Jamani, kwani lazima?

Jamani, kwani lazima?

Duh! inamaana Daudi1 unatu taste patience amma?
Tupiamo ka hadihi bhana!
 
Last edited by a moderator:
JAMANI KWANI LAZIMA?-35

ILIPOISHIA
"Mwenzetu inaonekana una ahadi na baba Riziki, mbona umejipodoa hivyo?" alihoji Stela huku akiachia tabasamu laini na kumpapasa Mozie kifuani huku Paulina akishuhudia.
TAMBAA NAYO MWENYEWE...


"Nadhani Stela unapitisha utani kwa mwenzako," alisema kwa ukali Mozie...
"Utani kivipi, kwani si kweli?""Ingekuwa kweli angekuja kukaa hapa sebuleni?"
Stela alibaki kimya lakini Paulina yeye ndiye alikuwa kimya zaidi kwani hata Stela wakati anazungumza hakumjibu kitu chochote zaidi ya kumtazama tu.

"Vitu vingine vina wakati wa kuongea na wakati siyo wa kuviongea, baba Riziki alikuja hapa tukazungumza na wewe ukiwepo. Kilichoongelewa ulikisikia sasa kwa nini unasema hivyo?" alihoji mume wa Paulina.

Paulina mwenyewe alisema...
"Kumbe huyu binti kama nitaamua kumvumilia naweza kuisimamisha ndoa yangu kama mwanzo. Nahisi anaropoka sana na kuropoka kwake Mozie hapendi," alisema moyoni Paulina huku macho yake yakiwa kwenye runinga...

"Mpira wa leo kiboko, hawa Man U wanaweza kufungwa sana," alisema Paulina akijifanya ameachana kabisa na mawazo kuhusu Stela aliyetaka kumpakia kwa maneno mengi mpaka akaingilia Mozie...
"Aaah! Wapi?" alidakia Mozie huku akitingisha kichwa kwamba, Man U hawawezi kufungwa.
Mazungumzo kuhusu mpira kati ya Paulina na mumewe yalikwenda vizuri kiasi kwamba, Stela alianza kusikia kero kwani alichotaka yeye ni kuona hakuna maelewano kati ya wawili hao.

"Baby mimi nakwenda kulala sasa," alisema Stela, akaendelea...
"Nataka kujua katika zamu za kulala utaanzia wapi?" Stela alimuuliza Mozie akiwa ameshasimama...
"Mimi ndiye nitakayepanga, ukiona sijaja kwako ujue nimeanza kwa Paulina, ukiona nimekuja ndiyo wewe unakuwa wa kwanza."

Stela alijikongoja na mtumbo wake hadi chumbani kwake na kumwacha Paulina na Mozie...
"Sina wasiwasi sasa, ilimradi Paulina amejua mimi ni mke mwenzake. Natakiwa kuwa na haki zote kama mke. Kwanza nimemzidi, mimi ni mama kijacho yeye hamna kitu," alisema Stela mle chumbani akiwa ameshapanda kitandani kulala, tena alilala akiangalia juu yaani chali!
"Baby na mimi nakwenda kulala," alisema Paulina kwa sauti iliyojaa mawazo...
"Poapoa."

Mozie alibaki sebuleni lakini hakuna aliyemwambia kwamba siku ile angeanza kulala kwake.
Alijawa na mawazo hata kuangalia tivii kwake ilionekana kama upuuzi mkubwa. Alifikiria hatua aliyoichukua na msimamo wa busara zake akagundua kuwa, alikuwa sahihi kwa vile moyo wake ulikuwa na amani.

Katika kuzama zaidi kwenye mawazo, Mozie alijikuta akipitiwa na usingizi na kuanza kukoroma palepale sebuleni.Ilikuwa saa saba na nusu, Paulina alishtuka usingizini na kugundua kuwa, kitandani alikuwa peke yake...

"Mh! Ina maana ameamua kuanza na Stela?" alijiuliza mwenyewe pale kitandani.
Aliamka, akatoka kitandani kwa lengo la kwenda sebuleni kuangalia...
"Kama ameanza na Stela atakuwa amempa kichwa sana. dawa ya Stela ni kuwekwa nyumanyuma kwa kila kitu," alisema moyoni Paulina akifungua mlango wa chumbani kwake.

