Jakaya Mrisho Kikwete ni nani?

Jakaya Mrisho Kikwete ni nani?

Ni "mpigaji"mzuri sana yuko nyuma ya escrow,epa, richmond,anaondoka ikulu akiwa multi billionear
 
By Paul Alex:
Nape ni mdomo tu wa wakubwa ndani ya CCM, na kiukweli sioni kama CCM ina mkubwa mwingine zaidi ya Kikwete!
Kuna namna wana CCM wanapaswa wamuone Kikwete.Ni mtu anayejaribu mambo bila kufanya hesabu, bila kujali tuseme!
He has a lot of power and he is simply misusing it! Swali ni kuwa mtu mwenye nguvu ya amiri jeshi mkuu alieonyesha tayari dalili tulizoona sijui ataishia wapi kuhakikisha anaibuka mshindi katika hii vita ya kunyang'anyana fito?
Nape hawezi kumuita Kingunge nguo ya ndani iliyochafuka.Hata kama kweli angekuwa hivyo, maneno ya busara kidogo yangepooza makali ya kuondoka kwa kingunge!
Seriously mimi ni mwanachama wa CHADEMA ila napenda sana kupima effect ya maamuzi na mikakati! Nikiangali CCM sioni mikakati inayofanya kazi leo wala itakayofanya kazi miaka kumi ijayo.Naona Kama vile kuna mtu anarusha jiwe kwenye giza alafu anafunga macho akiomba lilenge ndege!
Mdomo wa Nape umeshaigharimu sana CCM na utaendelea kuigharimu. Mtu mwenye mkakati wa kutumia mdomo wa Nape anakosea. Atafanikiwa kutoa ya moyoni kwake kwa kupitia Nape lakini hatafanikisha lolote zaidi ya hilo.
Baadae Nirudi kwa Nape, Nape ni kijana na makubaliano ya kisiasa sio ndoa iliyofungwa mbinguni.Ni makubaliano ya muda mfupi yanayoweza kuvunjika, siasa ni kazi kama kazi nyingine. Usikubali tu mdomo wako kutumika kuongea vitu vichafu.
Kwanza vinakuchafua wewe na ukitaka kujua hili angalia tu mfano wa kujisaidia.Mtu anapoharisha, tumbo linajisikia vizuri sana. Lakini sehemu uharo unapotokea panachafuka. Na wewe usikubali kuwa hiyo sehemu!
Pili ni dhambi tu kwa Mungu bila kujali wewe ni wadini gani!
Tatu unajitengenezea maadui wengi ambao wewe binafsi huna ugomvi nao.
Nne, unajitengenezea Legacy ya kuwa mwanasiasa mwenye mdomo mchafu kuliko wote.Hakuna mtanzania atataka kuongozwa na mtu anayejisaidia kwa kutumia mdomo.
Politics is a profession, so start being professional. Natamaani siku nikiingia kwenye siasa nikutane na CCM yenye wanasiasa mahiri wenye hoja ili tuwashe moto.
Sio nikutane na walevi wenye matusi tu mdomoni!


Nimeipenda analysis yako. Yaani mpaka inashangaza. Walianza kupiga makelele akina Mgeja zamani sana kwamba jamani chama mnakiendesha ndivyo sivyo. Wakaambiwa watashughulikiwa. Hakuna busara wala maelewano. Chama chenye mwelekeo huungana na kumuunga mkono mgombea wao. Leo hii wagombea 30 hakuna hata mmoja aliyesimama na Magufuli jukwaani kuonyesha kuwa wako pamoja. Inatia aibu sana.
Mwanzoni Lowassa alipoondoka mi sikuwa na wasiwasi na nilidhani kuwa CCM wana strategy of containment kali sana kwani ni mtu wanayemjua vizuri na kimsingi ndiyo wamemlea na kumuacha akijitandaza na kujiimarisha kwa makumi ya miaka. Kumbe hawakuwa na strategy yo yote na wanajaribu hapa na pale bila mafanikio. Flicking unbelievable! Na mtu ungedhani pengine wamejifunza kitu. Halafu katibu wa propaganda anakuja na maneno kama haya. They haven't learned anything.
Ngoja tuone gemu litakavyoisha lakini nadhani hawatakubali kuachia madaraka hivi hivi. Wapinzani inabidi mlitambue hili na mjiandae kisaikologia



Nashukuru kama umekuwa na mtazamo huo, something very wrong is going on in CCM!
Na kawaida mtu ukikosa mkakati wa kufanikisha jambo huwa anaishia kutumia nguvu.
Kikwete hataki Lowassa aongoze nchi hii,hili hata ukimuuliza mtoto mdogo atakwambia.Na alioyafanya tayari kwa Lowassa na anayoyafanya kwa kupitia Nape yanakwambia wazi wazi kuwa yuko on war gear.
Tatizo langu ni kuwa rais ni mtu mwenye nguvu sana na hili mtu yoyote asijidanganye!
Watu waliobaki nae wanajua fika mtaani hawawezi kushinda na wameweka matumaini yao yote kwenye nguvu za rais.
Siko sana karibu na Lowassa lakini naamini kuna watu wa karibu na yeye wanapita huku.
Kuamini kwamba Kikwete atakaa asimame jukwaani kusema Rais ni Lowassa ni ndoto za mchana!
Kuwaweka wananchi mbele wakabiliane na nguvu ya rais, japo ndilo jambo linalofanywa sehemu nyingi duniani, ni kuwaumiza na japo haki haiombwi lakini ni busara tu kuwapunguzia wananchi mzigo huu.
Najua kuna watu wazima huko juu, so please, think of a strategy ili kama inafaa wananchi kikombe hiki tukiepuke, ila kama haifai, basi, mapenzi ya Mungu yatimizwe!

Hili la nape hata mi linanikera,na kiukweli naamini hata familia ya Kingunge imekerwa,Kingunge hakuzungumzia personal issues amezungumzia juu ya chama,Nape alipaswa kuja na majbu ya kisera na kiitikadi
 
Kuliko nipigwe ban la maisha JF, bora ni nyamaze. Ilaa!!!! Bahati yake...
 
mliambiwa mkapuuza sasa mmeona balaa lake!

Na balaa hilo hilo la kuvutiwa na sura, na kuvutiwa na uwingi wa watu ndilo mnataka kulirudia mwaka huu kwa Lowasa? no way., kuchagua Lowasa ni kurudisha aina ya uongozi wa Kikwete madarakani, na hatupo tayari kuendelea kuwa na aina ya uongozi wa Kikwete madarakani, ndio maana tunasema MAGUFULI 4 CHANGE.
Magufuli 4 change
Pamoja, tunaweza kulijenga taifa hili
#HapaKaziTu
 
Na balaa hilo hilo la kuvutiwa na sura, na kuvutiwa na uwingi wa watu ndilo mnataka kulirudia mwaka huu kwa Lowasa? no way., kuchagua Lowasa ni kurudisha aina ya uongozi wa Kikwete madarakani, na hatupo tayari kuendelea kuwa na aina ya uongozi wa Kikwete madarakani, ndio maana tunasema MAGUFULI 4 CHANGE.
Magufuli 4 change
Pamoja, tunaweza kulijenga taifa hili
#HapaKaziTu

Mkuu wanasema ndege wa aina moja huruka pamoja.Na sasa hivi Kikwete anaruka na Magufuli!
 
aliemteua nape ndo tunaambiwa wasaidizi wanamuangusha au yeye alishajiangusha?
 
Wadau kwa takwimu za wapiga kura alizozitoa mheshimiwa na ukimya wa Serikali juu ya alipo CDF; tutapona bao la mkono kweli?
 
Aliingia nchi ikiwa na mgao wa umeme..na anaondoka nchi ikiwa na mgao wa umeme
 
Ni raisi aliyeiletea Tanzania anguko kuu katika kila nyanja.
Rais wetu aliwahi kutoa onyo kuwa watu wasidanganyike na sura yake, wasidanganyike na tabasamu lake.

Nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu sana toka alipotoa maneno hayo ili nifahamu sura yake kamili na maana ya tabasamu lake ila nimefeli, sijaambulia kitu.

Ndio maana leo naomba msaada kwa waliomfahamu vizuri, wapendwa; Jakaya Mrisho Kikwete ni nani?

1. Je, ni mwanamapinduzi au labda ni mwanamageuzi?

2. Je,ni mtu asieogopa kujaribu au ni mtu asiyejua anachojaribu?

3. Je,ni dicteta aliyejificha kwenye ngozi ya democrasia au ni mtu mwenye misimamo isioyumba?

4. Je, ni mtu msafi aliyezungukwa na wezi au ni mafia anayetumia mkono wa giza kufanya mambo yake?

5. Je, Magufuli ni zawadi ya Kikwete kwa Tanzania au ni toleo la pili la Kikwete?

Au ni mchawi anayetaka kuizamisha Tanzania?

6.Uzuri wake mkubwa ni nini na kosa lake kubwa ni nini?

7.Je, ni rais aliyehujumiwa na watendaji wake au anatumia kisingizio cha kuhujumiwa kuficha udhaifu wake?

8.Je, anajua alipo Mwamunyange? na kama anajua mbona hatuambii?

9.Je, CCM ikishindwa uchaguzi atarudi Msoga kulima kweli?

Wadau nisaidieni kujua, Jakaya Mrisho Kikwete ni nani?
 
Back
Top Bottom