Jamani kumbe wabunge wetu umombo...Mmmmm

Jamani kumbe wabunge wetu umombo...Mmmmm

Na yule aliyesema amesoma Advanced Diploma in CERTIFIED ACCOUNTANT..aliniacha hoi sana kwa kweli.
 
Nashauri bunge liendeshwe kiingereza. Tutacheka mpaka kuvunjika mbavu maana kuna watu wanapiga umombo kama hawana akili nzuri.
 
Jamaa hawajui tenses!!!, wanachanganya badala ya past continuous tense yeye anasema past tense, hata speaker shida! Wa chadema amejitahidi anaonekana anajua tenses

wote maimuna........
 
Itabidi naye Prof.Maji Marefu atuwakilishe,na du huo ung'eng'e wa mheshimiwa aliyekuwa mkaguzi wa hesabu na hata ndugu Ole nae bado
 

Agreed
. That wasn't an English class you people. Mimi niliona kipindi hicho live na kuridhika jinsi wengi wao walivyojieleza hasa kwa vile Kiingereza siyo Lugha yetu. Hali kama hiyo ingejitokeza pia endapo ungewataka Wajeremani, Wafaransa, Wachina au Watu wa Scandinavia wazungumze kingereza Bungeni mwao. Tatizo letu Watanzania tunapenda sana kuchunguza grammer kwenye spoken English kama vile tuko kwenye Mtihani wa Literature. Mtu akikosea kidogo basi tutacheka kama mazuzu. Ni rahisi kukosoa kuliko kutenda. Wengi wetu tungepewa nafasi ile ya kujieleza jana, hali ingekuwa mbaya kuliko tulivyoiona. Hata aliyeanzisha mada/post hii anajua Kihaya zaidi kuliko Kiswahili au Kingereza. Ni majigambo na ujinga tu ndiyo vinatusumbua.

Mkuu nadhani labda unashindwa kupata point ya muhimu kuhusu hi hoja, ni kuwa hao wabunge wataenda kuiwakilisha Tanzania SADC, na wanaenda huko kwa maslahi ya Taifa na inawapasa wawe na uelwa wa kile kinachoongelewa, SADC ina lugha nne za kiofisi
1) Kiingereza kwa Botswana, Tanzania, Zambia, Malawi, Zimbabwe
2) Kifaransa kwa DRC, Comoro na Madagascar
3) Kireno kwa Mozambique na Angola
4) Africans kwa South Africa na Namibia
hizo ndizo lugha zinazotambuliwa kwa hiyo ili uchangie vizuri hoja zako kwa faida ya nchi yako inakupasa uwe na uelewa wa Mzuri wa angalau Lugha Moja ya hizo,
Tatizo kubwa nililoliona jana ni kuwa pamoja na wengi wa hao Wagombea kuwa na level ya Bachelor na kuendelea, lakini upeo wa kujua mambo pia ni mdogo sana, na mwisho wa siku utakuta hao wagombea wameingia kwenye hicho kinyanganyiro kimaslahi binafsi na wala hawajuhi wanaenda kufanya nini huko na kwa mwendo wa Broken kama ule nadhani wote watakuwa ni mabubu tu kule Gaborone
 
acheni kutukuza lugha kiasi hicho. mbona mi ni msomi mzuri tu ila si mzuri kwa kiindereza na ninapata kazi ndani na nje ya nchi na ninazifanya vizuri tu! kiingereza ni lugha tu, haina uhusiano mkubwa sana na matokeo ya utumishi wao
 
Ningelikuwa mimi ningelijali zaidi knowledge ndogo waliyo nayo wabunge wetu juu ya hiyo SADC wanayotaka kwenda kutuwakilisha kuliko level ya kiingereza chao.

Kiingereza ni lugha ya wengine na kama hutumii kila siku na ghafla ukaambiwa ujieleze kwenye hiyo lugha utatababaika tu.