Kumbe wakati yeye ameamka, Stela naye kule chumbani kwake alishtuka kutoka usingizini, akagundua amelala peke yake. Alipoangalia simu yake ya mkononi alibaini ni saa saba usiku...
"Mh! Ina maana baby wangu kaanza zamu kwa kulala na Paulina? Poa tu lakini si vizuri ajue Paulina huyohuyo ndiye aliyemsaliti kwa baba Riziki...

"Ngoja nikamwangalie sebuleni, labda bado anaangaliza tivii," alisema moyoni Stela akitoka kitandani.
Paulina alipokaribia kutokea sebuleni, alisimama na kuchungulia, akamwona Mozie amelala na anakoroma. Lakini kabla hajawaza lolote, akamwona Stela naye anachungulia kwa upande aliotokea chumbani kwake, naye alisimama.

Paulina kumwona Stela aliamua kujitokeza kabisa kumfuata mumewe, Stela naye alifanya vivyo hivyo. Walijikuta wote wamefika na kusimama kwa Mozie...
"Baby...we baby," aliamsha Paulina...

"My love...mume wangu," Stela naye hakubaki nyuma kumwamsha Mozie. Ni kama walikuwa wakimgombea maana mwingine alitingisha mabega, mwingine kifua...
"M...m..." Mozie alikurupuka usingizini, akakaa akishangaashangaa na kuwaangalia wanawake zake hao...
"Mbona unalala sebuleni mume wangu?" aliuliza Paulina...
"Twende ukalale ndani baba kijacho," alisema Stela akimshika mkono...
"Ngojeni kwanza, mimi nitaamua nakwenda kulala wapi leo. Stela we kalale, nitakuja."

Stela aliondoka kwa kusikiliza neno ‘nitakuja'. Paulina naye aliondoka akijua si zamu yake kuanzia siku hiyo.
Mozie alijinyoosha akasimama, anaenda chumbani kwa Paulina.
Paulina alishtuka kwanza, alijua Mozie ameingia kuchukua shuka ili akalale kwa Stela lakini alipomwona anavua nguo na kujipakia bukta kisha anapanda kitandani alijua kumbe amechaguliwa kuwa wa kwanza.
***
Saa tisa usiku, Stela alishtuka kutoka usingizini, akajikuta yupo peke yake kitandani, akakasirika sana. alitoka kitandani kwa lengo la kwenda kumbeba Mozie na kumwingiza chumbani kwake japokuwa nguvu hizo hakuwa nazo...

"Yaani huyu ameanza tabia gani ya kulala sebuleni?" alisema Stela akifungua mlango wa chumbani kwake na kwenda sebuleni...
 


JAMANI KWANI LAZIMA?-36

ILIPOISHIA
akakasirika sana. Alitoka kitandani kwa lengo la kwenda kumbeba Mozie na kumwingiza chumbani kwake japokuwa nguvu hizo hakuwa nazo...
"Yaani huyu ameanza tabia gani ya kulala sebuleni?" Alisema Stela akifungua mlango wa chumbani kwake na kwenda sebuleni...
ENDELEA KIVYAKO...
Khaa! Yuko wapi sasa? Au amekwenda kulala kwa Paulina? Si alisema atakuja kwangu? Ndiyo nini sasa?" Alijiuliza Stela na kuamua kwenda moja kwa moja chumbani kwa Paulina ili kujua kama Mozie alikuwa kule au la!

"Ngo...ngo...ngo," Stela aligonga mlango kwa nguvu...
"Atakuwa nani huyo?" Aliuliza Paulina...
"Ndani ya nyumba hii tupo wawili, unadhani atakuwa nani kama siyo Stela?" Alijibu mumewe...
"Ngo...ngo...ngo," Stela aliendelea kugonga mlango.

Mozie alitoka kitandani, akiwa ndani ya bukta akafungua mlango...
"Mume wangu kwani umeamua kuanza zamu kwa mwenzangu au amekulazimisha?" Alihoji Stela...
"Stela," aliita Mozie...
"Abee."

"Unajua kwa siku mbili tu nimekugundua wewe ni bogasi kabisa. Sasa sikia, sitaki niwe mume wako wala shemeji. Kama ni mtoto utazaa, nitamhudumia lakini mapenzi mimi na wewe mwisho leo."

Paulina alitoka kitandani haraka sana baada ya kusikia kauli ya Mozie, hakuamini...
"Baby, mbona unamjibu vibaya Stela?" Aliuliza Paulina akijifanya yeye ni mwema.
"Namshangaa mke mwenzangu, hivi anaweza kunijibu mimi maneno machafu kama hayo. Eti mimi bogasi, bogasi mwenyewe bwana."

Hasira zilizidi kumpanda Mozie akamrushia kofi lakini Paulina aliliwahi kulizuia...
"Paulina niache nimshughulikie huyu. Kwanza nimegundua nimedili na mtu asiye na akili timamu. Hivi we uliona alivyokuwa akizungumza mambo ya kijinga kuhusu wewe pale sebuleni? Anasema una ahadi na baba Riziki. Mara anasema sijui utumbo gani, mpaka nikamsema."
"Sasa wewe unakerwa na nini niliposema Paulina anakwenda kwa baba Riziki, si alikuwa anakwenda kweli. Kwani uongo? Sema una lako jambo, umeshanipa mimba sasa unajiandaa kunitelekeza," alisema kwa hasira Stela.

"Stela sikia, nenda kalale, mimi nazungumza kama dada yako sasa. Kalale asubuhi sana tutazungumza."

Stela aliondoka, akaenda kulala. Asubuhi kulipokucha, Mozie aliweka kikao kizito cha watu watatu, akaweka msimamo wake kwamba, yeye na Stela ibaki kuwa historia.
"Na nataka nikwambia ukweli kwamba, wewe kaa hapa mpaka ujifungue. Kila kitu utapata..."
"Na hata ukishajifungua utaendelea kukaa hapahapa mpaka mtoto akue," alidakia Paulina. Stela alikuwa mpole baada ya kugundua kuwa, Mozie alikuwa siriasi na uamuzi wake.

Aliamini kitendo chochote kile cha kutaka kuweka ukorofi angeweza kukosa bara na pwani...
"Sawa," alijibu kwa upole Stela.
"Na sitapenda kusikia unamjibu vibaya Paulina, ni bosi wako kama zamani. Hii chukulia ni agizo na msimamo wangu kwako, sawa?"
"Sawa."

Saa kumi jioni ya siku hiyo, Stela alishikwa na uchungu akakimbizwa hospitali na Paulina kwenda kujifungua. Paulina alikaa nje baada ya Stela kupokelewa.
Baada ya kama saa tano kupita, nesi mmoja alitoka nje kwa Paulina...
"Dada mgonjwa wako ameshajifungua," alisema yule nesi akimwambia Paulina...
"Kweli, mtoto gani?"

"Wa kiume. Kwani baba wa mtoto ni Mwarabu?"
"Mwarabu?! Hapana, kwani vipi?" Aliuliza kwa mshtuko Paulina...
"Mtoto ni Mwarabu kwa asilimia mia moja. Una maana baba yake ni mswahili?" Nesi aliuliza...
"Si mswahili tu, ni mweusi japo si sana lakini ni mweusi wala si maji ya kunde," alisema Paulina huku moyoni akiombea uarabu wa mtoto huyo usipinduke hata marra moja.
"Hii kwangu poa sana, Mwarabu? Ina maana Stela alikuwa anatembea na Mwarabu. Lakini ni Mwarabu gani atakuwa?"

Paulina aliingiza wodini ambako Stela alihamishiwa baada ya kujifungua...
"Hongera sana Stela," alisema Paulina.
"Asante sana."
"Hebu mfunue nimwone kidogo."
Stela aligoma kumfungua sura mtoto huyo...
"Sitaki."

"Khaa! Kisa nini?"
"Nimesema sitaki umbeya wako."
Baadhi ya wazazi waliokuwa hapo kwa ajili ya uzazi nao walishangaa sana, akiwemo nesi aliyemwita Paulina...
"We dada mbona sikuelewi. Huyu si ndiye amekuleta?" Alihoji nesi...
"Hata kama," alijibu Stela kwa sauti yenye dalili ya kiburi.
Paulina palepale aliondoka, aliamua kurudi nyumbani...
"Vipi za huko?" Mozie alimuuliza...
"Mwenzangu mbaya."

"Ubaya wake nini?"
"Stela amejifungua mtoto wa kiume, lakini nilipoingia wodini amenigomea kumwona mtoto."
"Kwa nini kagoma?"
"Mtoto Mwarabu."
"Mtoto Mwarabu?"
"Mwarabu ndiyo."

"We Paulina mwongo. Ulijuaje ni Mwarabu kama alikukatalia usimwone?"
"Aliniambia nesi."

***
Kesho yake saa tano asibuhi, Stela aliingia nyumbani hapo akiwa na mtoto wake huku akiangua kilio.
ITAENDELEA IJUMAAA...................
 
Daud one jaman.... hv uko wapi uwiii
Aiseeeee jamani poleni sana mtandao wa tigo umenifanyia yote haya nimejiunga bando la mwezi sasa toka alhamis network inasumbua sana sijui kuna shida gani nisameheni bure tu
 
Mkuu Daudi1 vp mbona kimyaa!? Leo ni ijumaa mkuu njoo ulete mambo huku.
Dah! mkuu sorry sijaweka toka ijumaa network ya tigo ilikuwa mbovu hivyo nikashindwa ila nimeweka zote mbili endele kupata uhondo
 
Jamani naomba mniwie radhi tu nilishindwa kuendeleza kutokana na tatizo la mtandao wa tigo toka jumatano, atleast leo umekaa vizuri ndo maana nimeweza kuzitupia
 


JAMANI KWANI LAZIMA?-36

ILIPOISHIA
akakasirika sana. Alitoka kitandani kwa lengo la kwenda kumbeba Mozie na kumwingiza chumbani kwake japokuwa nguvu hizo hakuwa nazo...
“Yaani huyu ameanza tabia gani ya kulala sebuleni?” Alisema Stela akifungua mlango wa chumbani kwake na kwenda sebuleni...
ENDELEA KIVYAKO...
Khaa! Yuko wapi sasa? Au amekwenda kulala kwa Paulina? Si alisema atakuja kwangu? Ndiyo nini sasa?” Alijiuliza Stela na kuamua kwenda moja kwa moja chumbani kwa Paulina ili kujua kama Mozie alikuwa kule au la!

“Ngo...ngo...ngo,” Stela aligonga mlango kwa nguvu...
“Atakuwa nani huyo?” Aliuliza Paulina...
“Ndani ya nyumba hii tupo wawili, unadhani atakuwa nani kama siyo Stela?” Alijibu mumewe...
“Ngo...ngo...ngo,” Stela aliendelea kugonga mlango.

Mozie alitoka kitandani, akiwa ndani ya bukta akafungua mlango...
“Mume wangu kwani umeamua kuanza zamu kwa mwenzangu au amekulazimisha?” Alihoji Stela...
“Stela,” aliita Mozie...
“Abee.”

“Unajua kwa siku mbili tu nimekugundua wewe ni bogasi kabisa. Sasa sikia, sitaki niwe mume wako wala shemeji. Kama ni mtoto utazaa, nitamhudumia lakini mapenzi mimi na wewe mwisho leo.”

Paulina alitoka kitandani haraka sana baada ya kusikia kauli ya Mozie, hakuamini...
“Baby, mbona unamjibu vibaya Stela?” Aliuliza Paulina akijifanya yeye ni mwema.
“Namshangaa mke mwenzangu, hivi anaweza kunijibu mimi maneno machafu kama hayo. Eti mimi bogasi, bogasi mwenyewe bwana.”

Hasira zilizidi kumpanda Mozie akamrushia kofi lakini Paulina aliliwahi kulizuia...
“Paulina niache nimshughulikie huyu. Kwanza nimegundua nimedili na mtu asiye na akili timamu. Hivi we uliona alivyokuwa akizungumza mambo ya kijinga kuhusu wewe pale sebuleni? Anasema una ahadi na baba Riziki. Mara anasema sijui utumbo gani, mpaka nikamsema.”
“Sasa wewe unakerwa na nini niliposema Paulina anakwenda kwa baba Riziki, si alikuwa anakwenda kweli. Kwani uongo? Sema una lako jambo, umeshanipa mimba sasa unajiandaa kunitelekeza,” alisema kwa hasira Stela.

