Jamani hii kitu ni ndege ama nini

Jamani hii kitu ni ndege ama nini

Ni ndege,..ila huwa na sauti kubwa..mnooo kwahyo hupita juu zaidi ili kuepusha noise pollution,.mtafaruku kwa watu..
 
Huo ni uongo Mkuu, kama huelewi jambo ni vema ukae kimya kuliko kuleta stori za wajuba wa vijiweni

Ndege inamwaga mafuta wakati wa kutua kwa emergency tu. Na ndege zinazomwaga mafuta ni zile ambazo zilikuwa zifanye safari ya masafa marefu (long haul) lakini muda mfupi baada ya kuruka ikapata emergency inayomlazimu atue wakati bado ana mafuta mengi, na uzito wa mafuta, mizigo na abiria ni mkubwa akitua bila kupunguza uzito ataharibu landing gear. Pia wanaweza kumwaga mafuta kama emergency landing ina hatari ya moto, kwa mfano, kama landing gear imekataa kutoka na hivyo inabidi atue kwa tumbo. Atamwaga mafuta kupunguza uwezekano wa moto mkubwa. Na pia uzito mkubwa wa ndege maana yake umbali mrefu wa ku brake, kwa kuwa momentum inakuwa kubwa.

Ndege ya kwenda Mbeya kutoka Dar ikipata emergency hata eneo la Kibaha tu inaweza kurudi na kutua bila kumwaga mafuta kwa kuwa ndege huwa hawajazi mafuta kwa kusema weka full tank. Hata ndege ya kwenda South Africa inaweza kurudi na kutua bila kumwaga mafuta, kwa kuwa mafuta atakayokuwa amechukua sio mengi kiai hicho kwa safari ya masaa matatu ya kwenda Johannesburg

Hakuna pilot atamwaga mafuta baada ya kufika destination eti aliweka mafuta mengi au alipatwa na mgandamizo mkubwa njiani. Hizo n stori za vijiweni.


Mkuu asante sana kwa jibu zuri nimekuelewa haswaaa ila naomba kuuliza swali hayo mafuta yanamwagwa wapi angani kabla ndege haijatua au wapi?

Asante.
 
Ni ndege ukiwa na samsung s20 ultra unaweza kuizoom na kuiona
 
Kwa uelewa wangu huu mdogo, ila wanaojua zaidi watasema hii ni Ndege Kasi aina ya Concorde ambayo kwa Afrika inatua tu Cairo na Cape Town.
Maelezo yako kwa asilimia kadhaa yameshabihiana na uongo tuliodanganywa enzi hizo.

NAKUMBUKA TULIVYOKUWA TUNADANGANYWA NA WAZEE WETU KWAMBA HIZO NI ROCKET NA AFRIKA ZINATUA NCHI MBILI TU MISRI(CAIRO) NA AFRIKA KUSINI (JO.BERG)

Baada ya kuwa na uelewa na ufuatiliji wa mambo ya NASA na vita za mashariki ya mbali na kati na kule korea ya kaskazini, mpk muda huu najiuliza ROCKET ZINAZOBEBA WATU NA MIZIGO ZILIENDA WAPI, maana za siku hizi zinaweza kubeba MABOMU na vifaa vya kwenda anga za mbali tu.
 
Hii nadhani kwa Tanzania kila mtu ameshawahi kuona ikipita angani hasa pasipo kuwa na mawingu. Wakati mdogo, mzee aliniambiaga inaitwa roketi ni jamii ya ndege lakini Africa hamna uwanja wa kutua alafu ikitua humwaga mafuta Kwanza lakini niki-Google sioni story yake kwa anaejua nisaidie.

Yaani utafikiri mzee wako alikuja kwetu pia,na sisi tukiwa wadogo tuliambiwa na ndege kubwaaaaaaaa,haiwezi kutua hapa kwetu
 
Ndege yenye Jet engine hutoa hizo Condensation trails, husababishwa na hewa ya moto iliyotoka kwenye engine inapokutana na hewa ya ubaridi, hupoa haraka na kutengeneza hilo kama wingu.

Rocket sio ndege wala haina uwanja wa kutua bali huwa na lauching pad, pia rocket husafiri vertical na sio Horizontal,
Rocket sio ndege bali ni chombo kinachotumika kupeleka vifaa kwenye sayari za mbali.
mweeh
 
Kwa ufupi tu kinachotokea pale ni kwamba,kama umewahi kuishi sehemu zenye baridi kama Iringa au Mbeya kuna muda ukiamka asubuhi ukiongea unatoa moshi/mvuke mdomoni sasa basi hewa inayotoka mdomoni inakua ni ya moto kuliko inayokuzunguka nje. Hivyo inakua inalazimishwa kupoa itokapo mdomoni hapo ndipo unaona ule moshi ukipumua kupitia mdomo na ndivyo hivyo hivyo kwenye ndege zinazopita kwenye anga za kimataifa pale kunakua na baridi kali kwa hiyo hewa ya joto kali inayotoka kwenye jet engine ikikutana na baridi kali inalazimishwa kupoozwa hapo ndipo unapo ona ule moshi/mvuke.

Nadhani utakua umeelewa kwa ufupi mleta uzi
Boss asante sana ,nimepata maelezo murua,watoto wakijilengesha wakaniliza nawamiminia material
 
Ngoja ngoja twende taratibu jibu na hili inakuwaje hapa duniani tunapata joto kali na huko juu kuwe na baridi kali wakati joto tunalolipata huku ndo linatoka huko..??????
Swali konki sana hili
 
Anga la kimataifa ndo huko juu kabisa zinapopita hizo ndege kubwakubwa.. it means hakuna nchi inamiliki hilo anga isipokuwa Kuna kimo ukipita Kuna anga la kila taifa mfano tz .. sijui umbali exactly wa kwenda juu ndo inakuwa si anga lakimataifa ila nafikiri upo umbali huo.. so ukishuka chini ya huo umbali unakuwa umeingia kwenye anga la nchi fulani itategemea na upo nchi gani so wanahaki ya kukuhoji,kukuzuia usitue endapo wakitia shaka n.k..
Asante mkuu
 
Back
Top Bottom