Jamani hii kitu ni ndege ama nini

Jamani hii kitu ni ndege ama nini

nilijua ni vumbi kwenye barabara ya ndege angani

huko angani kuna trafiki?
Trafiki wapo ila wanakaa ardhini na waitwa air traffic controllers. Ndio wanaosababisha ndege zisigongane ovyo angani. Huwezi kurusha ndege au kutua bila kuongozwa na hawa jamaa, na lazima utii maagizo yao, hata kama wewe hupangiwi na mtu!

1597752405967.png
 

Samahani kuuliza, unaposema anga la kimataifa inamaanisha nn? na hua zinaelekea wapi? haziwezi tua hapa kwetu?
Lugha nzuri ingesema kima kirefu (high altitude), nadhani kasema hivyo kwa sababu anga za kimataifa zinakuwaga kwny high altitude ili kupunguza mwingiliano na anga za ndani, lkn ndg ikikaribia kutua itashuka mpaka low altitude
 
Fuatilia huu uzi wangu vizuri hasa aya ya mwisho utapata jibu lako. Nimeshindwa kuuambatanisha hapa labda mods mnisaidie ili ajifunze zaidi
Screenshot_2020-08-18-15-00-13.jpg
 
Ngoja ngoja twende taratibu jibu na hili inakuwaje hapa duniani tunapata joto kali na huko juu kuwe na baridi kali wakati joto tunalolipata huku ndo linatoka huko..??????
The higher the altitude the low the temperature. Cjui kama nakumbuka vizuri hii kitu nilisoma nikiwa form 1 au 2 hivi, watu wa Physics nisaidieni.
 
Duuh,Mkuu mababu zetu huwaga wasanii ila wakwako kazidi aisee,ningetamani nimuone, Ok kwa kifupi hiyo ni ndege kubwa(jet) yaweza kuwa aina yeyote Airbus, Noon nk, kuhusu suala la kumwaga mafuta wakati wa kutua ni uongo na pia Kama ukibahatika safiri safari za kimataifa huko Angani utaziona nyingi tu na ni ndege za kawaida, kuhusu uwanja kwa zamani ndege kubwa tulikuwa hatuna Ila Sasa hivi ndege yeyote yaweza tua DIA.

Sasa mkuu mbona hizi zinazopita anga la chini hatuoni moshi wake kama tunavyoweza kuona moshi wa hizo za anga la mbalii!?
 
Kwa ufupi tu kinachotokea pale ni kwamba,kama umewahi kuishi sehemu zenye baridi kama Iringa au Mbeya kuna muda ukiamka asubuhi ukiongea unatoa moshi/mvuke mdomoni sasa basi hewa inayotoka mdomoni inakua ni ya moto kuliko inayokuzunguka nje. Hivyo inakua inalazimishwa kupoa itokapo mdomoni hapo ndipo unaona ule moshi ukipumua kupitia mdomo na ndivyo hivyo hivyo kwenye ndege zinazopita kwenye anga za kimataifa pale kunakua na baridi kali kwa hiyo hewa ya joto kali inayotoka kwenye jet engine ikikutana na baridi kali inalazimishwa kupoozwa hapo ndipo unapo ona ule moshi/mvuke.

Nadhani utakua umeelewa kwa ufupi mleta uzi

Hapa nimekusoma mkuu
 
Sio kweli! Nenda Lushoto uamke asubuh utoke nje upige miayo,utakachokiona kinatoka kwenye mdomo ndo sawa na huo moshi wa ndege

Wajinga ( Mangumbaru ) sijui mtaisha / mtapungua lini duniani na hasa hapa nchini Tanzania.
 
Nilishajibu

Ndege inamwaga mafuta wakati wa kutua kwa emergency tu. Na ndege zinazomwaga mafuta ni zile ambazo zilikuwa zifanye safari ya masafa marefu (long haul) lakini muda mfupi baada ya kuruka ikapata emergency inayomlazimu pilot atue wakati bado ana mafuta mengi, na uzito wa mafuta, mizigo na abiria ni mkubwa akitua bila kupunguza uzito ataharibu landing gear. Pia wanaweza kumwaga mafuta kama emergncy landing ina hatari ya moto, kwa mfano, kama landing gear imekataa kutoka na hivyo inabidi atue kwa tumbo. Atamwaga mafuta kupunguza uwezekano wa moto mkubwa. Na pia uzito mkubwa wa ndege maana yake umbali mrefu wa ku brake, kwa kuwa momentum inakuwa kubwa.

Ndege ya kwenda Mbeya kutoka Dar ikipata emergency hata eneo la Kibaha tu inaweza kurudi na kutua bila kumwaga mafuta kwa kuwa ndege huwa hawajazi mafuta kwa kusema weka full tank. Hata ndege ya kwenda South Africa inaweza kurudi na kutua bila kumwaga mafuta, kwa kuwa mafuta atakayokuwa amechukua sio mengi kiasi hicho kwa safari ya masaa matatu ya kwenda Johannesburg

Hakuna pilot atamwaga mafuta baada ya kufika destination eti aliweka mafuta mengi au alipatwa na mgandamizo mkubwa njiani. Hizo n stori za vijiweni.
Wewe ni noma mkuu, asante kwa kunielewesha
 
Hii nadhani kwa Tanzania kila mtu ameshawahi kuona ikipita angani hasa pasipo kuwa na mawingu. Wakati mdogo, mzee aliniambiaga inaitwa roketi ni jamii ya ndege lakini Africa hamna uwanja wa kutua alafu ikitua humwaga mafuta Kwanza lakini niki-Google sioni story yake kwa anaejua nisaidie.

Ndege za mizigo tu hizo na zinatua hapo Adis Ababa Ethiopia mbona
 
Hii nadhani kwa Tanzania kila mtu ameshawahi kuona ikipita angani hasa pasipo kuwa na mawingu. Wakati mdogo, mzee aliniambiaga inaitwa roketi ni jamii ya ndege lakini Africa hamna uwanja wa kutua alafu ikitua humwaga mafuta Kwanza lakini niki-Google sioni story yake kwa anaejua nisaidie.

Hiyo ni ndege ya kawaida (lakini bombadi haioni ndani)hapo inapiga anga la kimataifa yaanihata kama kuna vita kwetu hapa hairuhusiwi uidungie
 
Hii nadhani kwa Tanzania kila mtu ameshawahi kuona ikipita angani hasa pasipo kuwa na mawingu. Wakati mdogo, mzee aliniambiaga inaitwa roketi ni jamii ya ndege lakini Africa hamna uwanja wa kutua alafu ikitua humwaga mafuta Kwanza lakini niki-Google sioni story yake kwa anaejua nisaidie.

Tukupe jibu la kisayansi na kama umesoma ingalau sayansi kidogo, utelewa.
Ndege ikiwa anga za juu(kilometa 10 angani-33,000ftau zaidi), huacha mkia wa exhaust trail.
Hii exhaust ni mchanganyiko wa vumbi kama linalotoka kwenye exhaust ya gari.
Exhaust hizo kuna vumbi pamoja na gesi nyingine na mvuke wa maji kutokana na kuungua mafuta(combustion).
Lakini kule anga za juu kuna baridi kali sana na mvuke ule ukitoka tu kwenye exhaust ya ndege, huganda.
Na huo ndo exhaust trails -mikia tunayoiona.
 
Back
Top Bottom