Jamani hii kitu ni ndege ama nini

Jamani hii kitu ni ndege ama nini

Mada kama hii ililetwaga humu jamvini 2014. Mda mrefu wabongo tumelishwa sana matango na kamba iyo ni rocket
na kama unakumbuka tulivyojadiri hapa ndio serikali wakaanza mchakato wa kununua rada zile tano kwa bilion 67 moja dsm ,zanzibar, kia,mwanza ,mbeya
siyo mbaya wakatushukuru member wa hapa jf naamini kwa 100% walichukua wazo hapa
. 😎 🤣
 
Acheni stori nyingi, hizi ni ndege za kawaida ila zikimwaga mafuta ndo utaona hivo. Kwa siku hizi sio common ndege kumwaga mafuta ndo maana hizo picha hazionekani sana, ila zaman kidogo ilikuwa ni kawaida saana ndege kuwa na mafuta mengi na kutua viwanja visivo salama ilikuwa lazima ndege zimwage mafuta ndo maana tulikuwa tunaona hizo ndege kila mara, ila mara baada ya kuongezeka kwa usalama wa airports na teknolojia za safari then hiyo kumwaga mafuta ni kama imeisha except kwenye emegency landing tu utaona ndege ikiwa hivo

Not true
 
ndege hiyo inapita internation air space ila kwa kuomba na wanalipia ushuru lakini kama nchi husika mna rada ya kisasa kama ambazo zimefungwa sasa tanzania ,zamani walikuwa wanajipitia tu bila ushuru bila kuomba kifupi nchi ilikuwa uchi kabisa

😎
kuna vibali vinatolewa na IATA na vile vya IASA ni tofauti kiutendaji.
Hawa wa anga la kimataifa wanahusiana na IATA ilihali wale wa anga la nchi husika wanasimamiwa na IASA mfano TCAA, FAA n.k.
 
Safi sana maana zamani tulilishwa matango pori,

Wakuu nahitaji ufafanuzi wa kina kama hamtojali kwa wale wanaojua ili nami nijue zaidi

Bado najiuliza maswali

Kama ni ndege ya kawaida kama hizi za kwetu kwa hiyo inaweza kubeba abiria?

Inaruhusiwa kuruka umbali gani ndo itue?

Je hizi za kwetu kwa zinaweza kuruka kwa kiasi hicho?

Huwa zinabeba nini hizo zinazopaa umbali huo?
 
Kwa ufupi tu kinachotokea pale ni kwamba,kama umewahi kuishi sehemu zenye baridi kama Iringa au Mbeya kuna muda ukiamka asubuhi ukiongea unatoa moshi/mvuke mdomoni sasa basi hewa inayotoka mdomoni inakua ni ya moto kuliko inayokuzunguka nje. Hivyo inakua inalazimishwa kupoa itokapo mdomoni hapo ndipo unaona ule moshi ukipumua kupitia mdomo na ndivyo hivyo hivyo kwenye ndege zinazopita kwenye anga za kimataifa pale kunakua na baridi kali kwa hiyo hewa ya joto kali inayotoka kwenye jet engine ikikutana na baridi kali inalazimishwa kupoozwa hapo ndipo unapo ona ule moshi/mvuke.

Nadhani utakua umeelewa kwa ufupi mleta uzi
Wazee wetu walijitahidi kujibu ili kupunguza maswali. Ufafanuzi mzuri sana huu.
 
Ndege yenye Jet engine hutoa hizo Condensation trails, husababishwa na hewa ya moto iliyotoka kwenye engine inapokutana na hewa ya ubaridi, hupoa haraka na kutengeneza hilo kama wingu.

Rocket sio ndege wala haina uwanja wa kutua bali huwa na lauching pad, pia rocket husafiri vertical na sio Horizontal,
Rocket sio ndege bali ni chombo kinachotumika kupeleka vifaa kwenye sayari za mbali.
Elimu Dunia!
 
Safi sana maana zamani tulilishwa matango pori,

Wakuu nahitaji ufafanuzi wa kina kama hamtojali kwa wale wanaojua ili nami nijue zaidi

Bado najiuliza maswali

Kama ni ndege ya kawaida kama hizi za kwetu kwa hiyo inaweza kubeba abiria?

