Jamani hii kitu ni ndege ama nini

faustincheyo

JF-Expert Member
Jul 18, 2020
201
250
Hii nadhani kwa Tanzania kila mtu ameshawahi kuona ikipita angani hasa pasipo kuwa na mawingu. Wakati mdogo, mzee aliniambiaga inaitwa roketi ni jamii ya ndege lakini Africa hamna uwanja wa kutua alafu ikitua humwaga mafuta Kwanza lakini niki-Google sioni story yake kwa anaejua nisaidie.

52018761-jet-plane-in-sky-vapor-trail-of-air-vehicle-in-clear-sky.jpg
 

mapololo

Senior Member
Jul 28, 2015
190
250
Duuh,Mkuu mababu zetu huwaga wasanii ila wakwako kazidi aisee,ningetamani nimuone, Ok kwa kifupi hiyo ni ndege kubwa(jet) yaweza kuwa aina yeyote Airbus, Noon nk, kuhusu suala la kumwaga mafuta wakati wa kutua ni uongo na pia Kama ukibahatika safiri safari za kimataifa huko Angani utaziona nyingi tu na ni ndege za kawaida, kuhusu uwanja kwa zamani ndege kubwa tulikuwa hatuna Ila Sasa hivi ndege yeyote yaweza tua DIA.
 

yonga

JF-Expert Member
Mar 17, 2012
1,870
2,000
Kwa ufupi tu kinachotokea pale ni kwamba,kama umewahi kuishi sehemu zenye baridi kama Iringa au Mbeya kuna muda ukiamka asubuhi ukiongea unatoa moshi/mvuke mdomoni sasa basi hewa inayotoka mdomoni inakua ni ya moto kuliko inayokuzunguka nje. Hivyo inakua inalazimishwa kupoa itokapo mdomoni hapo ndipo unaona ule moshi ukipumua kupitia mdomo na ndivyo hivyo hivyo kwenye ndege zinazopita kwenye anga za kimataifa pale kunakua na baridi kali kwa hiyo hewa ya joto kali inayotoka kwenye jet engine ikikutana na baridi kali inalazimishwa kupoozwa hapo ndipo unapo ona ule moshi/mvuke.

Nadhani utakua umeelewa kwa ufupi mleta uzi
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,060
2,000
Kwa ufupi tu kinachotokea pale ni kwamba,kama umewahi kuishi sehemu zenye baridi kama iringa au mbeya kuna muda ukiamka asubuhi ukiongea una toa moshi/mvuke mdomoni sasa basi hewa inayotoka mdomoni inakua ni ya moto kuliko inayokuzunguka nje kwa hiyo inakua inalazimishwa kupoa itokapo mdomoni hapo ndipo unaona ule moshi ukipumua kupitia mdomo na ndivyo hivyo hivyo kwenye ndege zinazopita kwenye anga za kimataifa pale kunakua na baridi kali kwa hiyo hewa ya joto kali inayotoka kwenye jet engine ikikutana na baridi kali inalazimishwa kupoozwa hapo ndipo unapo ona ule moshi/mvuke

Nadhani utakua umeelewa kwa ufupi mleta uzi
Ngoja ngoja twende taratibu jibu na hili inakuwaje hapa duniani tunapata joto kali na huko juu kuwe na baridi kali wakati joto tunalolipata huku ndo linatoka huko..??????
 

The Icebreaker

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
6,590
2,000
Mi nilijuaga huo Moshi ndo mnogesho wa safari sasa..😂
Ndege yenye Jet engine hutoa hizo Condensation trails, husababishwa na hewa ya moto iliyotoka kwenye engine inapokutana na hewa ya ubaridi, hupoa haraka na kutengeneza hilo kama wingu.

Rocket sio ndege wala haina uwanja wa kutua bali huwa na lauching pad, pia rocket husafiri vertical na sio Horizontal,
Rocket sio ndege bali ni chombo kinachotumika kupeleka vifaa kwenye sayari za mbali.
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,060
2,000
Ndege yenye Jet engine hutoa hizo Condensation trails,husababishwa na hewa ya moto iliyotoka kwenye engine inapokutana na hewa ya ubaridi,hupoa haraka na kutengeneza hilo kama wingu,

Rocket sio ndege wala haina uwanja wakutua bali hua na lauching pad,pia rocket husafiri vertical na sio Horizontal,
Rocket sio ndege bali ni chombo kinachotumika kupeleka vifaa kwenye sayari za mbali.
Rocket nasijua mkuu tena vizuri kushinda vizuri kwenyewe..😜

Nilikuwa nataka tu kujua huo Moshi inakuwaje kuwaje.
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,060
2,000

Samahani kuuliza, unaposema anga la kimataifa inamaanisha nn? na hua zinaelekea wapi? haziwezi tua hapa kwetu?
Anga la kimataifa ndo huko juu kabisa zinapopita hizo ndege kubwakubwa.. it means hakuna nchi inamiliki hilo anga isipokuwa Kuna kimo ukipita Kuna anga la kila taifa mfano tz .. sijui umbali exactly wa kwenda juu ndo inakuwa si anga lakimataifa ila nafikiri upo umbali huo.. so ukishuka chini ya huo umbali unakuwa umeingia kwenye anga la nchi fulani itategemea na upo nchi gani so wanahaki ya kukuhoji,kukuzuia usitue endapo wakitia shaka n.k..
 

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
17,216
2,000
Kwa ufupi tu kinachotokea pale ni kwamba,kama umewahi kuishi sehemu zenye baridi kama iringa au mbeya kuna muda ukiamka asubuhi ukiongea una toa moshi/mvuke mdomoni sasa basi hewa inayotoka mdomoni inakua ni ya moto kuliko inayokuzunguka nje kwa hiyo inakua inalazimishwa kupoa itokapo mdomoni hapo ndipo unaona ule moshi ukipumua kupitia mdomo na ndivyo hivyo hivyo kwenye ndege zinazopita kwenye anga za kimataifa pale kunakua na baridi kali kwa hiyo hewa ya joto kali inayotoka kwenye jet engine ikikutana na baridi kali inalazimishwa kupoozwa hapo ndipo unapo ona ule moshi/mvuke

Nadhani utakua umeelewa kwa ufupi mleta uzi
Safi kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom