Ripoti: Hatua kwa hatua hadi ndege ya Precision kuanguka ziwani

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
996
Moshi. Novemba 6 mwaka jana, Tanzania iliamshwa na habari mbaya za kuanguka kwa ndege ya Shirika la Precision Air iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba mkoani Kagera na kusababisha vifo vya abiria 19, huku 24 wakiokolewa.

Ndege hiyo iliondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa 12:10 asubuhi kwenda Bukoba ikiwa na watu 43, marubani wawili, wahudumu wawili na abiria 39 wa ndege hiyo.

Kulingana na ripoti ya pili ya uchunguzi iliyotolewa juzi na Serikali, ndege hiyo ilitarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Bukoba saa 2:25 asubuhi na ilianza maandalizi ya kushuka katika uwanja huo ilipofika saa 1:58.

Ilipofika saa 2:08, kulikuwa na tangazo kutoka chumba cha marubani likiwajulisha abiria kuwa watatua Bukoba saa 2:26 badala ya saa 2:25.
Dakika tisa baadaye, chumba cha kuongoza ndege katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kiliwashauri marubani kuwa hali ya hewa ilikuwa tulivu na kwamba uoni (visibility) ulikuwa ni umbali wa kilomita 10 na hapakuwa na mawingu mengi.

Hata hivyo, wakati wakiendelea kushuka, marubani walianza kuona mabadiliko na dalili za hali mbaya ya hewa kuelekea wanapokwenda, yaani Bukoba.

Katika majadiliano yao, marubani waliona wanaweza kutua uwanja wa ndege wakitokea upande wa ukanda wa mlima ambako kuna njia ya kutua na kurukia namba 13, lakini hiyo ingewezekana kama wangeiona Bukoba kwa chini.

Saa 2:19:32, marubani waliwajulisha kituo cha kuongozea ndege cha Mwanza kwamba wanauona Uwanja wa Ndege wa Bukoba lakini saa 2:24:01 rubani mkuu alisikika akimuuliza rubani msaidizi aangalie kama anaona njia ya kutua.

Ni katika muda wa dakika moja, rubani mkuu alitoa kauli hiyo mara tatu akisema look the runway akimaanisha angalia njia ya kutua na rubani huyo msaidizi akamjibu I am looking, akimaanisha anaangalia kuiona hiyo njia namba 13.

Saa 2:25:45 walishusha magurudumu ya ndege kujiandaa kutua, lakini wakati huo bado njia ya kutua ilikuwa haionekani na hii ni kulingana na mazungumzo yaliyorekodiwa katika vifaa vya kurekodia mazungumzo ndani ya ndege hiyo.

Kulingana na ripoti, saa 2:29:35, rubani alihamishia umiliki (control) kwa rubani msaidizi na hapo walianza majadiliano kuhusu kiwango cha chini cha mafuta kinachotakiwa ili kuweza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Rubani msaidizi akatoa wazo waende kutua Mwanza, kwani itakuwa sahihi zaidi ingawa wakati huo bado walikuwa wakizunguka angani kuutafuta uwanja.
Saa 2:33:33 ndege ilishushwa kutoka urefu wa futi 5,500 hadi futi 5,300 na ilipofika saa 2:33:34, rubani alimwagiza rubani msaidizi kuipeleka ndege uelekeo wa Kemondo na kujaribu tena na hapo rubani aliwatangazia abiria wasingeweza kutua Bukoba kutokana na mvua kubwa hivyo inabidi wasubiri.

Saa 2:34:43 alarm ya umbali kutoka ardhini hadi ilipo ndege (EGPWS), ililia ikionya wako karibu kabisa na ardhi na ilitaka marubani kuipaisha juu na sauti hiyo ya alarm ilisema ‘terrain, terrain, pullup’ kwamba wasishuke tena.
Hata hivyo, kulingana na taarifa hiyo, marubani hawakulifanyia kazi onyo hilo ipasavyo, badala yake waliendelea kujadiliana kuhusu hali ya hewa ya Bukoba na wakawajulisha abiria kuwa wanatakiwa kwenda kutua Mwanza.

Ili kutua Mwanza, kulihitaji kusubiri hadi dakika 20 kwa vile uwanja nao ulikuwa hauonekani vizuri na wakati huo marubani waliendelea kukumbana na ngurumo, radi na mvua kubwa wakati ndege ikielekea Kemondo.

Saa 2:39:56, rubani mkuu alimuuliza rubani msaidizi kama anakiona Kisiwa cha Musila, naye akajibu kuwa amekiona lakini taarifa inasema katika muda wa sekunde 78, bado marubani hao walikuwa wakijaribu kukitafuta bila mafanikio.

Ilipofika saa 2:40 ndege ilishushwa hadi urefu wa futi 4,500 na ilipotimu saa 2:41, rubani alimwagiza rubani msaidizi kwenda spidi ya 102 na aliafiki, lakini sekunde chache baadaye rubani alisikika akimtahadharisha msaidizi wake “watch your speed, speed, speed, i need power” kwamba alihitaji nguvu zaidi.

