Jamani.. Jamani, serikali imeanza kutumia RANGE ROVER VOGUE kama STK..!?

Jamani.. Jamani, serikali imeanza kutumia RANGE ROVER VOGUE kama STK..!?

bluetooth23

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2013
Posts
348
Reaction score
326
Jamani wana JF.. Mpaka muda huu sijaamini nilichokiona asubuh hii muda mfupi uliopita. Nipo kwenye daladala natokea mwenge nakwenda job posta, daladala niliyopanda inatokea mwenge kwenda posta kwa kutumia barabara ya Alli Hassani Mwinyi, tumefika kwenye mataa pake kona ya kwenda Oyesterbay na nyingine kinondoni tulisimama kidogo, nimeona gari aina ya Range Rover Vogue ina plate namba za serikali STK ikitoka Oyesterbay inaelekea town. Jaman mpaka muda huu cjaamini kama kwel serikali imeanza kutumia aina hyo ya gari za bei mbaya kwa watumishi wake. Jaman kama kuna mwingine aliyeiona tena au mwenye kufahamu atuambie..
 
Mimi niliona siku ya jumamosi maeneo ya airport na kustaajabika!
 
Yawezekana ni kwa HISANI YA WATU WA UINGEREZA! Na kwa kuwa STL zimetoka mbona lipo siku nyingi!
 
Mimi niliona siku ya jumamosi maeneo ya airport na kustaajabika!

Kama ni kweli basi tulipofika hapaelezeki. Serikali ya kikwete inayoitwa sikivu inamsikiliza nani? Wametafuna kodi zetu kwa ajili ya mafuta ya ma V8 wameona haiotoshi na sasa wameamua kununua hayo majini. Hivi kuna raha gani kwa serikali kuoperate kifahari namna hiyo wakati inaowaongoza hata panadol hawawezi kuafford? Hivi hamfeel guilty kupita na hiyo mivogue yenu kwenye huu umaskini uliotukuka? Shame on you!
 
halafu tunalalamika eti nchi yetu masikini.
mipango na matumizi yetu havileti maana
 
Wnapima upepo! mkianza kulalamika hivi wanaweza sitisha kuyaleta kwa wingi ila mkinyamaza basi mjue mpaka mheshimiwa sana anaondoka Magogoni halitakuwa moja tena na utasikia haya ni ya mawaziri kwa ajili ya matumizi ya wikiend........kwa CCM kila kitu kinawezekana.
 
aisee we ndo unaziona leo mbona hapa posta tunapishana nazo daily ila.kumbukuka kuna watu wanazo zao binafsi wanaomba namba za serikal baada ya hapo wanazitoa siku wakiwa waanastaf
 
Hata Benjamin mkapa anatumia aina hiyo ya gari kitambo sana tangu 2007, Misafara ya jakaya imebadilishwa Ross roy ndo mpango mzima, Wakistaafu wanajiuzia kama gari chakavu kama vile walivyojiuzia Mercedes Benz 60 walizonunua 2004 kwa ajili ya mkutano wa Marais wa Sadec baada ya mkutano waliuziana kama gari chakavu wakati zilifanya kazi kwa siku 16 tu.
 
Scanner pale muhimbili iliaribika hakuna pesa..madawati shuleni hakuna bajeti ndogo...polisi ukienda ukikuta gari basi mafuta hakuna na ukikuta mafuta gari hakuna..magari ya wagonjwa hayapo....madawa hakuna hospitalini..lakini pesa zote zinaishia kwenye vitu visivyo vya lazima..wajifunze toka india na china serikalini yanatumika magari madogo yasiyo na gharama katika manunuzi..uendeshaji na vipuri kama vitz
 
hiyo STK huwa inapatikana pale mahakama kuu. ni nyeusi
 
Deeni la taifa linazidi kuongezeka na bado wanafanya vitu vya namna hiyo kweli???
 
Mkuu achana na hiyo kuna nyingine ni ya police ina plate number za PT ipo sana pale central
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom