Nyuki wananisumbua sana - Naomba MSAADA wenu

Abdullah01

Member
Jul 5, 2023
14
36
Habari zenu ndugu zangu.

Hapa ninapoishi kuna nyuki wapo ndani ya ceiling board. Nimeshawahi kupuliza dawa ya Rungu na kuwaua wote.

Lakini kila bàada ya muda mfupi mfano mwezi wanahamia nyuki wengine, napuliza dawa wanakufa, halafu baada ya muda wanakuja wengine. Hawa waliokuja awamu hii ni wakali sana.
NAOMBA MSAADA WENU - kwa yeyote anayejua dawa ambayo nikiweka itatoa harufu ya kuwafanya nyuki wasije tena kukaa hapa walipozoea kuja kukaa.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.

ASANTE 🙏
 
Ungekuwa wewe ni muhaya, ningejua sababu na ningekupa mbinu. Ila kama sio Muhaya si rahisi sababu mambo mengine ni imani tu.

Hata hivyo kama ni Muhaya, hao nyuki hawawezi kuwauma familia yako wala wewe..
 
Back
Top Bottom