Jamani eti hii kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani eti hii kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LOOOK, May 18, 2011.

 1. LOOOK

  LOOOK JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,392
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wajumbe kwanza ningependa kuwashukuru sana baadhi ya watu wanao jaribu kudadavua waasisi wa chdema na ccm sasa ambacho naweza kusema ni kwamba si jambo la hekima sana tukianza kuzalisha hayo kwa sasa na kuyafanya yawe mwongozo katika maisha yetu hata kama yapo.

  Nijuavyo mimi chochote kile ambacho kitaanzishwa katika jamii ya binadamu nilazima kitawahusu binadamu wenyewe sasa naomba kuuliza inamana tukianza kuyasema hayo tunataka mtu au muasisi wa kitu chochote asiwe na dini au kabila?lakini babdo mtasema cha wapagani, sababu akishakuwa na dini kila alicho anzisha mtasema kitahusishwa na dini yake na akiwa na kabila kila kilicho anzishwa kitahusishwa na kabila lake na kama ni hivyo basi pia tutafute pia rangi za hao waasisi wa hivyo vyama walikuwa na rangi gani ili kama walikuwa ni weusi tuite pia chama cha watu weusi na kama walikuwa weupe basi tuite ccm au chadema ni chama cha watu wenye rangi nyeupe na kama tutaendelea hivyo basi pia tutarudi tena na kuangalia wasisi walikuwa warefu au wafupi na kama ni warefu turudi na kusema ccm au chadema ni chama cha warefu au wafupi.

  Mimi naona hii si sawa kwani binadamu yoyote yuyle lazima ana dini yake na kabila lake sasa tukianza kuhusisha kila kinacho anzishwa naye tuseme ni cha kabila lake au dini yake basi tutaona kila kitu tunacho fanya hapa ni cha dini au kabila fulani baadae tutaanza kutafuta hata muasisi wa hii jf kama ni muislamu au mkritu au ni kabila gani ili tuanze kusema kwamba hata jamii forum ni ya wakristu ama ni yawaislamu.

  Sasa mimi nafikiri tusifike huko kwani tutaendelea kupandikiza sumu mbaya kwa wale ambao huwa hawayafikirii mambo kwa mapana na marefu ambao husubiri kisemwe ili wakifuate ,naweza sema kwamba hapo hakuna udini kwani chochote kinacho anzishwa lazima kitamuhusu mtu wa dini au kabila fulani na sisi wapokeaji tunatakiwa kukipokea pasipo kuangalia ninani muasii na alikuwa na dini gani na kabila gani ili mradi tu kiwe chema kwa jamii husika kwani tukuangalia hayo tutakosoa mengi sana kinacho takiwa hapo ni kuwaunga mkono wale tunao ona wanauchungu na jamii pamoja na nchi kwa ujumla pasipo kujali muasisi ninani bali angalia wewe kitakuafaa vipi? Na kuacha na ushabiki usio na maana nafikiri hapo itakuwa vema zaidi kuliko kuanza kuchambua hiki kaazisha huyu sijui mkristo au muislamu sijui mchaga sijui mdigo haitakiwi chamno angalia wewe kile kinakufaaje?ndipo ukiunge mkono kama utaona kinakufaa,,,

  Nakama utaona hakikufai waweza acha ingawa naamini hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye anaweza kukiacha kile kinacho mfaa sababu eti yeye cha dini fulani huu ni utumwa wa imani na kama ndo ivo hata vyakula tunavyo kula pia vina makabila yake tuache na kila mtu ale cha kabila lake tuone kama itawezekana tusifanye ivo ndugu zangu tufanye kile ambacho tutaona kina kufaa wewe na jamii nzima pasipo kuwa na ubinafsi wala mawazo ambayo kimsingi haya mshiko wowote bali ni ubinafsi ambao tunataka kuupandikiza katika jamii.

  lakini pia
  huwezi ukaacha mkuki ukuchome kwa vile eti umerushwa na baba yako ni lazima utaukwepa tu sababu unajua ukikuchoma utakuumiza na maumivu hayajali kaurusha baba au nani,, maumivu yatakuwa ni yaleyale sasa, ukiona mtuhataki kukwepa mkuki eti kisa karusha baba yake na anamuheshu, huyo hana akili timamu kabisa katika akili yake.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  tubomoe tutajenga baadae
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  font, size and paragraphs please - utatumaliza macho.
   
 4. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ndugu, waka paragraph usomeke vizuri. Hoja ni nzuri ila umeiunga kama jongoo!
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,766
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  nakubaliana na kauli ya kauk
  kauli za ubaguzi zinapotolewa na viongozi wa juu wa chama zinamadhara makubwa sana!
  Ona sasa wananchi wanakata tamaa! Nape awaombe msamaha wachaga,
  Bora angefanya kama mwenyekiti wake hataji majina wakati huwa tunajua anakisema chama gani!
   
 6. c

  chigwiye JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umenikumbusha ule wimbo'bomao eee! bomoa eee,bomoa mamaaa tutajenga keshoooo,tutajenga keshooo,imaraaa' sjui ulishazaliwa? serikali iliufungia huo wimbo kupigwa redioni.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  mazoea ya kupost kule kwetu!
  lAKINI HII AVETARI TAYARI IPO SOMEWHERE HUMU!

  [​IMG] Junior Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Join Date : 17th May 2011

  Posts : 5
  Thanks0Thanked 0 Times in 0 Posts

  Rep Power : 0
   
 8. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  kweli kabisa Kauk
  Huyu Nape hataki kukwepa mkuki uliotupwa na .......sasa umemchoma jumla.
   
Loading...