Ndugu wanajamii,nina rafiki yangu ambaye tunafanya nae biashara hapa Dar es Salaam,yeye ameoa miezi mitatu iliyopita na mkewe ana mdogo wake ambaye alinitambulisha kwake siku ya harusi maana nilimfuata ubungo na gari yangu kutokana na yeye kubanwa na shughuli za harusi.Katika mazungumzo yetu kama majirani maana tumejenga jirani shemeji yake ametokea kunipenda na mimi sikuona shida na sasa ni kama mwezi umepita tangu tuwe na mawasiliano na huyu shemeji yake.Wiki iliyopita nilimpigia simu yule shemeji yake ila alikuwa anaoga na jamaa ndio alipokea simu na kuniambia anaoga kifupi aliitambua sauti yangu na akaniuliza nimepata wapi namba yake nikamwambia amenipa mwenyewe(shemeji) yake.Wiki iliyopita amenitumia meseji za kunitukana na hata biashara anasema hataki tushirikiane na leo amekuja kuchukua vitu vyake ofisini akisema nimemkosea heshima sana na mimi sijagombana nae zaidi ya kumwambia afikiri vizuri kabla sijamjibu ila amenikasirisha sana na kuniudhi.Jamani naombeni ushauri wenu nina makosa kwa hili na nimwache shemeji yake anayedai ananipenda kwa sababu ya jamaa?Samahani kwa maneno mengi