Mithali 9

1. Hekima umeijenga nyumba yake, Amezichonga nguzo zake saba;
2. Amechinja nyama zake, umechanganya divai yake, Ameiandalia meza yake pia.

3. Amewatuma wajakazi wake, analia, Mahali pa mjini palipoinuka sana,
4. Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,

5. Njoo ule mkate wangu, Ukanywe divai niliyoichanganya.
6. Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu.

7. Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu.
8. Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda.

9. Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
10. Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.

11. Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa.
12. Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako; Na kama una dharau, utaichukua peke yako.

13. Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.
14. Hukaa mlangoni pa nyumba yake, Juu ya kiti mahali pa mjini palipoinuka,
15. Apate kuwaita wapitao njiani, Waendao moja kwa moja katika njia zao.

16. Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,
17. Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza.
18. Lakini huyo hajui ya kuwa wafu wamo humo; Ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni.
 
Wawe na uwazi kwenye mapato na matumizi yao wachekwe? Maana wakifanya hivyo wafuasi wao watagundua kama hawa jamaa nao ni mafisadi tu ambao wanaishi maisha ya hali ya juu kwa michango chungu nzima toka kwa waumini wao na wakati huo huo hawana unabii wowote ule ni wanafiki tu.

Nadhani suala la kuonesha vitabu vya fedha, ni makubaliano tu baina ya waumini na wachungaji wao. Kama waumini wanaendelea kutoa michango kwa Mwenyezi Mungu, kupitia kanisa lao, hata kama mchungaji anazifuja, thawabu ipo palepale. Na kama wanaendelea kutoa, ni dalili tosha kuwa wanaridhishwa na mwenendo mzima wa uendeshaji wa makanisa yao. Hivyo tuache sentensi za jumlajumla, zenye lengo la kuwatweza watumishi wa Mungu. Hapa mleta thread namuunga mkono.
 
sasa ebu angalia Kakobe anavyopendeza na suti yake safi na Kitambi juu wakati waumini wake akina mama maskini yaani choka mbaya utadhani hawajapata msosi siku 3 hivi!

Sasa wewe ulitaka avae magunia au midabwada ili nafsi yako iridhike?

Nadhani unasahau kuwa uchungaji ni kazi kama kazi nyingine, inayostahili mafao. Wachungaji wana mahitaji kama mimi na wewe, wana familia , ndugu na jamaa wanaowategemea, sasa unategemea waishi vipi, na wahubiri injili saa ngapi?

Naomba tusiingilie imani na majukumu ya watu, kwa maana ni vichekesho kuanza kuongelea vitu tusivyovijua vyema.
 
Naomba kueleweshwa tumeambiwa kuwa manabii karibu wote waliteremshiwa vitabu na Mmungu sasa huyu Nabii geor davie ameletwa au ameteremshiwa kitabu kipi?

Aliyekwambia hivyo amekudanganya, hivyo basi, kimisingi swali lako sio genuine.
 
Watu wakishindwa kukabiliana na Mazingira ya maisha hukimbilia kwenye imani, mie nabii mie nani. WIZI MTUPU

Anapojiita nabii, muulize ana maana gani, sio kukurupuka na kuanza kusema WIZI MTUPU. Huku ni kuosha kinywa.
 
Dr umenipa link ambayo haijajazwa minofu........btw huwa sipendi nikiuliza swali napewa link...nataka uniambie wewe dr mtindio unaelewaje neno nabii......

Maana general ya nabii nimekuelekeza kule kunapostahili. Mimi sio authority ya kutoa definition ya neno 'nabii'. Kama unaona link haikutoshi, ni kujumu lako kama muuliza swali, ku-pursue further literature.

I hope that helps.
 
Mwisho upi?

Acha kutisha watu! Hata miaka 1300 AD walisema ni wakati wa mwisho leo ni 2009!

Mtu ukushakuwa brain washed na dini you can not think beyond the box!

Mwache mdau aeleze anachoamini. Kumwambia kuwa dini ina-brainwash is an insult of highest order.
 
.

Imani yako ndio ikayo kuokoa au kukuangamiza! Nabii? Karnehii iliyo jaa wajanja na vituko vya kila aina kuna na bii kweli? ...Ndio waliwao.

Kama huamini kuna manabii ktk siku za leo, huna haja ya kuwasanifu wanaoamini kuwa ndio waliwao. Huenda wewe ndiwe uliwaye, hivyo kuwa na busara next time.
 