Hata hivyo, ilipofika saa 2:42:16, rubani msaidizi akasema ameiona njia ya kutua lakini rubani akamuuliza “where is the runway” kwamba iko wapi njia ya kutua na rubani msaidizi akamtaka aitizame kupitia kwake japo mvua inazuia.

Hapo rubani akamwagiza rubani msaidizi kwa kumwambia “lets go bit lower” kwamba tushuke chini zaidi na saa 2:43:07 wakawa urefu wa futi 900 na saa 2:43:07 ndege ilikuwa imebakiza umbali wa kilomita 2.26 kufika kwenye njia.

Saa 2:43:09 rubani akasikika akimtahadharisha rubani msaidizi awe makini na urefu waliopo kutoka usawa wa bahari na akajibu sawa lakini saa 2:43:28 ikajitokeza alarm ikitahadharisha kiwango cha kushuka kilikuwa kikubwa.

Hata hivyo, saa 2:43:38 rubani msaidizi alisikika akipaza sauti “pull up captain” akimtaka aipaishe ndege juu kwa haraka na sekunde moja baadaye alarm ikaendelea kulia. Muda huohuo, sauti ya rubani msaidizi ilisikika tena ikimwambia rubani mkuu “lift up captain” kwamba rubani aipaishe ndege lakini kulikuwa hakuna jibu na akapaza tena sauti “pull up captain” na ndege ikajipiga ziwani.

Mwananchi
 
Kwahiyo ripoti imetamatishaje? Uzembe wa Pilots au Visibility ndo chanzo cha ajali?

Kama Captain angemsikiliza Co-pilot, kwa muda alioambiwa pull up mpaka muda wa kupiga maji, wangefanikiwa kurudi angani salama?

Report nyingi za kibongo ziko open ended zikiacha maswali na kuogopa uwajibikaji. Nasubiri conclusion ingawa naona marubani wameuziwa kicheche ingawa mwisho rubani mkuu ameangushiwa zigo kwa kutokua na maamuzi ya haraka ambayo ni well informed na existing situation.

Sijui lini tutakua na findings ambazo hazina utata! Anyway kama ndo hivyo wacha wenyewe wata draw conclusion.
 
Moshi. Novemba 6 mwaka jana, Tanzania iliamshwa na habari mbaya za kuanguka kwa ndege ya Shirika la Precision Air iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba mkoani Kagera na kusababisha vifo vya abiria 19, huku 24 wakiokolewa.

Ndege hiyo iliondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa 12:10 asubuhi kwenda Bukoba ikiwa na watu 43, marubani wawili, wahudumu wawili na abiria 39 wa ndege hiyo.

Kulingana na ripoti ya pili ya uchunguzi iliyotolewa juzi na Serikali, ndege hiyo ilitarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Bukoba saa 2:25 asubuhi na ilianza maandalizi ya kushuka katika uwanja huo ilipofika saa 1:58.

Ilipofika saa 2:08, kulikuwa na tangazo kutoka chumba cha marubani likiwajulisha abiria kuwa watatua Bukoba saa 2:26 badala ya saa 2:25.
Dakika tisa baadaye, chumba cha kuongoza ndege katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kiliwashauri marubani kuwa hali ya hewa ilikuwa tulivu na kwamba uoni (visibility) ulikuwa ni umbali wa kilomita 10 na hapakuwa na mawingu mengi.

Hata hivyo, wakati wakiendelea kushuka, marubani walianza kuona mabadiliko na dalili za hali mbaya ya hewa kuelekea wanapokwenda, yaani Bukoba.

Katika majadiliano yao, marubani waliona wanaweza kutua uwanja wa ndege wakitokea upande wa ukanda wa mlima ambako kuna njia ya kutua na kurukia namba 13, lakini hiyo ingewezekana kama wangeiona Bukoba kwa chini.

Saa 2:19:32, marubani waliwajulisha kituo cha kuongozea ndege cha Mwanza kwamba wanauona Uwanja wa Ndege wa Bukoba lakini saa 2:24:01 rubani mkuu alisikika akimuuliza rubani msaidizi aangalie kama anaona njia ya kutua.

Ni katika muda wa dakika moja, rubani mkuu alitoa kauli hiyo mara tatu akisema look the runway akimaanisha angalia njia ya kutua na rubani huyo msaidizi akamjibu I am looking, akimaanisha anaangalia kuiona hiyo njia namba 13.

Saa 2:25:45 walishusha magurudumu ya ndege kujiandaa kutua, lakini wakati huo bado njia ya kutua ilikuwa haionekani na hii ni kulingana na mazungumzo yaliyorekodiwa katika vifaa vya kurekodia mazungumzo ndani ya ndege hiyo.

