Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,270
- 9,716
Ndugu zangu watanzania,
Kwa sasa hali ni mbaya sana sana ndani ya CHADEMA ,chama kimepasuka na kugawanyika vipande vipande.hakuna maelewano,hakuna mipango wala mikakati ya pamoja,hakuna mshikamano wala umoja wa wanachama na viongozi ndani ya chama hicho,hakuna Dira wala muelekeo wa pamoja wala lugha ya pamoja ndani ya nyumba hiyo.
Hakuna sera za pamoja,hakuna ajenda za pamoja ndani ya chadema kwa sasa,hakuna maono wala misingi ya chama inayowaunganisha CHADEMA kwa sasa.kila mtu kivyake ,kila mtu na anavyoamini na njia za kufikia.kila mtu na njia yake ,kila mtu na muelekeo wake,kila mtu na misamiati yake,hakuna msimamo wa pamoja kama chama.
Kila mmoja anajiendea anakotaka mwenyewe,kila mmoja anazungumza lugha yake mwenyewe na kuielewa mwenyewe lugha hiyo,kila mmoja na mikakati na mipango yake,kila mmoja na Dira yake ,kila mmoja anajiona yupo sahihi na anajiona yeye ndiye anapaswa mawazo yake kuongoza chama.chama hakina msemaji wala mwenyekiti wa kuheshimika,kila mmoja anamwenyekiti wake na katibu wake na msemaji wake anayemuamini akizungumza. Chama kimebaki kama mkusanyiko wa kondoo waliotelekezwa na mchungaji wake na kubakia wakitanga tanga.
Kwa sasa ndio maana hakuna habari za mikutano wala operation, kwa kuwa hakuna maelewano mazuri kati ya mwenyekiti wa chama na makamu wake,hakuna maelewano kati ya wanachama na uongozi wa juu,hakuna imani na kuaminiana miongoni mwa viongozi wenyewe, kila mmoja yupo upande wake kwa malengo yake binafsi na siyo chama.
Tuhuma na kutuhumiana ndiko kumetawala ndani ya CHADEMA, hisia za usaliti na kusalitiana ndiko kumeteka hisia za chama chote kuanzia juu mpaka chini,kila mmoja akimuona mwenzake ni msaliti na anakisaliti chama.
Lissu kaona isiwe shida kaamua kususa chama na shughuli zote za chama,kaamua kuwa mbali na chama,kaamua kuangalia mambo mengine,kaamua kunyoosha mikono juu.kaona sasa CHADEMA ni kama ipo katika ujenzi wa mnara wa Babeli ambapo ni lugha gongana ndio iliyotawala ndani ya chama,hakuna kusikilizana wala wa kusikilizwa.hakuna cha mkubwa wala mdogo,wote ni makambale na wote ni mabeberu walioota ndevu na wote ni mafahari ndani ya Zizi ,kila mmoja anangurumaa kwa sauti nzito kuonyesha umwamba wake na kwamba yeye ndiye mkubwa na mbabe .
Sasa yasemekana kuna uwezekano chama hicho kisishiriki uchaguzi wowote kati ya mwakani na mwaka unaofuata.maana umoja na mshikamano umevunjika na kinaona hakiwezi kupata wala kuambulia chochote kile katika uchaguzi wowote ule ambao kitashiriki. Kwakuwa hakina nguvu kutokea ndani yake ambayo ndio msingi wa ushindi kwa chama chochote kile kuwa na umoja na mshikamano kutokea ndani yake kabla ya kwenda kupambana nje.
Tuendelee kutulia kuangalia mnyukano unaoendelea ndani ya chama hicho kinachorusha lawama kwa baadhi ya viongozi wake wa juu kuwa wanajichotea na kujipakulia sana minyama ya Minofu laini laini na kujinenepesha wao huku chama na wanachama wakiendelea kukondeana na kudhoofika kila uchwao.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.