Mimi kila nikikukuruka nihame hii nchi naishia kutapeliwa ila ntaondoka tu.
Mi dume je wewe ni mke wa mtu au ni me ila wenzio wanakugeuza nimeshindwa kukuelewa?hahahahah mkuu njoo kwa mabaharia tukupeleke mambere lkn huko waweza kuwa mke wa mtu
Elfu 3 Kwa kilo au debe ?Pumba za kuku tulikuwa tunanunua 2000 sasa hivi elfu 3000 sijui tuendako
Jamaa yangu wewe ni mpiga dili ulizoea dili, mshahara unatosha sana haina haja kuongeza na wengine tunawapunguzia..
Wewe huoni midege inatua Chato pale, SGR, stiggler, shule bureee, ATCL imetua SA, uchumi unakua kwa 7% na umasikini umepungua, awamu ya tano inapiga kazi balaaa
Hahaa aisee....basi ngoja tukanunue ugali mboga itakua madege hayo kwenye bakuli
Mimi kila nikikukuruka nihame hii nchi naishia kutapeliwa ila ntaondoka tu.
Ha ha ha!!! Wafundishe kudanga!!!!Mfuko wa 50kgs chakula cha kuku umepanda toka 40,000/- hadi 45,000/-.Halafu kuku wangu wa kienyeji nimewazoesha kuwapa chakula hawajui kudanga !
Kweli ndio mana wanaake wengi wanaenda ulaya na uropa kutafuta maisha sisi wanaume tupambane tu hapahapa.Mwanamme hakimbii matatizo bali hupambana nayo labda vinginevyo utakuwa wakike....
Wakuu habari zenu poleni na majukum ya kitaifa
Kuna jambo limenishangaza sana mbona maisha yanazidi kupanda sana toka tarehe moja nimeenda dukani kununua sukari kilo moja kwetu huku ilikuwa tsh 2600 sasa hivi imefika 2800
Bati pia hivyo hivyo bando moja hizi za rangi nimekuta bei imepanda toka 370000 mpk 390000
Hizi za kawaida simbadum zimepanda toka laki mbili themanini mpaka laki tatu na arobaini.
Cement nayo imepanda hatari jamani tunaelekea wapi sasa mbona hatari hii kwa wafanyakazi kipato bado kile kile pia wafanyabiashara hali ya biashara ngumu
Hii hali hii mbona umri unaenda hatufanyi lolote la maana kwa ajiri ya watoto wetu zaidi ya kujibana kula na kuvaa napo kwa shida.
Huku naona hapajaguswa kabisaNiko na siku nyingi sijakanyaga bar. Vipi huko nako bei zimekwea ngazi?