Jamani hii ya Kamanda Kova imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani hii ya Kamanda Kova imekaaje?

Discussion in 'Jamii Photos' started by Mzee Mzima, Apr 10, 2012.

 1. M

  Mzee Mzima Senior Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naomba msaada kujua Kweli Salute ni nani anapigiwa kwani hapa naona anatoa salute wakati wa kumuaga Kanumba, I think this is not right, wanaojua please enlight me. kova salute.jpg
   
 2. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,824
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Wewe ndi hujui protocol za kijeshi...kijeshi maiti yeyote inapigiwa salute...sasa wewe raia haya mambo huyajui bora ukae kimya...
   
 3. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,441
  Likes Received: 9,089
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona hata sugu kampigia salute SCK....
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Imekaa njema haina tatizo kwa kamanda Suleiman Kova kufanya hvyo.
   
 5. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Hapigi saluti hapo.
  Anamwambia hivi"mkubwa mzima ulikua una-mbabu seya Lulu?bora ulivyokufa"
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Tafuta kwanza tafsiri sahihi ya neno Salute, ukishaipata maana yake basi haitakusumbuwa hata chembe.
   
 7. s

  sawabho JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Katika taratibu za kijeshi maiti yo yote, hata ya kwako inapigiwa salute na askari aiyevaa sare wakati wa kutoa heshima za mwisho.
   
 8. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Sasa mkiwa vitani utapiga saluti ngapi kwa wote watakaokufa?
   
 9. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Za maadui je?
   
 10. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Sugu ni kamanda.
   
 11. J

  John W. Mlacha Verified User

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  kwani kova alikuwa haangalii movie za kanumba? inauma acheni
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  eti kuna mtu anauliza kuwa sugu ni kamanda?

  nenda mbeya kaulize sugu ni nani?

  baada ya jeshi kushindwa ukamada chadema imeamua kusimamia mambo yote yanayohusu ukamanda.
   
 13. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #13
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Kamanda Bangi
   
 14. luhala

  luhala JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 412
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimesoma gazeti la Tanzania Daima leo habari hii na imenishangaza sana
  Ukweli ni kwamba Kova alikuwa sahihi kabisa kwa kitendo alichofanya na kwa ufafanuzi alioutoa na nimemkubali kwa elimu aliyoitoa kwani kisheria Saluti ni alama ya heshima kwa mkuu au mtu mwenye mamlaka juu yako. Kimsingi nyuma ya Majeshi yote duniani yana raia kama wawezeshaji wakuu wa uwepo wao. Katika mila na desturi za kijeshi Raia wa kawaida hapigiwi saluti isipokuwa kama yafuatayo yatajiri:
  i. Akiwa na cheo cha kisiasa ambacho moja kwa moja anamwakilisha Rais , Mfalme, Malkia au Mkuu wa nchi.
  ii. Akiwa amefariki ambapo askari au Afisa bila ya kujali cheo chake hata kama ni CDF (Chief of Defence Forces) IGP
  au Kamishna anapaswa kusimama kwa heshima na kuupigia saluti mwili kutoa salamu na heshima kwa Raia yule
  ambaye kimsingi ndiye aliyekuwa mwajiri wake. Saluti kwa mwili haijalishi umri, jinsia, wala cheo cha marehemu
  alipokuwa mzima wala rika la marehemu kulinganisha na anayeitoa saluti hiyo. Kwa maana hiyo askari aliyeiva
  sawasawa kama Kamanda Kova na anayejua wajibu wake ataupigia saluti hata mwili wa mtoto mdogo ukiwa
  umeandaliwa kwa mazishi au ukiwa safarini kuelekea huko.
  iii. Katika nchi za kifalme Malkia na familia ya kifalme hupigiwa saluti.
  NB: Ninayeandika haya ni Afisa Mwandamizi Mstaafu aliyehudumia JWTZ kwa zaidi ya miaka 40 hadi kustaafu na aliyefanya mafunzo (Na kufundisha) ndani na nje ya nchi hii.
  Changamoto: Maafisa na maaskari wa leo ambao awali hamkuwa mkijua hili kama huyo Afisa aliyenukuliwa na gazeti hilo (Kwenye grey bold) mjifunze kutokana na somo alilolitoa Kova.
  Inatisha, kusikitisha na kukatisha tamaa kuona wapo ndani ya majeshi yetu aina ya maafisa kama huyo aliyenukuliwa na gazeti hilo.
  Bravo Commander Kova.
   
 15. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Huyo mzee alikuwa anatafuta jinsi atakavyotoka kiaina. Kanumba alikuwa na title gani hadi kupigiwa saluti?
   
 16. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mguuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu pande Sawaaaaaaaaaaaaaaaa

  sawa afandeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 17. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni yangu kamanda Kova hakuwa sahihi kuipigia salute maiti ya Kanumba.

  Sababu salute ni salamu au heshima ya kijeshi kwa mtu aliyekuzidi cheo au mamlaka.

  Kova anajua miko ya salute lakini nadhani alipitiwa tu.
   
 18. K

  Kipara kikubwa Member

  #18
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hata wewe hujajibu. Kwa ufupi Kova alikuwa sahihi kupiga salute ile ni msingi wake si mwili wa marehemu bali hoja ya kwanza ni kuwa alivaa uniform na pale alikuwepo Makamu wa Raisi na baadhi ya Mawaziri amabao wanapigiwa salute kwa hiyo anapopita pale pamoja na mwili salute inaonyesha utii wa kijeshi kwa wakuu waliokuwapo ktk wale waombolezaji km kusingekuwa na hao heshima kijeshi au kwa askari alovaa unform hawezi bend atakunja mikono na kuinuka kidogo lkn kwa uwepo wa viongozi wale anatoa heshima hiyo kutambua uwepo wao hapo. Tanzania daima nao wakurupukaji
   
 19. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Kama ana heshima ampigie basi Dk. Slaa kama haujasikia another version of story, labda aseme to the late Kanumba was secret service na alikua na cheo kuliko yeye, otherwise babu kachemka mazima
   
 20. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  kova hajakosea.., polisi na jeshi, wote wanapaswa kum-salute marehemu YOYOTE..., awe na cheo asiwe na cheo.., ni heshima anayopewa marehemu..,

  haku-salute kwa sbb ni kanumba, amesalute kwa sbb yule ni marehemu na anapewa heshima yake....,

  kama hujui kanuni na nidhamu za kijeshi usibishe vitu usivovijua.., lakn ku-avoid kuchanganya watu wasiojua haya mambo ndio maana servicemen wengi wanaenda na civ clothes,

  Ile ni nidhamu ya kijeshi kwa marehemu wetu si kwa sbb ni kanumba, nada!
   
Loading...