Ingelikuwa vizuri laiti wangelikuwa wazuri sana wa Kiingereza lakini sio the most important factor. Angalia wawakilishi mbalimbali hapa duniani, pamoja na lugha zao kutokuwa nzurri, hawajashindwa kufanya kazi zao. Hata katibu mkuu ya UN anaongoza baraza kwa kiingereza chake kisicho timamu na hujasikia wajumbe wakimcheka.

Watanzania tuna ujinga mwingi ambao tunaufumbia macho na kuweka nguvu zote kwenye nani anaweza kuongea Kiingereza bila makosa. Ukiangalia hata kiswahili tunaongea kwa makosa japo tuna confidence nacho na ambayo inaficha makosa kibao ya waziwazi.

Wabunge wajitahidi kusoma ili kuongeza uwezo wao wa kujua mambo ya dunia na challenges mbalimbali ambazo zinaikabili dunia kwasasa na namna ya kupambana nazo. Tupunguze hii ya nyama choma kila jioni na badala yake kuwe na muda wa japo kujisomea vitabu.


Tatizo nililoliona la wabunge wetu baada ya kufuatilia huu mjadala ni yote mawili; lugha na knowledge.

Kuhusu swala la lugha sijui kwa nini tunajitetea sana wakati english ni official language. Swala ni kukubali umaimuna unatusumbua na lugha ni tatizo la kitaifa period!!! Sioni sababu ya mtu kuja hapa kusema kuwa english ni tatizo kwa kuwa siyo lugha yetu!!! Hivi nchi kama Kenya, Uganda, Zambia, Malawi n.k. wao english ni lugha yao?? au sisi tunatofauti gani na wao?? Kama tuliamua english kuwa official language ilitakiwa tuipe uzito unaostahili. Usije shangaa miaka 10 ijayo Rwanda watakuwa wametupita kwa kiingereza ingawa wamenza nacho juzijuzi tu!!

Actually, tatizo la nchi yetu siyo english tu hata kiswahili ni tatizo. Kama huamini pitia mijadara humu ndani utagundua watu kibao kiswahili kinatupiga chenga. Badala ya kuandika Rais Kikwete, mtu anaandika Rahisi Kikwete; Badala ya kuandika Majira, mtu anaandika majila.......Kuna mifano mingi tu.

My conclusion, kwa ujumla watanzania hakuna lugha tunayoifahamu vizuri. Sasa ukichanganya na knowledge na exposure yetu kuwa chini then huko SADC jamaa kama wanakwenda kufuata DSA tu period. Kama wanashindwa kuchangia kwenye bunge lao la kiswahili hapo Dodoma unategemea nini huko nje?? Nakumbuka kama kuna wakati kulikuwa na list humu JF ya wabunge kibao ambao hawajachangia hoja kwa miaka mitano. Mwenye nayo naomba atuletee hapa, probably MKJJ!!!
 
Eee bwana weee wacheni kukandia hao wabunge wetu kwa issue ya lugha.

Mimi huwa nahudhuria mikutano mikubwa ya kimataifa yanayohusiana na field yangu. Utakuta Professa limebobea kwenye taaluma yake lakini kwa vile amebadilisha lugha (labda from Spanish or French to English) basi na yeye huwa 'zis is zat is'. Lakini huwa anapewa heshima zote.

Muhimu ni mchango wake katika hilo bunge.

Nakubali ktk mikutano ya kimataifa kunakuwa lugha nyingi na mkalimali (interpreters). Huko unaweza kumpeleka mwakilishi ambaye ni mtaalam wa somo lake lakini anababaisha azungumzapo umombo. Lakini ktk SADC Forum, ambako hawa wenzetu watawakilisha Tz wanazungumza umombo tu, bila mkalimali. Ni lazima Tz. tupeleke wanaoweza hii lugha.

Mwakilishi aliyezungumza umombo bila wasiwasi ni yule Mbunge wa Arumeru Magharibi, licha ya kuwa ni CCM.
 