WATUMISHI WA MUNGU WANAKULA MADHABAHUNI - huwezi kucheki fedha ya Mungu

FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA MUNGU - hiyo inayokwenda kwa KAISARI ndio itachekiwa lakini ya MADHABAHUNI - no way - itachekiwa huko huko makanisani - lakini TRA hawawezi kuigusa - kwa taarifa huwa Waumini wanatoa 10% ya mapato yao Kanisani -
 
Kwanini tuchanganyikiwe? sidhani kama solution ni kuhama hama dini eti kwa vile una shida fulani unataka itatuliwe. Haya maisha magumu hayajaanza leo wala jana!

Kama una dini yako tulia nayo, uwe na imani kwa kila uombalo au unachokiabudu!
Kila mtu ana haki yake ya msingi kuchagua vile apendavyo,kama dini aliyoridhishwa na wazazi wake imemboa,ruksa kuhamia nyingine kadri apendavyo,tuheshimu haki yake ya msingi ya kuchagua ali mradi havunji sheria.
 
Naomba kueleweshwa tumeambiwa kuwa manabii karibu wote waliteremshiwa vitabu na Mmungu sasa huyu Nabii geor davie ameletwa au ameteremshiwa kitabu kipi?

Aaah kumbe sio wote....basi kumbe anaweza kuwa nabii bila kuteremshiwa kitabu
 
..nasikia kuna wengine wana kanisa lao linaitwa la Watakatifu waliopo duniani. Inakoelekea kuna mashindano pia ya kutumia vivumishi vya sifa kwenye majina na vyeo vya wahubiri wao. ni lazima kila mmoja awe askofu, nabii, mtume?[/QUOTE]

Hapana sio lazima,na nadhani miongoni mwa watanzania Million 36,hawazidi ata Million 1,hivyo wapo sawa kwa kigezo hicho!!
 
Haya ni matatizo ya kuamini maono. mtu analala, akiamka anatangazia kupata maono kuwa awe nabii.
kwa mtaji huu kila mtu anaweza kuwa nabii.
 
Wadau,

Naonakama tunaacha point ya msingi hapa na tunajichomeka zaidi kwenye maswala ya imani ambao wengi wa wanaochangia tumantoa conclusion katika ufinyu wa ufahamu wa munayozungumzia.

Biblia inasema wazi kuwa Mungu ameweka manabii, wachungaji, mitume, wainjilist, waalimu nawengine (Efeso 4:11)...Hivyo mtu mmoja au wawili kuonekana wana shida katika utumishi wao, sio ushahidi wa kukanusha au kuki-nulify kile ambacho Mungu anakisema wazi katika neno lake. Kama huamini kuwepo kwa mitume, manabii na wengine ni wewe labda na dini yako lakini usifike mbali kwa kuanza kukanusha kweli ya Mungu.

Pia wale wanaokashifu uponyaji, maombezi na mengine, kuweni makini. Mwaweza kujikuta munakuwa wa kwanza kutafuta watumishi wa Mungu kuwaombea sababu hakuna msaada hospital wa tatzo lako. Sisi wengine tumeponywa maganjwa ya kufisha na mungu. tena magonjwa tuliyozaliwa nayo. tumeiona ndugu zetu wakiponnywa kansa na uvimbe kwa maombi. sasa sijui wewe ni nani na kwa mamlaka gani unasema hayapo haya na ni wizi mtupu. Kumbuka katika wengi kuna mengi. inawezekana una habari za maombezi feki au watumishi wa Mungu wanajifanya watumishi kwa interest ya pesa. Bado hilo haliondoi kweli ya Mungu kuwa ana watumishi wanaomtumikia kwa uamnifu. Kama wewe umeokoka na kweli ya Mungu imekuweka huru, huna haja ya kusumbuka. ni rahisi sana kujua hawa walio wadanganyifu. utaifuata kweli na kweli itakuongoza siku zote.

Kama mmoja wetu alivyosema, watumishi wa Mungu ni watu wenye mahitaji kama sisi. Wanatumia muda wao usiku na mchanga kumtafuta Mungu kwa maombi, kusoma, na utulivu ili nao wafundishike kabla ya kufundisha. wakati huohuo wana familia, watoto na ndugu kama sisi, wanastahili malipo tena mazuri. kama watusmihi wa serikali au makampuni wanalipwa mamilioni watumishi wa Mungu wanastahili zaidi kunapokuwa na uwezekano. Huwezi kusema kuwa mtumishi asivae vema au kuwa na afya nzuri eti kwa sababu kuna wakristo wenye hali ngumu.

