Ivi ata zamani kulikuwa na ST Kayumba?
Alafu UKO SADC si waongee kiswahili alafu watatafsii maana mambo ya kujiuma unakosa confidence na point zinapotea
Mkuu huwezi kutumia lugha yako ya nyumbani kama huna nguvu ya kutosha kiuchumi. China wameweza hilo kwenye G 20 sababu ya uchumi imara.
Sisi bado tunauza udongo kwa wenzetu na wao wanatuuzia vyungu baada ya kutumia huo udongo sasa unategemea nini.
Halafu hakuna sababu ya msingi ya kutojua lugha zingine...huko ni kujiendekeza tu. Nilipokuwa Switzerland nilikutana na watanzania wenzangu wanafanya kazi za uhudumu kwenye migahawa na walikuwa wana uwezo wa kuzungumza kijerumani, kiingereza na kifaransa kwa ufasaha kabisa. Hawa ni watu walioenda huko miaka michache iliyopita kutafuta maisha.
Kuna maafisa ubalozi wanakuja kwetu wakiwa na umri wa miaka 50 na zaidi na baada ya kukaa nchini kwa miezi miwili, tayari wanazungumza kiswahili vizuri na kwa ufasaha ikiwa ni lugha ya tano au zaidi. Wanajua kuwa hawawezi kutetea vema maslahi ya nchi zao bila kujua lugha kuu katika mahala husika.
UTATUZI sio kutumia kiswahili na kutafuta wakalimani. Tuache uvivu, tuanze kujifunza kiingereza, kifaransa, kijerumani, kihispanola, kichina n.k. Ni rahisi mno kama tusipojiendekeza.
Ilitakiwa watu wanaogombea ubunge sifa mojawapo iwe uelewa mzuri wa lugha za kigeni.
Ndio maana mawaziri wetu na wataalam wao wanashindwa kusoma mikataba nyeti. Kama English ya kawaida tu ni tatizo je ya kitaalam itakuwaje? Hivi lugha za kisheria, kichumi na kibiashara( Business English) itakuwaje kwa mtu ambaye kujieleza kwake ni
Ze ze honorabo supika, and ze my membazi of of of ze paliamenti of ze Tanzania. I want to vai for ze zis pozisheni of ze riprizentingi ze Tanzania paliamenti in ze Sadeki of ze paliamenti.
So i beg you to vote ze for me.!!!!!!!!
Lamberto!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!