Interestingly, hii thread pia majadiliano ni katika kiswahili. Nashangaa kujaribu kufunga wengine kengele. Hata hivyo sitetei hao waheshimiwa wabunge kwa ukilaza wao uliotukuka
 
Ni utwana tu unatusumbua, eti kuwania uwakilishi SADC lugha ya kujieleza ngeli!! Yule Mnyaa pumbafu ngeli yake mabaga lakini amepewa kuwakilisha upinzani! what a shame? nway ni uzuzu wetu ndio unatuponza sana, nyaraka zote serikalini hata vikao muhtasari na madokezo ni swahili 100% Ubunge wa Sadc ngeli!!!!
 
Mkuu mi mwenyewe nimecheka mnooo jinsi mdau alivyo m-quote speaker eti Senkiuu,enye q!
Ila kusema kua Africa tuna janga la lugha sidhani kama ni wote!nchi za west africa karibia zote wako poa kwa ngeli,east africa ni Tz tu yenye challenge coz KY,UG etc wote wanatema mbaya,south africa countries ndo usiseme!
Kuna haja watu wakaelewa kua hii luga ilikuja na MELI ila ni ya muhimu kinoma!
Wakati sisi tunahangaika na Ngeli wazungu wanahangaika na kujifunza kichina coz ndo itakayo lipa baadae!
Yaani speaker ndo kabisaaaaa hoi!
NB:Kingereza ni luga iliyokuja na meli!!!!kaaziii kweli kweli!ha ha haaaaaaaa


Mkuu, sijasema ni janga la Africa, bali ni janga la kitaifa nikimaanisha Tz. Upo sahihi kabisa, hii lugha ingawa sio asili yetu ni budi tukaitilia mkazo. Pendekezo langu ni kwamba wabunge wote wawe wanajuwa hii lugha kwa ufasaha, iwe moja ya masharti ya kugombea ubunge vinginevyo kama walivyosema wachangiaji wengine, mikataba mibovu ndio uanzia hapa. Sasa wabunge wasiojuwa kingereza wanapotembelea nchi za nje kwa shughuli za kibunge/kamati ya bunge itabidi waende na wakalimani? If so akalimani hao watalipwa na nani? Mbona Tz tunakazi kubwa kiasi hiki!!

Nimeona wachangiaji wengine wakisema hakuna mauhisiano kati kujuwa kingereza na uwezo wa kuchambua mambo. Wakati hili ni sahihi kwa nchi za wenzetu, kwa Tz dhana hii yaweza kuwa sio sahihi. Tz wengi wanaoongea lugha hii ni wale ambao angalau wamehitimu chuo kikuku au kusoma katia shule bora za kimataifa, hii ina maana kwamba yawezekana upo uwiano chanya baina ya elimu yao (ambayo wameipata kwa lugha ya kingereza) na uwezo wao wakuitumia elimu na lugha hiyo katika uchambuzi wa mambo. It is an hypothesis worth testing.
 
Ai Nooo!

Spikingi Inglishi izi noti izi iveni fo graduetsi.

Bati iti izi okee

ifu yuhevu pointi jasti go thea endi spiki yua brkeni ingilshi, ze mosti impotanti singi izi tu deliva ze messeji.

iveni Kenyani,hu wi sinki hevu guudi inglishi du spiki brokeni ingilishi tuu.

Ifi wani keni noti spiki inglishi theti izi noti a problemueti olu spiki awa bilavudi Kiswahili endi leti azazi heso tu transileti.

Hii hiii:becky::becky:
 
Ai Nooo!

Spikingi Inglishi izi noti izi iveni fo graduetsi.

Bati iti izi okee

ifu yuhevu pointi jasti go thea endi spiki yua brkeni ingilshi, ze mosti impotanti singi izi tu deliva ze messeji.

iveni Kenyani,hu wi sinki hevu guudi inglishi du spiki brokeni ingilishi tuu.

Ifi wani keni noti spiki inglishi theti izi noti a problemueti olu spiki awa bilavudi Kiswahili endi leti azazi heso tu transileti.

Hii hiii:becky::becky:

Yua komenti izi veri interesitingi, bekauzi iti tuku mi moa zani faivu minuti tu andasitandi zisi wedi '' BILAVUDI '':smile-big:, bati ati lasiti ai goti iti.
 
Back
Top Bottom