Mwisho wa dunia upo. Kumbuka tangu Yesu alipopaa ni yeye mwenyewe alisema mwisho umekaribia na tuwe tayari kwnai hakuna ajuaye muda wa saa. usijione wadunda ukadhani nikwa ujanja na maarifa yako. ni neema ya Mungu tu na muda wowote unaweza ukawa unadunda ndani ya box ardhini. Mungu anakupa muda zaidi ili umjue yeye na kuigeukia kweli. Mwisho upo na kila mmoja anawajibika kujiweka tayari kwa huo.

Mjadala wetu uliletwa na utata wa kauli za Joyceline kuhusu ngurumo. sasa tusilazimishe kuwahukumu watumishi wote na kuidharau kweli ya neno la Mungu kwa ajili ya hilo.

Mungu awabari na ninawakaribisha kwa Yesu. wokovu ni bure na unapatikana kwa kila amwaminiye yesu Kristo kama bwana na mwokozi. Unapojaribu kujadili mambo ya kimungu kwa ufahamu wako usio na uwezo hata wa kujitambua wewe mwenyewe vizuri ni kujidanganya. ni lazima uwe ndani yake Mungu ili uyafahamu mambo ya rohoni. Roho mtakatifu ndiye pekee atufundishaye kuzijua siri za Mungu.
 
Kweli ipi?

Mara Mujjahidin wanasema wao wanachoamini ndo Kweli! Mara Wakristo wanachoamini ndo Kweli, Wahindi nao wanachoamini ndo kweli, Makalasinga nao pia wanesema imani yao ndo ya kweli!

Tupo watu 7 bilioni duniani kila dini ina % kiasi tu sidhani kama kuna wanozidi 2 bilioni?

Ndo maana nikasema sisi kama wanadamu tupendane, tuheshimiane na sii kuonyesha ni imani ipi ni bora!
 
hakuna nayepinga kupendana, kusheshimiana na mengine. wala hakuna anayesema dini yake ni bora. BALI BIBLIA INAWEMA WAZI KUWA YESU NDIYE NJIA KWELI NA UZIMA. Bila yeye mtu hafiki kwa BABA.

halafu kwa ufahamu tu, Ukristo sio DINi kama zilivyo nyingine. Yesu hakuja kuleta dini duniani bali ukombozi kwa wote watakaomwamini. Ni wanadamu ndio wameiita dini ila ukweli ni kuwa Ukristo sio dini....kwa nini?

DINI ni mpango/njia/taratibu alizojiwekea mwanadamu katika jitihada zake za kumtafuta mungu (can be any God hata mti).....lakini Ukristo ni mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu aliyekuwa dhambini.....siyo jitihada ya mwanadamu kujiokoa bali ni jitihada za Mungu kumuokoa mwanadamu.

Hivyo unapozungumzia dini/udini, weka ukristo pembeni kati ya hizo ulizozitaja. Ukristo ni njia ya Mungu kumtafuta mwanadamu...ni wale walimwamini Krsto kama bwana na mwokozi bila shaka maishani mwao na kukubali kuishi kulingana na neno lake wakiongozwa na yeye mwenyewe.

Hivyo mimi sikuambii Ukristo ni dini nzuri, bali nakummbia karibukwenye jitihada za Mungu kumtafuta mwanadamu aliyepotea....kwa kauli nyingine....wewe uko kwenye maji umeishiwa nguvu na unagharikishwa, then there come a savor ananyosha mkono anakuambia kamata mkono wangu nikutoe majini. Hakulazimishi, anataka kukubali kwako. Na ndio mana, tofauti na dini nyingine, ukristo hautishiwi na dini zingine, haulazimishi mtu kuwa mkristo au kumzuia mtu asiache ukristo.

Unatufundisha kumfahamu Mungu na kuchagua kumfuata.

mungu akubariki na karibu katika safari hii ya njia ya uzima
 
the issue here is what you believe. Kama unaamini kudondoka kama ndio muujiza hiyo ndio imani yako. Lakini argument ya kwamba hutaki kujua anatumia nini alamradi tu anataja jina la YESU, unakuwa unashau kuwa siku za mwisho watatokea manabii wa uongo ambao watatumia jina la YESU vibaya. Kwahiyo sometimes we need to investigate before we believe directly.
 
Back
Top Bottom