Kulingana na ripoti, saa 2:29:35, rubani alihamishia umiliki (control) kwa rubani msaidizi na hapo walianza majadiliano kuhusu kiwango cha chini cha mafuta kinachotakiwa ili kuweza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Rubani msaidizi akatoa wazo waende kutua Mwanza, kwani itakuwa sahihi zaidi ingawa wakati huo bado walikuwa wakizunguka angani kuutafuta uwanja.
Saa 2:33:33 ndege ilishushwa kutoka urefu wa futi 5,500 hadi futi 5,300 na ilipofika saa 2:33:34, rubani alimwagiza rubani msaidizi kuipeleka ndege uelekeo wa Kemondo na kujaribu tena na hapo rubani aliwatangazia abiria wasingeweza kutua Bukoba kutokana na mvua kubwa hivyo inabidi wasubiri.

Saa 2:34:43 alarm ya umbali kutoka ardhini hadi ilipo ndege (EGPWS), ililia ikionya wako karibu kabisa na ardhi na ilitaka marubani kuipaisha juu na sauti hiyo ya alarm ilisema ‘terrain, terrain, pullup’ kwamba wasishuke tena.
Hata hivyo, kulingana na taarifa hiyo, marubani hawakulifanyia kazi onyo hilo ipasavyo, badala yake waliendelea kujadiliana kuhusu hali ya hewa ya Bukoba na wakawajulisha abiria kuwa wanatakiwa kwenda kutua Mwanza.

Ili kutua Mwanza, kulihitaji kusubiri hadi dakika 20 kwa vile uwanja nao ulikuwa hauonekani vizuri na wakati huo marubani waliendelea kukumbana na ngurumo, radi na mvua kubwa wakati ndege ikielekea Kemondo.

Saa 2:39:56, rubani mkuu alimuuliza rubani msaidizi kama anakiona Kisiwa cha Musila, naye akajibu kuwa amekiona lakini taarifa inasema katika muda wa sekunde 78, bado marubani hao walikuwa wakijaribu kukitafuta bila mafanikio.

Ilipofika saa 2:40 ndege ilishushwa hadi urefu wa futi 4,500 na ilipotimu saa 2:41, rubani alimwagiza rubani msaidizi kwenda spidi ya 102 na aliafiki, lakini sekunde chache baadaye rubani alisikika akimtahadharisha msaidizi wake “watch your speed, speed, speed, i need power” kwamba alihitaji nguvu zaidi.

Hata hivyo, ilipofika saa 2:42:16, rubani msaidizi akasema ameiona njia ya kutua lakini rubani akamuuliza “where is the runway” kwamba iko wapi njia ya kutua na rubani msaidizi akamtaka aitizame kupitia kwake japo mvua inazuia.

Hapo rubani akamwagiza rubani msaidizi kwa kumwambia “lets go bit lower” kwamba tushuke chini zaidi na saa 2:43:07 wakawa urefu wa futi 900 na saa 2:43:07 ndege ilikuwa imebakiza umbali wa kilomita 2.26 kufika kwenye njia.

Saa 2:43:09 rubani akasikika akimtahadharisha rubani msaidizi awe makini na urefu waliopo kutoka usawa wa bahari na akajibu sawa lakini saa 2:43:28 ikajitokeza alarm ikitahadharisha kiwango cha kushuka kilikuwa kikubwa.

Hata hivyo, saa 2:43:38 rubani msaidizi alisikika akipaza sauti “pull up captain” akimtaka aipaishe ndege juu kwa haraka na sekunde moja baadaye alarm ikaendelea kulia. Muda huohuo, sauti ya rubani msaidizi ilisikika tena ikimwambia rubani mkuu “lift up captain” kwamba rubani aipaishe ndege lakini kulikuwa hakuna jibu na akapaza tena sauti “pull up captain” na ndege ikajipiga ziwani.

Mwananchi
Hapo kuna mawili, kwa kuisoma tu report unaweza ona kuwa maruban ndio awazembe.

Lakin ukisoma report katikati ya mistari nazan wawajibikaji wakubwa walikuw ni tower wao wanaona hali ya hewa mbaya na ndege inahangaika angan takriban dak 25 wangeamuru ndege iende mwanza mara moja. Maon yang tuu maana sjui muamuzi wa mwisho n nan kwenye hayo maswala
 
Kila mtu aamue anavyoone yeye, kila mtu alaumu mtuwake, mimi namlaumu Raila Odinga
Imenikumbusha report ya Escrow wakati wa Ludovick Uttoh…kuna page ukisoma ilikuwa inasema ule Mzigo ulikuwa wa Serikali na kuna page ilikuwa inasema ni mzigo wa kina Rugemalila na conclusion pia ikasema either wa Serikali or wa kina Seth

Chawa wa kila upande wakatumia report ya CAG kwa namna walivyopenda kutetea or kupopoa
 
Kwa mujibu wa hiki kilichoripotiwa na mwananchi, hatuna wa kumlaumu! Inavyoonekana uwanja wa mwanza pia wasingeweza kutua kwani nako kulikuwa na hali mbaya ya hewa. Vinginevyo wangetakiwa kwenda Chato!
 
Back
Top Bottom