By
luhala
Nimesoma gazeti la Tanzania Daima leo habari hii na imenishangaza sana
Ukweli ni kwamba Kova alikuwa sahihi kabisa kwa kitendo alichofanya na kwa ufafanuzi alioutoa na nimemkubali kwa elimu aliyoitoa kwani kisheria Saluti ni alama ya heshima kwa mkuu au mtu mwenye mamlaka juu yako. Kimsingi nyuma ya Majeshi yote duniani yana raia kama wawezeshaji wakuu wa uwepo wao. Katika mila na desturi za kijeshi Raia wa kawaida hapigiwi saluti isipokuwa kama yafuatayo yatajiri:
i. Akiwa na cheo cha kisiasa ambacho moja kwa moja anamwakilisha Rais , Mfalme, Malkia au Mkuu wa nchi.
ii. Akiwa amefariki ambapo askari au Afisa bila ya kujali cheo chake hata kama ni CDF (Chief of Defence Forces) IGP
au Kamishna anapaswa kusimama kwa heshima na kuupigia saluti mwili kutoa salamu na heshima kwa Raia yule
ambaye kimsingi ndiye aliyekuwa mwajiri wake. Saluti kwa mwili haijalishi umri, jinsia, wala cheo cha marehemu
alipokuwa mzima wala rika la marehemu kulinganisha na anayeitoa saluti hiyo. Kwa maana hiyo askari aliyeiva
sawasawa kama Kamanda Kova na anayejua wajibu wake ataupigia saluti hata mwili wa mtoto mdogo ukiwa
umeandaliwa kwa mazishi au ukiwa safarini kuelekea huko.
iii. Katika nchi za kifalme Malkia na familia ya kifalme hupigiwa saluti.
NB: Ninayeandika haya ni Afisa Mwandamizi Mstaafu aliyehudumia JWTZwa zaidi ya miaka 40 hadi kustaafu miaka kadhaa iliyopita na aliyefanya mafunzo (Na kufundisha) ndani na nje ya nchi hii.
Changamoto: Maafisa na maaskari wa leo ambao awali hamkuwa mkijua hili kama huyo Afisa aliyenukuliwa na gazeti hilo mjifunze kutokana na somo alilolitoa Kova.
Bravo Commander Kova.