Jamani msiwaseme vibaya watumishi wa Mungu

Nimeisoma thread nzima na napenda kuchangia ifuatavyo:
1) tujue tuko katika nyakati za mwisho - nyakati ambazo maasi yameongezeka kwa kiwango cha juu - always - maasi yanapoongezeka, neema ya Mungu inaongezeka - hence miujiza imeongezeka kutokana na kiwango cha maasi Mfano - siku hizi utasikia watoto wadogo ni wachawi, watu wanauana kwa kutaka utajiri - (the case of Albino killing) - enzi za zamani hayakuwepo.

- so mchawi anapoku-chawia ukapata janga - basi hapo Mungu anaingilia kati na unapona kimiujiza - instantly - kwa jina la Yesu

2) Katika Biblia - imeandikwa kwamba Mungu alishusha HUDUMA TANO - ambazo ni a) Wachungaji b) Waalimu c) Mitume d) Manabii e) Wainjilisti
na pia Ndani ya Roho Mtakatifu kuna KARAMA i.e. - uponyaji, miujiza, kunena kwa lugha, Neno la Maarifa, Hekima, Tafsiri za Lugha, Kupambanua roho, unabii - hizi zote ni kwa ajili ya kuwajenga watu wa Mungu na kuujenga mwili wa Kristo.

3) Hatuingii mbinguni kwa kazi tufanyazo tu - bali kwa kumwamini Yesu na utakatifu - Wagalatia 5:22 - Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi - na TUNDA LA MWILI NI UASHERATI, UCHAFU, UFISADI, IBADA YA SANAMU, UCHAWI, UADUI, UGOMVI, WIVU, HASIRA, FITINA, FARAKA, UZUSHI, HUSUDA, ULEVI, ULAFI, na mambo yafananayo na hayo na watu watendao hayo KAMWE HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU

3) Mungu ni ROHO - inabidi kumwabudu katika ROHO na KWELI - hachunguziki kibinadamu au akili za mwanadamu - so miujiza yake ni ya ajabu kwani yeye pia ni wa AJABU - alituumba kwa ajabu, anatuita kwake kiajabu etc. so be in spirit - otherwise you will end up questioning Gods work for the rest of your life.

BE BLESSED ALL

Mwisho upi?

Acha kutisha watu! Hata miaka 1300 AD walisema ni wakati wa mwisho leo ni 2009!

Mtu ukushakuwa brain washed na dini you can not think beyond the box!
 
1) tujue tuko katika nyakati za mwisho - nyakati ambazo maasi yameongezeka kwa kiwango cha juu - always - maasi yanapoongezeka, neema ya Mungu inaongezeka

Watu wa dini kwa kujifariji mmmh!
Nyakati za mwisho zilisha sikika enzi hizo hata babu wa babu yako hajazaliwa.
We utatangulia watakuja wengine nao watadanganywa hivyo hivyo kama wewe eti nyakati za mwisho.Wakati wa mwisho ni kufa kwako wewe na kupotea na kurudi mavumbini hapo ndo unakuwa wakati wako wa mwisho acha kuogofya watu wenye mioyo miepesi.Mlidanganya ooh 2000 ndo mwisho wa dunia tunadunda mpaka kesho.
 
2meambiwa tufuate maneno siyo matendo, hutakiwi kujua anafanya nini au anatumia nini ananiombea kwa jina la yesu ninapona, mambo yangu yanafunguka ananisomea mistari ya biblia hayo mengine mimi sina shida nayo kwa sababu namwamini Yesu ni bwana na mwokozi wa maisha yangu atumie nini , au nini i dont care.
na kama ni swala la kwenda kutangaza injili vijijini huwa anaenda kwani mwaka mzima anakuwaga dar msiongee kwa ushabiki ongeeni vitu mlivyo na uhakika navyo yeye hatutangazii injili nadhani wengi tangu sunday school tunasoma biblia wengiene ni mabigwa wa wokovu lakini hajawahi kuponywa na mambo yake ni mabaya daily ndo mana tukaletewa watu wa kutufungua na vifungo. kama wengine wanavyosema wengi watakuja kwa jina langu mimi kama mkristo natakiwa niangalie kuna mahali unaingia wewe mwenyewe unaona hapa ni usanii mtupu. mchungaji anaombea mtu mwka mzima hajapona yeye akiona imani yako iko chini sana yani umeenda kujaribu hakuombei maana usipopona ndo utamuona muongo, anafanya kazi na watu wenye imani na wasio na imani anawatia moyo wamwamini Mungu ndo watapona mpo hapo?



.


Kwa hiyo kuna haja ya hospatal , wakati BWANA anaponya.
 
nilisema msiwaseme vibaya sababu najua watu lazima wangecomment vibaya kuhsu haya ninayotaka kuandika.
mimi binafsi naongea habari za huyo mtu siyo kwamba namfanyia promo nina experience nimeanza kuhudhuria maombi yake tangu 2005 mjini arusha mpaka nikaja huku dar kila mara akija nahudhuria , nimeamini na nimebarikiwa kwa hiyo kwa upande wangu sioni tatizo liko wapi but kila m2 ana mtazamo wake.imani yako ndo itakuokoa



.


Imani yako ndio ikayo kuokoa au kukuangamiza! Nabii? Karnehii iliyo jaa wajanja na vituko vya kila aina kuna na bii kweli? ...Ndio waliwao.
 
Joyceline
Kabla ya 2005 ulikuwa unasali kanisa gani? Je hukuwa na imani huko au nini kilitokea
ukahamia hilo kanisa jipya?

Dini yako ndiyo imani yako,hiki ni kitu cha kukumbuka.
 
Shule ya jumapili????
Nimezoea kusoma kwenye biblia nabii Musa na wenzake ndio natatizika kuwa kwa sasa duniani kuna manabii........miaka ya 80-90 sikuwahi kusikia manabii...how come mate?
Mkuu unayafatilia maandiko vema? unajua kuwa hata nguvu za giza zinaponya?
Mkuu unahitaji somo la kutosha........unakumbuka kuna wakati mashehe walilimwa virungu na vijana wa afande tossi mbona hawakupiga swala wale maafande wakisiwapege?
.
Hayo mambo ya kudanganyana, kuponya, kufunguliwa! Hayapo kwao.
 
naomba nijibu kwa ujumla kwanza hakutangaza sababu ile siyo biashara wanaoamini waje wasioamini wasije waliojua wakafika ndo hao ndo mana huwezi kukuta kwenye matangazo anasema leteni wagojwa na wenye shida kama wewe unaamini utaleta mgonjwa na mwenye shida.
kwenye biblia Yesu aliponya watu akawaambia msiseme lakini wale watu walishidwa kunyamaza wakasema na habari zikaenea na hapo ukitoka huambiwi katengaze ukiamua tangaza ukiamua jikaushe lakini ukitendewa mema kwa nini usimrudishie Mungu sifa na utukufu?
Ukisoma Mathayo 7: mstari wa tisa kama sikosei sina uhakika mtanisamehe biblia inasema " nendeni ulimwenguni kote mkahubiri mkisema ufalme wa Mungu umekaribia,mkaponye wagonjwa, kufufu wafu nk. sasa hapo utaona kwamba mkimaliza kuhubiri mponye wagonjwa na msaidie watus hida zao.kama nitakuwa nimequote vibay mnisahihishe kwa wale mnaojua.
Haya story ya yule mama ilikuwa hivi.
yule mama alikuwa mgonjwa muda mrefu akaenda kwenye maombi akaambiwa wewe ni mgonjwa muda mrefu na hapo ulipo una roho ya mauti usipotubu na kuacha dhambi na kumrudia Mungu utakufa yule mama alikuwa ananguvu za giza zinamfuata baada ya mkutano sasa akarudi nyumbani akamuambia mume wake mtumishi kaniambia hivi na hivi na kweli usiku wake mama akafa, ndo mume akaenda kutoa ripoti polisi geor davie akakamatwa lakini baada ya uchunguzi ikagundulika ni nini na mama alipopimwa na madaktari kilichomuua ni cancer ya kizazi alikuwa nayo mda mrefu, nadhani mmenipata
Bibblia inasema kuna walimu, wainjilisti, wachungaji, maaskofu na manabii,hata enzi na agano la kale manabii walikuwepo musa , elia nk. nabii ni mtu anayewasiliana na roho wa Mungu anaweza akajua mambo yako yajayo na yaliyopita na yaliyopo.
.
Hawa manabii waleo mbona hawawaponyi wenye ukimwi?, mbona hawaombi utajiri wanawakamua waumini wao tu! Toeweni sadaka mtafunguliwa mbona hawajifunguwi wao kwanza?
 
I dont trust someone called himself "Nabii" Since that time hakuna nabii wala mtume atapatikana zaidi ya wale waliowahi. Nafikir kwa hili hatuna mchango zaidi ya kila mtu kushika imani yake. Unajua kila kinawezekana kwa imani. Hata wewe kama una imani bila kutoka nyumbani kwako ukashika biblia au msahafu ukasali mwenyewe mambo yanaenda.
Wengi tunafurahia matangazo ya manabii kuwa sehemu fulani, je una imani ndani yako au unatembea kama garasa?



.


Thats right.
 
Watu wa dini kwa kujifariji mmmh!
Nyakati za mwisho zilisha sikika enzi hizo hata babu wa babu yako hajazaliwa.
We utatangulia watakuja wengine nao watadanganywa hivyo hivyo kama wewe eti nyakati za mwisho.Wakati wa mwisho ni kufa kwako wewe na kupotea na kurudi mavumbini hapo ndo unakuwa wakati wako wa mwisho acha kuogofya watu wenye mioyo miepesi.Mlidanganya ooh 2000 ndo mwisho wa dunia tunadunda mpaka kesho.



.


Hakuna mwanzo usio namwisho.
 
Juzi jpili nilihudhuria kwenye maombi ya ngurumo ya upako na nabii geor davie ambaye aliendesha maombi kwenye ukumbi wa diamond jubilee kwa kweli yesu anatenda miujiza pamoja na kwamba watu watasema mengi lakini nimeshuhudia kwa macho yangu , mimi sitakiwi kujua anatumia nini na anafanya nini bora anataja jina la yesu natakiwa nisikilize maneno.
Mkutano huo ulitangazwa jmosi jioni lakini watu walijaa ile mbaya na hajatangaza kwenye redio wala gazeti tumeambiwa tupashane habari.

Ni hivi nabii geordavie atakuwa anaendesha maombi yake dar kwa muda wa wiki nne kwa sababu lile eneo alilokuwa anatumia kule kisongo arusha mwenyewe kamnyan'ganya na linanunuliwa na mfanya biashara mmoja arusha kwa hiyo wakati eneo lingine linaaandaliwa atakuwa dar kwa muda huo kuna muumini ametoa eneo la ekari 2 ndo liko kwenye matengenezo kwa hiyo kwa muda huo waumini wa dar tutapokea upako live pale makonde maeneo ya mbezi beach.

Naomba kueleweshwa tumeambiwa kuwa manabii karibu wote waliteremshiwa vitabu na Mmungu sasa huyu Nabii geor davie ameletwa au ameteremshiwa kitabu kipi?
 
Watu wakishindwa kukabiliana na Mazingira ya maisha hukimbilia kwenye imani, mie nabii mie nani. WIZI MTUPU
 
Tusiwaseme vibaya watumishi wa Mungu? kwa vipi? Kuwasema vibaya vipi?
Mi nadhani maisha yao ndiyo yatawasema walivyo na si vibaya watu wakasema na kutoa tahadhali kwa kile wanadhani hakiko sawa katika utumishi wa wajamaa wengine. Vinginevyo tukitaka kusifia tuuuuuuuuuu WATAPOTEA YAMKINI NA WATEULE. Najua wengi hawapendi criticism wakati tunajua hata Yesu halikuwa criticised hakujali. Alikubali kila kitu.
 
kwikwikwikwikwi watz siku hizi tunachanganyikiwa najua maisha yamekuwa magumu.......

Kwanini tuchanganyikiwe? sidhani kama solution ni kuhama hama dini eti kwa vile una shida fulani unataka itatuliwe. Haya maisha magumu hayajaanza leo wala jana!

Kama una dini yako tulia nayo, uwe na imani kwa kila uombalo au unachokiabudu!
 
..nasikia kuna wengine wana kanisa lao linaitwa la Watakatifu waliopo duniani. Inakoelekea kuna mashindano pia ya kutumia vivumishi vya sifa kwenye majina na vyeo vya wahubiri wao. ni lazima kila mmoja awe askofu, nabii, mtume?
 
Juzi jpili nilihudhuria kwenye maombi ya ngurumo ya upako na nabii geor davie ambaye aliendesha maombi kwenye ukumbi wa diamond jubilee kwa kweli yesu anatenda miujiza pamoja na kwamba watu watasema mengi lakini nimeshuhudia kwa macho yangu , mimi sitakiwi kujua anatumia nini na anafanya nini bora anataja jina la yesu natakiwa nisikilize maneno.
Mkutano huo ulitangazwa jmosi jioni lakini watu walijaa ile mbaya na hajatangaza kwenye redio wala gazeti tumeambiwa tupashane habari.

Ni hivi nabii geordavie atakuwa anaendesha maombi yake dar kwa muda wa wiki nne kwa sababu lile eneo alilokuwa anatumia kule kisongo arusha mwenyewe kamnyan'ganya na linanunuliwa na mfanya biashara mmoja arusha kwa hiyo wakati eneo lingine linaaandaliwa atakuwa dar kwa muda huo kuna muumini ametoa eneo la ekari 2 ndo liko kwenye matengenezo kwa hiyo kwa muda huo waumini wa dar tutapokea upako live pale makonde maeneo ya mbezi beach.

Mathayo 7:15, 21-23 "Jihadharini na manabii wa uongo watu wanowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa wa mwitu wakali. 21-23, Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu."
 
Wait a minute, mbona heading reads msiwaseme watumishi wa Mungu halafu mleta hoja anasema alihudhuria mahubiri na kutangaza kuwa kutakuwa na upako etc? i dont see the connection, Anyway its good marketing. To be honest I dont believe in any of the so called nabii, mtume etc si kwa sababu mahubiri mabaya no ila ni undeshaji mzima wa hizi ministries kwaninin hamna uwazi kwenye mapato,matumizi, kudelegate mambo mf utakuta mchungai/nabii anamanage kanisa peke yake akisafiri basi mahubiri via tv, all these pose a big question mark to me. I dont know if am wrong but i smell something fishy!

Wawe na uwazi kwenye mapato na matumizi yao wachekwe? Maana wakifanya hivyo wafuasi wao watagundua kama hawa jamaa nao ni mafisadi tu ambao wanaishi maisha ya hali ya juu kwa michango chungu nzima toka kwa waumini wao na wakati huo huo hawana unabii wowote ule ni wanafiki tu.
 
Back
Top Bottom