JAMANI KWANI LAZIMA?-33
ILIPOISHIA
Lakini mume wangu mimi kwangu afadhali ungetembea na mwanamke mwingine wa mtaani kuliko msichana wangu wa kazi.
Mimi kwa upande wangu afadhali ungetembea na msukuma mkokoteni kuliko baba Riziki.
ENDELEA KIVYAKO...
Maneno yale yalimfanya Paulina azidi kunyongonyea, hakuwa na la kujibu zaidi ya kumkodolea macho Mozie aliyekuwa akiendelea kupaki zile nguo zake kwenye begi.
Mume wangu!
Nani mume wako? Nimesema naondoka kamwite baba Riziki na mimi niondoke na Stela wangu.
Stela wako?Ndiyo Stela mke wangu aliyenijaalia kubeba mimba yangu.
Ndiyo baby! Alidakia Stela na kumfanya Paulina amuangalie kwa jicho la kukata.
Baby muda unakwenda... aliongea Stela kiuchokozi.
Nyamaza huko, unajua muda wewe!
Paulina unamwambiaje mke wangu mtarajiwa?
Paulina aliishiwa nguvu kwa mara nyingine, aliinua ile karatasi aliyopewa na Mozie, karatasi iliyokuwa na makubaliano ya kutoa mimba kati yake na baba Riziki kisha akaiangalia huku chozi likitaka kumuwahi.
***
Muda wote baba Riziki masikio na macho yake yalikuwa na hamu ya kutaka kujua kinachoendelea ndani ya nyumba ya Mozie. Roho ya umbeya ikamtawala na kuamua kufunga safari hadi kwa Mozie.
Hodi wenyewe!
Harakaharaka, Stela akachomoka na kukimbilia sebuleni kufungua mlango baada ya kuisikia ile hodi.
Wenyewe wapo?Wenyewe ndiyo sisi anamwitaji nani?
Sema shida yako kwani hata mimi ni muhusika?
Basi namhitaji Mozie, nataka kujua kama Paulina kazinduka?
Paulina yule mkeo ambaye ulimpa mimba mkaandikishana?
Stela alianza kuonyesha maudhi kwa baba Riziki.
Nani huyo anabisha mke wangu? Sauti ya Mozie ilisikika ikitokea chumbani.
Baba Riziki!Anasemaje? Amekuja kumchukua mkewe Paulina?
Ndiyo
Maneno yale kutoka kwa Stela yakamfanya Paulina kudondoka kwa mara ya pili na kuzimia, akapoteza fahamu. Roho ya kikatili ikamnyemelea Mozie na kujikuta baada ya kumpatia huduma ya kwanza akamburuta hadi sebuleni huku Paulina akiwa hajielewi.
Mzazi mwenzangu vipi tena nimesikia kishindo tu?
Nashukuru umelitambua hilo mzazi mwenzangu, huyu hapa anasingizia tu hapa alipo hajazimia wala nini, kakusikia umekuja anajifanya amezimia, yote haya yametokea baada ya kumuonyesha ile karatasi niliyochukuwa kwako.
Ahhh umeharibu mzazi mwenzangu!
Sikia nikwambie baba Riziki, tumeishi kwa muda mrefu kama majirani na kosa ulilofanya umenikosea sana, haina jinsi kwa sababu kama kulipiza nimeshalipiza kwa huyu mke wangu mtarajiwa, Stela.
Aliongea Mozie huku akimsogelea Stela na kumkumbatia sambamba na kutoa mabusu yasiyo na idadi.
Mozie alishtuka Paulina. Maneno yote aliyokuwa akiyaongea mumewe, Mozie yalikuwa yakimuingia akilini lakini kitendo cha kuyaona mabusu kwa jicho la kuibia akiwa pale chini kilimfanya kushtuka, akainuka.
Mozie, hunitendei haki kabisa!
Unataka haki gani? Mumeo huyu hapa wala usizuge kwa lolote, mchukue uondoke naye au niwaache mimi niondoke.
Tuwaache sisi tuondoke! alidakia Stela.
Safari hii, Mozie hakutaka mzaha hata kidogo, alitaka kumwonyesha Paulina kuwa ana uwezo wa kumfanyia jeuri na vilevile akaishi na wote wawili.
Alichokifanya alimgeukia baba Riziki kisha akatoka nduki hadi chumbani na baada ya dakika chache akarudi na begi lake kubwa lililokuwa na nguo zake ndani.
Baba Riziki kuanzia sasa nimekuachia mke wangu rasmi, sipo tayari kuandikishana kumchukua kama mlivyofanya ulivyomtundika mimba ila niliye naye huyu anatosha.
Hapana, hapana usifanye hivyo Mozie, naomba tupate usuluhishi juu ya hili.
Usuluhishi wa nini tena?
Mkeo!
Siyo mke wangu tena huyo ni wako, mimi mke wangu huyu hapa Stela.
Stela akajisogeza kwa ukaribu tena, Paulina hakuwa na cha kuongeza zaidi ya kusikia utetezi kutoka kwa baba Riziki.
Sikilizeni niwaambie? Mozie alishusha pumzi.
Kila mtu ana kosa kwa hilo inabidi lieleweke, sawa!
Sawa! aliitikia Paulina harakaharaka akijua msamaha unaenda kutoka.
Ninachotaka hapa mbele ya baba Riziki, Paulina kachukue kalamu na karatasi ndani. Paulina alitoka mbio na kurudi navyo.
Paulina, baba Riziki, Stela na mimi nataka tukubaliane hapa kwa maandishi. Nitaandika kuwa nipo tayari kuishi na wake wawili yaani Stela na Paulina na wewe baba Riziki utaweka sahihi kama shahidi sawa?
Sawa, aliitikia baba Riziki baada ya kuona maji yamefika shingoni.
Mozie aliandika harakaraka, baba Riziki akatia sahihi kukubaliana na yale maandishi.
Tumemalizana sawa! Stela peleka mizigo yako chumbani kwako na wewe Paulina peleka ya kwangu chumbani kwako, kuanzia sasa nikitaka kulala chumba cha Stela ruksa na nikitaka kulala kwangu na Paulina ruksa, sawa!
Baby mimi wala sina kinyongo kwa hilo niko sawa, na hiki kiumbe?
Hiyo ni mali yangu na tutamlea wote pamoja na Paulina, kuanzia sasa wewe si mfanyakazi bali mke wa pili kama nilivyoandika hapa!
ITAENDELEA JUMATATU...................................