Jamani, Dr. Ulimboka yuko wapi siku hizi?

Jamani, Dr. Ulimboka yuko wapi siku hizi?

Kitaani wanadai kuwa keshapigwa 'kufuli' yuko Uingereza anakula maisha na familia yake. Sijui kama ni kweli au laa
Sawa na yule anayekula mihogo Canada?
 
T
Usiwakumbushe watu ule mgomo wa madaktari pale Muhimbili watu wengi walipoteza maisha kwa kukosa Huduma na iliumiza sana watu wa chini.

Wengi wenye uwezo waliwatoa wagonjwa wao na kuwapeleka hospital za kulipia.

Dr Ulimboka anajua mwenyewe na familia yake alipo wala sitaki kabisa kulisikia hilo jina.

Nakumbuka nimewahi kufanya kazi na kaka yake naye ni Daktari pia tabia zao zinafanana.
Tabia zao zikoje ?
 
ana afya njema lakin ndo kibogoyo tena
Kule chini ofisi kuu nasikia nako waliminya minya na koleo na huenda yale mawe mawili waliyavunja. Umeongea na wife wake kuwa ofisi inaoperate au ilishafungwa?!
 
Inafurahisha sana kuona watu wanamcheka na kumkebehi Dr. Ulimboka. Ya Mungu mengi, naamini wale aliokuwa anawapigania dhamira zao zitawahukumu milele. Tusishabikie fujo na mabavu, mbona Kenya madaktari wamegoma miezi mitatu sasa na hakuna aliyekatwa korodani? Hatuoni aibu kwamba wenzetu wanasuluhisha mambo yao kistaarabu? Kumtesa mtu kwa kudai haki yake ni ujima wa hali ya juu.

Kamwe sitashabikia mateso kwa watu wanaodai haki zao. Watu waliozoea kutesa hawachagui. Juzi ilikuwa kwa daktari, leo kwa mwanamziki, kesho mwanasiasa, kesho kutwa mshabiki wa siasa, wiki ijayo zamu ya wafanyabiashara, mwezi ujao zamu ya wakulima. Tukemee vyombo vya dola vinavyofanya kazi kihuni(e.g. sodomy), hakuna kiumbe-hata mbuzi, anayestahili kufanyiwa hivyo.
Hata Mimi sishabikii Kuteswa kwa binadamu yoyote hivi utajua ule mgomo uligharimu Maisha ya watu wangapi? Tuliokuwa tunauguza kipindi kile ndo tunajua uvhungu
 
Shujaa alusema ukweli! Romakaficha! Mungu anakuona! Lete diffender! Kumbeeeh M.....a
 
Hata Mimi sishabikii Kuteswa kwa binadamu yoyote hivi utajua ule mgomo uligharimu Maisha ya watu wangapi? Tuliokuwa tunauguza kipindi kile ndo tunajua uvhungu
Watanzania wanakufa kila siku kwa magonjwa yanayotibika sababu ya huduma mbovu za hospitali zetu. Hupati huduma bora bila kutoa rushwa. Ni kama kuna passive resistance. Ni heri watu wagome wasiende kazini kuliko wakaenda halafu wakafanya kazi kwa kinyongo. Ule mgomo ulikuwa na faida moja kubwa-ulifungua mjadala wa kitaifa kuhusu huduma za Afya. Tulikuwa na fursa ya kurekebisha tatizo hilo once and for all. Haikutumika ipasavyo.

Nasikitika kwa mliopoteza wapendwa wenu kwa sababu ya mgomo. Mimi pia ni mhanga wa huduma mbovu za afya-nimepoteza ndugu kwa sababu ya magonjwa ambayo yanaweza kudhibitiwa. Hata hivyo sion kama ni busara kushabikia violence kwa sababu ya mtu anayedai haki yake. Pia kumbuka migomo haiepukiki-ndio maana ikatungiwa sheria. Serikali inatambua kwamba ni haki ya mfanyakazi kugoma. Lakini hakuna popote ambapo serikali inampa raia haki ya kuteswa na kujeruhiwa na dola. Hoja yangu inatokana na ukweli kwamba wapenda vurugu hawana mipaka. Wewe pia ni mhanga mtarajiwa wa yaliyomkuta Ulimboka.
 
Watu mnaongea utani kwa jambo serious km lile.....
Sikubaliani kwa alichofanyiwa kwa sababu tu ya kudai haki za madaktari.......
Leo kwake kesho kwa wengine.....ni uovu kutetea kutekwa na kutesa.......baada ya ulimboka ccm walipoona hakuna wa kuwakataza sasa wanaendelea kuteka na kutesa.....si unajua tena ukila nyama ya mtu

Ungekuwa ulipoteza Ndg yako wa karibu kwny ule Mgomo usingeandika ulichoandika
 
Watanzania wanakufa kila siku kwa magonjwa yanayotibika sababu ya huduma mbovu za hospitali zetu. Hupati huduma bora bila kutoa rushwa. Ni kama kuna passive resistance. Ni heri watu wagome wasiende kazini kuliko wakaenda halafu wakafanya kazi kwa kinyongo. Ule mgomo ulikuwa na faida moja kubwa-ulifungua mjadala wa kitaifa kuhusu huduma za Afya. Tulikuwa na fursa ya kurekebisha tatizo hilo once and for all. Haikutumika ipasavyo.

Nasikitika kwa mliopoteza wapendwa wenu kwa sababu ya mgomo. Mimi pia ni mhanga wa huduma mbovu za afya-nimepoteza ndugu kwa sababu ya magonjwa ambayo yanaweza kudhibitiwa. Hata hivyo sion kama ni busara kushabikia violence kwa sababu ya mtu anayedai haki yake. Pia kumbuka migomo haiepukiki-ndio maana ikatungiwa sheria. Serikali inatambua kwamba ni haki ya mfanyakazi kugoma. Lakini hakuna popote ambapo serikali inampa raia haki ya kuteswa na kujeruhiwa na dola. Hoja yangu inatokana na ukweli kwamba wapenda vurugu hawana mipaka. Wewe pia ni mhanga mtarajiwa wa yaliyomkuta Ulimboka.

Nakuombea kwa Mungu Siku ukiwa na Mgonjwa wako wa karibu sana ndipo na Madaktari nao wagome ndio ujue hasa Madhara ya Yule Muuaji Ulimboka ambae hakupaswa kuwa anaishi mpaka sasa!

Kuna Mama/Dada/ wake wa Watu wamefia kwny Ward za uzazi kwa kukosa tu daktari wa kuwafanyia Operation ndogo sana ya Uzazi!

Dhulma na hujuma aliyowafanyia Wanyonge wa Nchi hii hakika atasimama kujieleza Mbele ya Mwenyezimungu
 
Kwa hiyo wewe uliyepoteza ndugu yako kutokana na mgomo unasemaje ni vema yale aliyofanyiwa Dr. Ulimboka?

Angeuawa hata kwa Makombora ya kutungulia Ndege bado ingekuwa ni adhabu ndogo ukilinganisha na Mateso aliyosababisha!

Yule Kijana ni Miongoni mwa Viumbe wenye roho Mbaya sana kusomea Taaluma ya utabibu

Mwenyezimungu atatenda haki kwa ukatili aliosimamia kufanyika
 
Kwa hiyo wewe uliyepoteza ndugu yako kutokana na mgomo unasemaje ni vema yale aliyofanyiwa Dr. Ulimboka?

Angeuawa hata kwa Makombora bado ingekuwa ni adhabu ndogo ukilinganisha na Mateso aliyosababisha!
 
Back
Top Bottom