Jinsi Ya Kukabiliana Na Tatizo La Kuvurugika Mzunguko Wa Hedhi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
woman-in-blue-scrubs-with-hand-on-the-shoulder-of-a-woman-with-stomach-pain.jpg

TATIZO la kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi huwakumba wanawake wengi waliopo kwenye umri wa kuzaa au wale wanaokaribia kufikia ukomo wa hedhi.

Japokuwa wengine huchukulia tatizo hili kama kitu cha kawaida, kuvurugika kwa hedhi ni dalili kwamba kuna tatizo katika mfumo wako wa uzazi hivyo ni lazima uchukue hatua za haraka za kubaini tatizo hilo.

Kabla hatujaangalia tatizo lenyewe, ni vizuri tukatazama jinsi mzunguko wa kawaida wa mwanamke unavyotakiwa kuwa. Siku ya kwanza unayoona damu ya hedhi, kitaalamu ndiyo siku ya kwanza katika mzunguko wako.

Wapo wanawake wenye mzunguko mfupi na wapo wengine wenye mzunguko mrefu, wastani ukiwa ni siku 28. Hata hivyo, kitaalamu, mzunguko wa kawaida unajumuisha kuanzia wale wanaochukua siku 21 kukamilisha mzunguko mpaka wale wanaotumia siku 35.

Jambo la msingi la kuelewa ni kwamba urefu au ufupi wa mzunguko wako siyo tatizo, tatizo linakuja pale siku zinapopishana bila sababu ya msingi. Kwamba mwezi huu mzunguko wako umechukua siku 28, lakini mwezi unaofuata unachukua siku 32 na mwezi mwingine unaofuata unachukua siku 24.

Hapo ndipo penye tatizo, lakini hata kama mzunguko wako ni wa siku 32 lakini kila mwezi tarehe zinacheza hapohapo, basi hauna tatizo.

Wapo ambao wakati mwingine wanavusha hata mwezi mmoja au miwili bila kuona siku zao wakati hawana ujauzito, kama na wewe upo kwenye kundi hili basi tambua kwamba una tatizo ambalo ni lazima lishughulikiwe mapema.

CHANZO CHA TATIZO

Tatizo hili huweza kusababishwa na kuvurugika kwa mfumo wa homoni mwilini, hasa homoni au vichocheo vinavyoendesha na kudhibiti hedhi na uzazi kwa jumla.

Uwepo wa uvimbe ndani ya kizazi au kwenye vifuko vya mayai pia ni tatizo. Mabadiliko katika tabaka la ndani la kizazi, maambukizi sugu ya kizazi na kuharibika kwa mimba ni mojawapo ya matatizo haya yanayochangia siku za hedhi zitoke bila ya mpangilio.

Matumizi ya baadhi ya madawa huweza kuvuruga homoni na kusababisha matatizo haya.

DALILI ZA TATIZO

Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika kutofahamu mwenendo wa mzunguko wake, hulalamika damu kutoka muda mrefu au siku chache sana chini ya siku tatu, wakati mwingine hapati kabisa.

Anaweza kuwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu, maumivu wakati wa hedhi, maumivu wakati wa kujamiiana na hata damu kutoka mabonge au nyingi na nyepesi. Pia ataelezea ni muda mrefu anatafuta mtoto lakini hapati.

UCHUNGUZI

Tatizo hili humuathiri mwanamke kwa kiasi kikubwa hasa pale damu inapotoka kwa muda mrefu kwa zaidi ya siku saba au asipopata kabisa hedhi katika umri wake kama unamruhusu, pia mwanamke hatakuwa vizuri anapopata maumivu wakati wa hedhi, au anapotafuta mtoto halafu hapati ujauzito.

Uchunguzi hufanyika katika kliniki za madaktari bingwa wa akina mama katika hospitali za mikoa, vipimo mbalimbali vitafanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa. Vipimo pia vitazingatia mahitaji ya mwanamke kama yupo tayari kushika ujauzito kwa kipindi hicho. Kwa hiyo katika upimaji atachunguzwa na mfumo wake wa uzazi.

NINI CHA KUFANYA?

Ni vema mwanamke mwenye matatizo haya akazingatia ushauri wa daktari wake ili aweze kupona na kufanikiwa malengo yake ya kupata ujauzito. Baada ya uchunguzi wa kina ndipo utaratibu wa matibabu unaanza.

Mwanamke ambaye ameshafikia ukomo wa kuzaa yaani zaidi ya miaka arobaini na tano na ana matatizo haya basi azingatie sana uchunguzi na tiba.

Pamoja na kwamba tumeona vyanzo mbalimbali vya tatizo hili, lakini pia tusisahau saratani au kansa ya shingo ya kizazi, kwa ujumla vinabidi vichunguzwe kwani dalili zake hazitofautiani sana na matatizo mengine. Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba.
chanzo GBP.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom