Jamani mama yetu anaumwa sana-msaada

OME123

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,492
595
Ndugu zangu mama yangu anaumwa sana,tatizo lake anasumbuliwa na hedhi,kwani tangu mwezi wa saba alikuwa hajaona siku zake za hedhi,kwa sasa tatizo imeanza kama wiki mbili zilizopita anatokwa na mabonge ya damu ya hedhi mfululizo mpaka anaishiwa nguvu,jamani ndugu zangu wenye utalaam na haya mambo naombeni msaada kwani mpaka sasa hivi hali yake ni mbaya sana kwani nimechanganyikiwa jamani

natanguliza shukrani zangu
 

Pretty

JF-Expert Member
Mar 19, 2009
2,575
540
..........Itakuwa anaelekea menopause hiyo, muhimu hakikisha anakula chakula chenye madini ya iron kwa wingi.
Vile vile vizuri kwenda kumuona daktari wa magonjwa ya kike ili wamchunguze vizuri. Mpe mama pole, atakuwa vizuri tu.....mambo ya utu uzima hayo.
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,794
24,519
hilo suala la kuishiwa nguvu,linaashiria kua anahitaji kumuona daktari wa wanawake. lakini kama alivyosema pretty, damu ya hedhi kwa wingi na yenye mabonge inatokea wakati wa menopause. inaweza kuwa ni tatizo tofauti pia.poleni sana.
 

Azimio Jipya

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
3,363
1,124
Ndugu zangu mama yangu anaumwa sana,tatizo lake anasumbuliwa na hedhi,kwani tangu mwezi wa saba alikuwa hajaona siku zake za hedhi,kwa sasa tatizo imeanza kama wiki mbili zilizopita anatokwa na mabonge ya damu ya hedhi mfululizo mpaka anaishiwa nguvu,jamani ndugu zangu wenye utalaam na haya mambo naombeni msaada kwani mpaka sasa hivi hali yake ni mbaya sana kwani nimechanganyikiwa jamani


natanguliza shukrani zangu

Pole sana ... ! Sitegemei kuwa hujachukua hatua zozote ...hebu tueleze umechukua hatua gani hadi sasa ...!! Hospital ulizokwenda na majibu au ushauri uliopewa huko...

Karibu!!!
 

HAZOLE

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,552
693
baba, plz naomba umuone dr wa wanawake mapema. si tatizo kubwa sana maana sijajua anaumri gani but atakuwa fresh soon akipata dozi. usijali mwana.....hakuna kama mama na ndo maana umeongea kwa hisia kali, yaani mama ndo kila kila kitu.
 

Kayoka

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
2,085
1,514
Pole sana mkuu.! Hili tatizo la mama yako linanikumbusha tatizo la mke wa rafiki yangu ambaye kwa sasa ni marehemu kafark mwenzi wa 8 mwaka huu. Alikuwa anatokwa na damu ya hedhi kila cku halafu nyeusii, tuk.mpeleka mpaka kcmc wapi, muhimbili wapi, ocean road wapi mpaka kafia hapa nyumbani. Tutaja kugundua (japo siamini 50%) kumbe alirogwa. Rip Chausiku shemu wangu.
back to you: Nakushauri hangaika na mama hospitali zote na uwaone madaktari specialist wa magonjwa ya akina mama ikishindikana waone madaktari wa elimu dunia watamsaidia mama yako mpendwa. Pole sana.!
 

Kijuche

JF-Expert Member
Aug 26, 2010
418
35
Mpe pole sana mama ila ni vema akawahishwa hospitali ili akaonane na wataalamu wa hilo suala.
 