Inaruhusiwa kuruka umbali gani ndo itue?

Je hizi za kwetu kwa zinaweza kuruka kwa kiasi hicho?

Huwa zinabeba nini hizo zinazopaa umbali huo?
dreamliner👇
1597750216929.png
 
Hiyo ndege inatembea mda wote huku inamwaga mafuta?
Acheni stori nyingi, hizi ni ndege za kawaida ila zikimwaga mafuta ndo utaona hivo. Kwa siku hizi sio common ndege kumwaga mafuta ndo maana hizo picha hazionekani sana, ila zaman kidogo ilikuwa ni kawaida saana ndege kuwa na mafuta mengi na kutua viwanja visivo salama ilikuwa lazima ndege zimwage mafuta ndo maana tulikuwa tunaona hizo ndege kila mara, ila mara baada ya kuongezeka kwa usalama wa airports na teknolojia za safari then hiyo kumwaga mafuta ni kama imeisha except kwenye emegency landing tu utaona ndege ikiwa hivo
 
Ndege yenye Jet engine hutoa hizo Condensation trails, husababishwa na hewa ya moto iliyotoka kwenye engine inapokutana na hewa ya ubaridi, hupoa haraka na kutengeneza hilo kama wingu.

Rocket sio ndege wala haina uwanja wa kutua bali huwa na lauching pad, pia rocket husafiri vertical na sio Horizontal,
Rocket sio ndege bali ni chombo kinachotumika kupeleka vifaa kwenye sayari za mbali.
Umeua Mkuu. Yaani nilipoona thread karibu nicheke. Umejibu kisomi sana, watu kama nyie mnastahili heshima zenu humu JF. Ajabu atakuja yeboyebo anabishana na wewe!

Actually mtoa mada angepanda ndege akikaa dirishani anaweza pia kuona hiyo trail ndege inapopita eneo lenye super saturated air na baridi. Na nimefurahi ulivyofafanua juu ya contrails (condensation trails). Wengi wanadhani ni moshi wa ndege au rocket! Labda kwenye rocket wanamaanisha ni jet engine aircraft.
 
Kwa uelewa wangu huu mdogo, ila wanaojua zaidi watasema hii ni Ndege Kasi aina ya Concorde ambayo kwa Afrika inatua tu Cairo na Cape Town.
Concorde hakuna siku hizi hazisafiri kitambo sana zilikua zinakula sana mafuta so ikawa hasara kuzi oparate wakazipiga chini saizi zimebaki makumbusho
 
Kweli ndege inapotoka point A to point B rubani ana calculate umbali ,speed per miles kiasi cha mafuta na uzito wa ndege hivyo kama amatembea vzuri na amefika destination alafu hali ya upepo ikawa na mgandamizo mdogo yaani upepo wa kubeba uzito wa denge wakati inatua isitue kama mzigo kupunguza mshindo inabidi apunguze mafuta ili kupunguza uzito wa ndege na kumbuka mafuta yana kaa kwenye mabawa na huwa ya funguka wakati wa kupaa ili kasi yandege kwenye run way inasaidia kuinyanyua ndege juu kwa kukata upepo na mabawa hufunga kuinama chini wakati wakutua ili upepo upite kwa kiasi hivyo ndege huwa nzito hivyo akiona ndege ni kubwa na hakuna hali nzuri ya kutua hupunguza mafuta kama yapo mengi lakini ni mara chache maana ndege hutembea kwa vipimo ili kumaintain uzito angani hakiona halimbaya ya hewa au hatari ya kuanguka hufungua mafuta yatoke ili ikianguka isilipuke nimekujibu kwa njia ya jadi lkn utakuwa umenielewa
Huo ni uongo Mkuu, kama huelewi jambo ni vema ukae kimya kuliko kuleta stori za wajuba wa vijiweni

Ndege inamwaga mafuta wakati wa kutua kwa emergency tu. Na ndege zinazomwaga mafuta ni zile ambazo zilikuwa zifanye safari ya masafa marefu (long haul) lakini muda mfupi baada ya kuruka ikapata emergency inayomlazimu atue wakati bado ana mafuta mengi, na uzito wa mafuta, mizigo na abiria ni mkubwa akitua bila kupunguza uzito ataharibu landing gear. Pia wanaweza kumwaga mafuta kama emergency landing ina hatari ya moto, kwa mfano, kama landing gear imekataa kutoka na hivyo inabidi atue kwa tumbo. Atamwaga mafuta kupunguza uwezekano wa moto mkubwa. Na pia uzito mkubwa wa ndege maana yake umbali mrefu wa ku brake, kwa kuwa momentum inakuwa kubwa.

Ndege ya kwenda Mbeya kutoka Dar ikipata emergency hata eneo la Kibaha tu inaweza kurudi na kutua bila kumwaga mafuta kwa kuwa ndege huwa hawajazi mafuta kwa kusema weka full tank. Hata ndege ya kwenda South Africa inaweza kurudi na kutua bila kumwaga mafuta, kwa kuwa mafuta atakayokuwa amechukua sio mengi kiai hicho kwa safari ya masaa matatu ya kwenda Johannesburg

Hakuna pilot atamwaga mafuta baada ya kufika destination eti aliweka mafuta mengi au alipatwa na mgandamizo mkubwa njiani. Hizo n stori za vijiweni.
 
Hii nadhani kwa Tanzania kila mtu ameshawahi kuona ikipita angani hasa pasipo kuwa na mawingu. Wakati mdogo, mzee aliniambiaga inaitwa roketi ni jamii ya ndege lakini Africa hamna uwanja wa kutua alafu ikitua humwaga mafuta Kwanza lakini niki-Google sioni story yake kwa anaejua nisaidie.

Hyo haiitwi rocket jombaa hiyo inaitwa jet, rockets ni zile ndege zinaenda mwezini huko jombaa.
 
Haya hebu mwaga madini ewe mtaalamu.
Nilishajibu

Ndege inamwaga mafuta wakati wa kutua kwa emergency tu. Na ndege zinazomwaga mafuta ni zile ambazo zilikuwa zifanye safari ya masafa marefu (long haul) lakini muda mfupi baada ya kuruka ikapata emergency inayomlazimu pilot atue wakati bado ana mafuta mengi, na uzito wa mafuta, mizigo na abiria ni mkubwa akitua bila kupunguza uzito ataharibu landing gear. Pia wanaweza kumwaga mafuta kama emergncy landing ina hatari ya moto, kwa mfano, kama landing gear imekataa kutoka na hivyo inabidi atue kwa tumbo. Atamwaga mafuta kupunguza uwezekano wa moto mkubwa. Na pia uzito mkubwa wa ndege maana yake umbali mrefu wa ku brake, kwa kuwa momentum inakuwa kubwa.

Ndege ya kwenda Mbeya kutoka Dar ikipata emergency hata eneo la Kibaha tu inaweza kurudi na kutua bila kumwaga mafuta kwa kuwa ndege huwa hawajazi mafuta kwa kusema weka full tank. Hata ndege ya kwenda South Africa inaweza kurudi na kutua bila kumwaga mafuta, kwa kuwa mafuta atakayokuwa amechukua sio mengi kiasi hicho kwa safari ya masaa matatu ya kwenda Johannesburg

Hakuna pilot atamwaga mafuta baada ya kufika destination eti aliweka mafuta mengi au alipatwa na mgandamizo mkubwa njiani. Hizo n stori za vijiweni.
 
Kwa uelewa wangu, miale ya jua inavyokua inatoka kwenye source (jua) kuja ardhini huwa haichomi inakua na (long wave) bali kinachosababisha tuhisi tunaungua ni pale inapo hit ground ikiwa inarudi juu inakua na short wave hivo tuliopo ardhini tunahisi kuungua maana miale inapokua inarudi kwenye source (jua) inaanza kukutana na sisi tuliopo ardhini, na kadiri inavyozidi kurudi juu ndivo inapoteza nguvu inakua (long wave) hiyo ndiyo sababu huko anga la mbali inakua baridi na huku chini tunahisi joto, kwa anaeelewa zaidi atanikosoa , Asantee
uko sahihi mkuu physics form two hii sema wengi humu wakati sisi tunasoma wao walikua wanawinda ndege na manati kidding ha ha ha ha
 
nilijua ni vumbi kwenye barabara ya ndege angani

huko angani kuna trafiki?
 
Back
Top Bottom