Jamani mbona vitu vimepanda ghafla

Huu upandaji wa bei holela umefika anga za mateja? Au wao wanabwia kwa bei ile ile ?
 
Halafu unajiita member JF?
bure kabisa. Unaweza kuta mtu mwenye uchafu kichwani badala ya ubongo kama huyu anawajukuu
Sasa ulitaka ujibiweje kwan? Ujui mwaka wa bajet umeanza vitu vinaongezeka thamani ili walipa kodi waongeze mapato tujenge nchi maswali gan? Ayo unauliza uliza sukar kupanda mia mbili kelele acha ayo mambo ufanikiwe.
 
Njoo kakola namba mbili ubebe cargo za mawe. Kago moja ni buku mbili. Umbali wa dakika moja tu. Kaz nakupa Mimi hapa. Kama kuna ambae anaweza hiyo kaz na yupo namba mbili sasa hiv anichek. Kama kuna boda boda anaebeba mawe kutoka kakola kwenda nyarugusu pia anicheki. Mifuko minne ni 37elfu. Sio lazma uelewe
Asante mkuu sio kwa ujanja huo japo hela ngumu ila hiyo kazi ya kubeba makinikia si itanivunja kiuno mkuu nunua canter
 
Mfuko wa 50kgs chakula cha kuku umepanda toka 40,000/- hadi 45,000/-.Halafu kuku wangu wa kienyeji nimewazoesha kuwapa chakula hawajui kudanga !
Ni dhahiri na bei ya kuku itakuwa juu zaidi.
 
Nilimuuliza jamaa yangu hapo mtaani ana duka, akanambia kwa upande wa mazao tusubiri maumivu ya kutosha sababu wakulima wameruhusiwa kuuza nje mazao yao. Na kibaya zaidi mwaka huu mavuno ni hafifu.

Enewei, Mji umebaki mpweke, Faza kaenda Kijijini, Son kaenda Misri
 
Acha uvivu wewe, huo ugali ulionunua uliwezaje kuununua ushindwe kununua mboga, lakini sio lazima pia ule ugali na hapa ndipo inaonyesha namna ulivyoshindwa kuwa na kipaumbele.. Kuwa vegetarian tu mkuu achana na ugali huo nunua mchicha uchemche na maji ya bomba utafune shushia na ndizi mbili mbivu maji glasi mbili hapo poa kabisa tena diet ya uhakika kabisa hiyo.
Lazima kua vegetarian..unatupangia watanzania mboga ..unatupangia cha kula ..mna wazimu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom