Jamani, Dr. Ulimboka yuko wapi siku hizi?

Jamani, Dr. Ulimboka yuko wapi siku hizi?

Usiwakumbushe watu ule mgomo wa madaktari pale Muhimbili watu wengi walipoteza maisha kwa kukosa Huduma na iliumiza sana watu wa chini.

Wengi wenye uwezo waliwatoa wagonjwa wao na kuwapeleka hospital za kulipia.

Dr Ulimboka anajua mwenyewe na familia yake alipo wala sitaki kabisa kulisikia hilo jina.

Nakumbuka nimewahi kufanya kazi na kaka yake naye ni Daktari pia tabia zao zinafanana.
 
Inafurahisha sana kuona watu wanamcheka na kumkebehi Dr. Ulimboka. Ya Mungu mengi, naamini wale aliokuwa anawapigania dhamira zao zitawahukumu milele. Tusishabikie fujo na mabavu, mbona Kenya madaktari wamegoma miezi mitatu sasa na hakuna aliyekatwa korodani? Hatuoni aibu kwamba wenzetu wanasuluhisha mambo yao kistaarabu? Kumtesa mtu kwa kudai haki yake ni ujima wa hali ya juu.

Kamwe sitashabikia mateso kwa watu wanaodai haki zao. Watu waliozoea kutesa hawachagui. Juzi ilikuwa kwa daktari, leo kwa mwanamziki, kesho mwanasiasa, kesho kutwa mshabiki wa siasa, wiki ijayo zamu ya wafanyabiashara, mwezi ujao zamu ya wakulima. Tukemee vyombo vya dola vinavyofanya kazi kihuni(e.g. sodomy), hakuna kiumbe-hata mbuzi, anayestahili kufanyiwa hivyo.
 
alifanyiwa sadistic method of resistance neutralization
 
mbona hakuna aliyejibu swali yuko wapi dk.ulimboka kwa sasa ?

hata mm ningependa kujua
 
Ukituchezea tunakuonya ukizidisha tunakutembelea, usiposikia tunakupoteza Yeriko kimya, Mnyika kimya chunga sana.
hahaaaa JK alimsulibisha ulimboka waziwazi kabisa, alilalamika sana Ila vyombo vya usalama havikufuatilia ishu yake.
 
Hii jamhuri ya Tz hii imetenda makuu kuliko lucifa! Dr. Ulimboka alikutana na watu aina ya mbwamwitu! aliteseka sana!
 
Ulimboka ni Muuaji ambae ni makosa tu ya kisheria ndio kimemsitiri, ilifaa auawe kwa Kombora Kama kule Korea Kaskazini angeleta ule ushenzi wake

Ingekuwa Nchi za Wenzetu angeshtakiwa kwa kuchochea Mgomo uliosababisha vifo na Madhara makubwa sana kwa Raia Maskini kuliko hiyo Serikali
 
Nasikia yuko nchi za nje ila sitasema ni nchi gani kwa sababu za kipolisi.
 
Watu mnaongea utani kwa jambo serious km lile.....
Sikubaliani kwa alichofanyiwa kwa sababu tu ya kudai haki za madaktari.......
Leo kwake kesho kwa wengine.....ni uovu kutetea kutekwa na kutesa.......baada ya ulimboka ccm walipoona hakuna wa kuwakataza sasa wanaendelea kuteka na kutesa.....si unajua tena ukila nyama ya mtu
 
Mara ya mwisho alinitibu kichaa toka hapo sijawahi kuonana naye
 
Back
Top Bottom