Msaada wa kubadili umiliki wa umeme na maji unaponunua nyumba

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,037
2,953
Habari za muda huu ndugu zangu,

naombeni msaada wenu, nimenunua nyumba mwezi mmoja sasa hapa jijini dar es salaam, mita ya maji na lukuya umeme inasoma majina ya mwenye nyumba wa zamani (ambaye ameniuzia mimi), nilikuwa naomba utaratibu wa kufata ili niweze kubadili majina pamoja na namba ya simu ili niwe naweza kumenage mimi mwenyewe. Na naomba kujua atua zote izo zinghalimu kiasi gani na zinachukua muda gani, ili nitegene muda wa kufanya ayo yote maana nimekuwa ni mtu wa kusafiri sana .

Natanguliza shukrani zangu kwenu wadau
 
Fika kwenye mamlaka husika mfano nenda dawasa wata badili usajiri wako na tanesco
 
Kubadili jina la mita ya umeme nilifuatilia nikaona mlolongo mwingi nikaacha lilivyo, ishu ya maji ni kubadili tu namba ya simu ili meseji za Bill ziwe zinatumwa kwako
 
Kwa tanesco naona kuna ugumu ,na kufanikiwa ni ngumu sana,unless unabadili mita kabisa
Kwa ushauri tafuta fundi wa tanesco unaemjua mueleze kuna namna ya kuiusaidia wanajua
 
Nilikuwa kwenye mazingira yanayotaka kufanana na yako.

Mita ya maji ilikuwa na jina la mpangaji (alifanya mchakato wa kupata maji yeye)

Binafsi niliandika barua kwa Dawasa nikiomba jina la akaunti ya mita ya maji ibadilishwe.

Niliambatanisha;
1. Nakala la mkataba wa pango. Nilitaja
2. Akaunti namba ya mita
3. Namba ya simu
4. Majina kamili ya mmiliki

Bili za mwezi uliofuata zote zikawa zinakuja kwa namba niliyoorodhesha na kila kitu kikawa sawa.

Unaweza ukajiongeza kulingana na taarifa niliyokupatia na mazingira yako. Au nenda ofisi zao wakakupe utaratibu.
 
Back
Top Bottom