Sigma

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
5,009
1,249
Fibroid
Endometrial tumor
DUB
Peri-menopausal syndrome
Could be the problem. She should see a gynecologist.
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,347
17,368
ndugu zangu mama yangu anaumwa sana,tatizo lake anasumbuliwa na hedhi,kwani tangu mwezi wa saba alikuwa hajaona siku zake za hedhi,kwa sasa tatizo imeanza kama wiki mbili zilizopita anatokwa na mabonge ya damu ya hedhi mfululizo mpaka anaishiwa nguvu,jamani ndugu zangu wenye utalaam na haya mambo naombeni msaada kwani mpaka sasa hivi hali yake ni mbaya sana kwani nimechanganyikiwa jamani

natanguliza shukrani zangu

pole sana sana mkuu nasikia uchungu kwa matatizo ya mamaetu..ukiwa unamwamini mungu naomba mlete pale kwa gwajima
kanisa la ufufuo na uzima kawe uwanja wa tanganyika packers na mungu alie hai atamponya ..mamayangu alikuwa anaumwa sana sana mambo yao ya fibrous sijui kama nimepatia tulijua tunampoteza akiwa aghakan baada ya miaezi mitatu akaj mtu akamwombea akaniambia kuna siku ya maombi nimpeleke nikaomba hosp wakamkatilia nikamwomba dir wao akaenda kwenye maombi ndugu na imani ya mama ilimchukua wiki 2 dk wakauliza ule uvimbe umeenda wapi..na mpaka leo imebaki historia
 

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,485
15,211
Poleni sana. Mie sio daktari ila kwa ushauri mpelekeni hosipitali.
 

sweetlady

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
16,947
8,354
Poleni sana! Ni vizuri mkampeleka kwa daktari wa wanawake, naamin huko mtapata msaada zaidi. Mpeni pia juice ya rozela kwa wingi itamsaidia kuongeza damu inayopungua.
 

Laurence

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
3,104
418
Pole sana mpendwa,kwa sisi tuaminio,naendelea kufanya maombi kwa ajili ya huyo mama,pole Mungu atamsaidia
 

Kima mdogo

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
303
46
poleni sana wapendwa , dawa ya tatizo hili ni KUMWOMBA SN MUNGU NA KUFATA USHAURI WA DAKTARI.
 

Mupirocin

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,740
742
Please naomba kujua umri wa mgonjwa, afu tangu mwezi wa huo wa saba je hajakutana baba yetu? Na kama anaishiwa nguvu mpaleke hospital aongezewe damu. Jambo jingine afanye vipimo vifuatavyo UPT, abdomenal uss. Hii itatusaidia kujua kama alipata mimba na sasa imetoka coz hizo ndo dalili zake, pia tunajua kama ni fibroid, dysfunctional uterine bleeding (DUB) au cancer lakini nikijua umri wa mgonjwa itanarrow thinking yangu.
 

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,909
12,536
Kama walivyosema wachangiaji waliotangulia, mpeleke hospitali kwa madaktari wa magonjwa ya wanawake!
 

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
416
Huyo mama ana umri gani? Inawezekana anatumia uzazi wa mpango wa vipandikizi, mara nyingi tatizo hiln huwatokea wanawake wanaotumia njia hiyo ya uzazi wa mpango. Cha msingi ni kwenda kuwaona wataalamu mapema.
 

Mamzalendo

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,659
545
Mi sina msaada,lakini Pole sana mpe na mama pole,nitamuombea na naamini Mungu anasikia sala zetu atamponya,
 

OME123

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,492
595
Tafadhali dr g nipe number yako japo tuweze kuongea kwenye simu tafadhali,mama ana umri wa miaka 39 yrs
 

OME123

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,492
595
Please naomba kujua umri wa mgonjwa, afu tangu mwezi wa huo wa saba je hajakutana baba yetu? Na kama anaishiwa nguvu mpaleke hospital aongezewe damu. Jambo jingine afanye vipimo vifuatavyo UPT, abdomenal uss. Hii itatusaidia kujua kama alipata mimba na sasa imetoka coz hizo ndo dalili zake, pia tunajua kama ni fibroid, dysfunctional uterine bleeding (DUB) au cancer lakini nikijua umri wa mgonjwa itanarrow thinking yangu.
Tafadhali dr g nipe number yako japo tuweze kuongea kwenye simu tafadhali,mama ana umri wa miaka 39 yrs
 

OME123

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,492
595
Kibwenga mama yetu ana umri wa miaka 39,namba yangu ni 0714701242 au 0756777266 jamaani naombeni msaada pliz
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom