Jamani kuna uwezekano wa mtu kupata chat zangu za watsap without my information

Usiseme hana confidence sema ameloose trust on you.

Unakuwaje confident na mtu anae kuchezea akili....?!
Ukishaona humuamini mtu ni bora kuachana nae. Mahusiano sio jela ya maisha useme huna la kufanya.
Heri kukaa pembeni mapema kuliko kuliko kutafuta sababu za kuchomana na gunia2 za mkaa
 
Of course. Ila muda mwingine mtu anatafiti ili kupata ushahidi maana unaweza fanya maamuzi ya haraka unakuja gundua mtu hakuna baya alikuwa anakufanyia sema alikuwa hayupo comfortable kukuonyesha anachofanya pengine utamjudge tofauti. So ni sawa kumchunguza mtu.

Nitakupa mfano. Kuna jamaa aliona mke wake yupo busy na mtu wanachat sana, na hali fulani za usiri mwingi. Akahisi pengine ana mtu wa nje. Mwisho wa siku akamlipa private Investigator afuatilie ampe report.

Yule P.I kweli akaja na report ya awali kuonyesha bidada anaonana na mtu kwa siri.

Siku moja jamaa akapata report ya P.I kuwa mke wake anakwenda kwenye hotel moja ya gharama ameingia na yule jamaa.

Jamaa kwa mahasira akafura akamwambia yule P. I kuwa ampe address ya hiyo hotel. Then aende akafanye yake. Jamaa amefika kwenye hotel kweli akaona gari ya nyumbani ipo hapo kwenye hotel imepaki.

Akaingia ndani kwa hasira na kuanza kukikirishana na uongozi ambao waligoma kumpa ushirikiano kutokana na jazba aliyokuwa nayo.

Huku na kule mkewe anashuka katika elevator anakuja na jamaa. Mshikaji akawavaa anataka kuanzisha varangati na kuwasha moto. Huku na kule akamtolea maneno makali mkewe akapita hivi bila hata kumsikiliza, on the way aligonga gari ya mtu na kifupi siku ikawa mbaya kwa jamaa.

To cut the story short, jamaa baadae mkewe akamtumia ujumbe kuwa alikuwa anaandaa mazingira ya kumsuprise sababu anniversary yao imeshafika kesho yake na ni birthday yake pia. Pale hotelini alikwenda kufanya booking ya chumba ambacho alikuwa anakiandaa sababu ya siku hiyo ambayo yeye alitaka iwe siri amsuprise. Na yule mwanaume ni designer pia ni muandaaji wa matukio kama hayo ya kuvishana Pete, birthday parties na babyshowers.

Jamaa kweli aliporejea home mkewe kamuonyesha details zote. Jamaa akajua alibugi wapi.....
 
Ukishaona humuamini mtu ni bora kuachana nae. Mahusiano sio jela ya maisha useme huna la kufanya.
Heri kukaa pembeni mapema kuliko kuliko kutafuta sababu za kuchomana na gunia2 za mkaa
Sasa angesema amuache mkewe bila kujipa ushahidi unadhani ingekuwa ni busara.
 
Kindly let me go straight to the point,

Jamani kuna uwezekano wa mtu kupata chat zangu za watsap without my information.

I feel like nachunguzwa

My concerns ni je kweli inawezekana?bila mtu kushika simu yangu anaweza kupata chat zangu za whatsap. Muhusika ni mtu wa IT
Ameshawahi kuniambia nikifanya madudu atayajua tu na atanionyesha ushahidi.

I have been flirting here and there, sasa ameanza maneno kama vile anajua ninacho kifanya. Kama Kuna uwezekano wa kuzuia asione chats zangu pia I will be glad if I get any help.

Thank you
Shida yote ya nini!? Tumia kitochi!!
 
Yeah healthy on your way to cheating you useless cunt. The problem is you are not life focused, u like games while life is happening.

U should know better. If u want to flirt then admire your man and flirt with him and only him.
Useless cunt ni ya mama yako tu, yangu inatumika kama ilivyokusudiwa.
 
Wevuna ukichopanda, maana mwana kulitafuta umelipata.
Na kwanini usibaku njia kuu..
 
Hizi habari za kudukuana nazionaga za kitoto sana. Ukiona mtu kaanza kukudukua hana confidence na wewe na hapa najiuliza kwanini asikuache tu
.
Sielewagi kwanini mtu uendelee kuwa kwenye mahusiano unayoingia gharama kubwa kuyabomoa zaidi ya kuyajenga
Kwa nini ucheat? why aisee kuwa tu makini kama hamuhitaji huyo mtu acha kabisa nadhani hujawahi fahamu maumivu ya mpenzi, mme au mke kucheat na mwenzi wake akajua. Let me give you my own story, nilioa mwanamke baada ya miaka minne ya ndoa na tayari tukawa tuna watoto wawili niliamua kwenda kuongeza elimu kidogo, hivo nikatoka Arusha kuja Dar. Nikiwa chuoni mwaka wa pili mke wangu mienendo ikaanza kubadilika, kila Alhamis bibie ukipiga simu usiku hayuko nyumbani, ukiuliza anakwambia niko kwenye sendoff, sendoff kila wiki wewe ni MC hapana,
Kwa nini sendoff kila mara? siku ya siku bana kajichanganya katuma message kwa shogake mmoja hivi, nayo ilikuwa inasema ulivosema habari ya taulo nikambukua....... kataja jina la mtu fulani. Ghafla kengele ikalia kichwani ikabidi nimbane hakunyoosha maelezo. Nilichofanya nikasafiri kwenda Arusha ghafla, nilivofika kitu cha kwanza nikateka simu kwa muda wa wiki. Niliyokutana nayo yalikuwa yanafurahisha, mke wangu alikuwa na danga moja, na sponsor. Nikiwa nimeshika simu ikatumwa shiingi milioni laki tano kwa Mpesa, na message iliyokuwa inasema hiyo fanya shoping ujiandae ili nikupeleke kwa wazazi,
Sijamaliza task yangu ikaja sms nyingine hii ni kutoka kwa mtu mwingine ikilalamika kwa nini siku hizi anapigwa chenga, kipindi chote hiki nilichoshikilia simu mke alikuwa anaingia ndani anatoka, anaingia ndani anatoka kwa siku anaweza kufanya hivo hata mara hamsini.
Baada ya kugundua kuwa anacheat nikaamua nimwulize mke wangu ni kwa nini uliamua kutoka nje ya ndoa na kujitambulisha kuwa hujaolewa mpaka mtu anatangaza uchumba, nawe ukakubali.
Sikuwa mkali nikamwambia mpangie huyo jamaa yako siku ya kwenda kukutambulisha kwao, lakini umwombe wewe ndo uanze kwenda kumtambulisha. Nikiwa nimeshika sime mkononi nikamwambia piga simu sasa hivi kwanza kwa huyo bwanako mwambie siku fulani twende nikakutambulishe nyumbani. Simu ya pili mpigie babako na mamako uwaambie siku fulani nakuja kumtambulisho mchumba.
Akajifanya naomba unisamehe nikamwambia nahesabu mpaka tatu natenganisha kichwa na mwili alafu baadae hicho kitobo naingiza kisu nachanachana kama karatasi.
Akapiga simu kwa huyo mtu akamwambia naomba mimi ndo nianze kwenda kukutambulisha, kukawa na mvutano lkn jamaa akagundua kama anaongea kwa wasi wasi. Akauliza mbona kama haujiamini leo nikachukuwa simu nikamwambia huyo jamaa mheshimiwa huyu unayeongea ni mke wangu wa ndoa na nashukuru kwa hii milion moja na laki tano uliotuma.
Kuhusu wazazi wake aliniomba sana asiwapigie kwa sababu mamake ana pressure na angeweza kufa. Baada ya kutafakari nikaona sawa. Baada ya kukamilisha uchunguzi wangu usiku huohuo nikawaaga watoto wangu nikawambia naarudi Dar.
Kilichofuata ni sms na simu kila dakika kila siku.
nisiwachoshe lakini. Usiombe ukasalitiwa na mme au mke unayempenda.
 
Back
Top Bottom