“Stela sikia, nenda kalale, mimi nazungumza kama dada yako sasa. Kalale asubuhi sana tutazungumza.”

Stela aliondoka, akaenda kulala. Asubuhi kulipokucha, Mozie aliweka kikao kizito cha watu watatu, akaweka msimamo wake kwamba, yeye na Stela ibaki kuwa historia.
“Na nataka nikwambia ukweli kwamba, wewe kaa hapa mpaka ujifungue. Kila kitu utapata...”
“Na hata ukishajifungua utaendelea kukaa hapahapa mpaka mtoto akue,” alidakia Paulina. Stela alikuwa mpole baada ya kugundua kuwa, Mozie alikuwa siriasi na uamuzi wake.

Aliamini kitendo chochote kile cha kutaka kuweka ukorofi angeweza kukosa bara na pwani...
“Sawa,” alijibu kwa upole Stela.
“Na sitapenda kusikia unamjibu vibaya Paulina, ni bosi wako kama zamani. Hii chukulia ni agizo na msimamo wangu kwako, sawa?”
“Sawa.”

Saa kumi jioni ya siku hiyo, Stela alishikwa na uchungu akakimbizwa hospitali na Paulina kwenda kujifungua. Paulina alikaa nje baada ya Stela kupokelewa.
Baada ya kama saa tano kupita, nesi mmoja alitoka nje kwa Paulina...
“Dada mgonjwa wako ameshajifungua,” alisema yule nesi akimwambia Paulina...
“Kweli, mtoto gani?”

“Wa kiume. Kwani baba wa mtoto ni Mwarabu?”
“Mwarabu?! Hapana, kwani vipi?” Aliuliza kwa mshtuko Paulina...
“Mtoto ni Mwarabu kwa asilimia mia moja. Una maana baba yake ni mswahili?” Nesi aliuliza...
“Si mswahili tu, ni mweusi japo si sana lakini ni mweusi wala si maji ya kunde,” alisema Paulina huku moyoni akiombea uarabu wa mtoto huyo usipinduke hata marra moja.
“Hii kwangu poa sana, Mwarabu? Ina maana Stela alikuwa anatembea na Mwarabu. Lakini ni Mwarabu gani atakuwa?”

Paulina aliingiza wodini ambako Stela alihamishiwa baada ya kujifungua...
“Hongera sana Stela,” alisema Paulina.
“Asante sana.”
“Hebu mfunue nimwone kidogo.”
Stela aligoma kumfungua sura mtoto huyo...
“Sitaki.”

“Khaa! Kisa nini?”
“Nimesema sitaki umbeya wako.”
Baadhi ya wazazi waliokuwa hapo kwa ajili ya uzazi nao walishangaa sana, akiwemo nesi aliyemwita Paulina...
“We dada mbona sikuelewi. Huyu si ndiye amekuleta?” Alihoji nesi...
“Hata kama,” alijibu Stela kwa sauti yenye dalili ya kiburi.
Paulina palepale aliondoka, aliamua kurudi nyumbani...
“Vipi za huko?” Mozie alimuuliza...
“Mwenzangu mbaya.”

“Ubaya wake nini?”
“Stela amejifungua mtoto wa kiume, lakini nilipoingia wodini amenigomea kumwona mtoto.”
“Kwa nini kagoma?”
“Mtoto Mwarabu.”
“Mtoto Mwarabu?”
“Mwarabu ndiyo.”

“We Paulina mwongo. Ulijuaje ni Mwarabu kama alikukatalia usimwone?”
“Aliniambia nesi.”

***
Kesho yake saa tano asibuhi, Stela aliingia nyumbani hapo akiwa na mtoto wake huku akiangua kilio.
ITAENDELEA IJUMAAA...................

Mamaaaa mtoto mwarabu atakua Wa Daudi1
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaa nilisema mimi mke mkubwa ni mkubwa tu ..... stella anakiherehere na yamemchwea vibaya hapa nimefurah haswaaaaaa Daudi1
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom