Jakaya Mrisho Kikwete ni nani?

Jakaya Mrisho Kikwete ni nani?

Kwanini unahisi malengo yake hayafanikiwi?

Je ni kuwa na mikakati mibovu au kukosa mikakati kabisa?

Je, hoja ya kuwa anahujumiwa na watendaji ni ukweli au kisingizio cha kuficha udhaifu wake.Kama unajua naomba majibu!
Utendaji zero kwa sababu hakuna adhabu kwa kutotekeleza. Halafu anapiga dili na familia yake watendaji nao wanapiga dili.
 
Kwanini unahisi malengo yake hayafanikiwi?

Je ni kuwa na mikakati mibovu au kukosa mikakati kabisa?

Je, hoja ya kuwa anahujumiwa na watendaji ni ukweli au kisingizio cha kuficha udhaifu wake.Kama unajua naomba majibu!

habar za kusema watendaji wake wa chini wanamuhujumu huo ni uzushi ulopindukia.Lengo ni kuficha udhaifu wake.
 
Mh. Dr. J. M. Kikwete ni Rais aliyejitahidi kuleta uhuru wa vyombo vya habari ambao mtu ana uhuru wa kukosoa atakavyo, ingawa uhuru huu umechangia uvunjaji wa haki za binadamu (Mwangosi). Pia ni pongezi kwake kwa sababu amejitahidi na miundo mbinu hasa barabara (ingawa barabara sio za viwango) na viwanja vya ndege, ingawa miundo mbinu hii huenda imechangia kuongezeka kwa deni la taifa.

Pia, Rais wetu amejitahidi kusaidia uhifadhi wa mali asili ktk kipindi chake, lakini kwa bahati mbaya ni kipindi ambacho wanyama wamejangiliwa kwa kiasi kikubwa sawa na miaka ya 1960s hadi 1989 (Miaka 29), na Rais wetu labda kwa upendo au staha amehifadhi majina ya majangili ingawa alidai anayo kibindoni (nahisi hii ilikuwa njia tu ya kudai anawajua majangili ili kutisha majangili wasuiendelee na biashara yao chafu).

Sifa kuubwa ambayo nampongeza nayo Mh. Rais ni mvumilivu na mtu mwenye kupuuza maneno ya wakosoaji wake. He is a real smart shock absorber kitu ambacho ni muhimu sana kwenye maisha ya mtu yeyote. Ni vizuri sana kutoruhusu maneno au matendo ya mtu kukuyumbisha au kuusumbua moyo wako. Heko JK.

Ni imani yangu kuwa JK alikuwa na mapenzi mema sana na hii nchi, ila kuna kundi la watu waliomzunguka ndilo limefanya sehemu ya muda wake wa uongozi kuonekana mbaya kiutendaji. Kuna watu wamekuwa washauri wabaya kwa Mh. Rais. Lakini pia ikumbukwe kuwa kwa ujumla si Tanzania tu bali mataifa mengi yanayoendelea na yaliyoendela yanapita kwenye wakati mgumu, na maisha ya wananchi ni magumu, mna ushahidi wa maandamano ktk nchi mbalimbali duniani.

HIVYO BASI, WATANZANIA TUSITEGEMEE MIUJIZA KWA RAIS ATAKAYECHAGULIWA KWA AWAMU YA TANO, IWE MAGUFULI AU LOWASSA, NOTHING NEW KIVILE KWA KWELI.
 
tulia wewe ccm iko poa sana kwa sasa hivi so we mpe kura magufuli afu utapata hayo maendeleo unayotaka. Magu yupo kitofauti sanaaa

yupo kitofauti?mbona jamaani hamujibu kuhusu shutuma ya nyumba za serekali? vp kimada liye hogwa nikweli? je vipi kivuko bomu? vipi kauli zake zenye ukakasi? na je vp maamuzi mabovu aliyo yafanya yakagharimu taifa, tusiwe wanafiki huyu mtu hatufai hata ukuu wa wilaya, nadhani anamambo ya ubabe usio na maana hata kwake nyumbani nahisi hapako salama sababu ya tabia hizi
 
Kikwete ndo rais bora kabisa tanzania kuwahi kupata.

Rais wetu aliwahi kutoa onyo kuwa watu wasidanganyike na sura yake, wasidanganyike na tabasamu lake.

Nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu sana toka alipotoa maneno hayo ili nifahamu sura yake kamili na maana ya tabasamu lake ila nimefeli, sijaambulia kitu.

Ndio maana leo naomba msaada kwa waliomfahamu vizuri, wapendwa; Jakaya Mrisho Kikwete ni nani?

1. Je, ni mwanamapinduzi au labda ni mwanamageuzi?

2. Je,ni mtu asieogopa kujaribu au ni mtu asiyejua anachojaribu?

3. Je,ni dicteta aliyejificha kwenye ngozi ya democrasia au ni mtu mwenye misimamo isioyumba?

4. Je, ni mtu msafi aliyezungukwa na wezi au ni mafia anayetumia mkono wa giza kufanya mambo yake?

5. Je, Magufuli ni zawadi ya Kikwete kwa Tanzania au ni toleo la pili la Kikwete?

Wadau nisaidieni kujua, Jakaya Mrisho Kikwete ni nani?
 
Ni tolea la pili, Kwan Kwa hali iliyopo ni vigumu ccm kutuletea maendeleo tunayoyahitaji. Ikiwa pindi ipo madarakani ilikuwa hawez kufanya maamuz magumu zidi ya miss use of public funds
ukimwambia lowasa kuwa rafiki yake Kikwete hawezi kufanya maamzi magumu, atakushangaa sana.
 
Hahahaaaaaa.....unang'ata na kupuliza duuuh....

By Paul Alex:
Nape ni mdomo tu wa wakubwa ndani ya CCM, na kiukweli sioni kama CCM ina mkubwa mwingine zaidi ya Kikwete!
Kuna namna wana CCM wanapaswa wamuone Kikwete.Ni mtu anayejaribu mambo bila kufanya hesabu, bila kujali tuseme!
He has a lot of power and he is simply misusing it! Swali ni kuwa mtu mwenye nguvu ya amiri jeshi mkuu alieonyesha tayari dalili tulizoona sijui ataishia wapi kuhakikisha anaibuka mshindi katika hii vita ya kunyang'anyana fito?
Nape hawezi kumuita Kingunge nguo ya ndani iliyochafuka.Hata kama kweli angekuwa hivyo, maneno ya busara kidogo yangepooza makali ya kuondoka kwa kingunge!
Seriously mimi ni mwanachama wa CHADEMA ila napenda sana kupima effect ya maamuzi na mikakati! Nikiangali CCM sioni mikakati inayofanya kazi leo wala itakayofanya kazi miaka kumi ijayo.Naona Kama vile kuna mtu anarusha jiwe kwenye giza alafu anafunga macho akiomba lilenge ndege!
Mdomo wa Nape umeshaigharimu sana CCM na utaendelea kuigharimu. Mtu mwenye mkakati wa kutumia mdomo wa Nape anakosea. Atafanikiwa kutoa ya moyoni kwake kwa kupitia Nape lakini hatafanikisha lolote zaidi ya hilo.
Baadae Nirudi kwa Nape, Nape ni kijana na makubaliano ya kisiasa sio ndoa iliyofungwa mbinguni.Ni makubaliano ya muda mfupi yanayoweza kuvunjika, siasa ni kazi kama kazi nyingine. Usikubali tu mdomo wako kutumika kuongea vitu vichafu.
Kwanza vinakuchafua wewe na ukitaka kujua hili angalia tu mfano wa kujisaidia.Mtu anapoharisha, tumbo linajisikia vizuri sana. Lakini sehemu uharo unapotokea panachafuka. Na wewe usikubali kuwa hiyo sehemu!
Pili ni dhambi tu kwa Mungu bila kujali wewe ni wadini gani!
Tatu unajitengenezea maadui wengi ambao wewe binafsi huna ugomvi nao.
Nne, unajitengenezea Legacy ya kuwa mwanasiasa mwenye mdomo mchafu kuliko wote.Hakuna mtanzania atataka kuongozwa na mtu anayejisaidia kwa kutumia mdomo.
Politics is a profession, so start being professional. Natamaani siku nikiingia kwenye siasa nikutane na CCM yenye wanasiasa mahiri wenye hoja ili tuwashe moto.
Sio nikutane na walevi wenye matusi tu mdomoni!

Nimeipenda analysis yako. Yaani mpaka inashangaza. Walianza kupiga makelele akina Mgeja zamani sana kwamba jamani chama mnakiendesha ndivyo sivyo. Wakaambiwa watashughulikiwa. Hakuna busara wala maelewano. Chama chenye mwelekeo huungana na kumuunga mkono mgombea wao. Leo hii wagombea 30 hakuna hata mmoja aliyesimama na Magufuli jukwaani kuonyesha kuwa wako pamoja. Inatia aibu sana.
Mwanzoni Lowassa alipoondoka mi sikuwa na wasiwasi na nilidhani kuwa CCM wana strategy of containment kali sana kwani ni mtu wanayemjua vizuri na kimsingi ndiyo wamemlea na kumuacha akijitandaza na kujiimarisha kwa makumi ya miaka. Kumbe hawakuwa na strategy yo yote na wanajaribu hapa na pale bila mafanikio. Flicking unbelievable! Na mtu ungedhani pengine wamejifunza kitu. Halafu katibu wa propaganda anakuja na maneno kama haya. They haven't learned anything.
Ngoja tuone gemu litakavyoisha lakini nadhani hawatakubali kuachia madaraka hivi hivi. Wapinzani inabidi mlitambue hili na mjiandae kisaikologia

Nashukuru kama umekuwa na mtazamo huo, something very wrong is going on in CCM!
Na kawaida mtu ukikosa mkakati wa kufanikisha jambo huwa anaishia kutumia nguvu.
Kikwete hataki Lowassa aongoze nchi hii,hili hata ukimuuliza mtoto mdogo atakwambia.Na alioyafanya tayari kwa Lowassa na anayoyafanya kwa kupitia Nape yanakwambia wazi wazi kuwa yuko on war gear.
Tatizo langu ni kuwa rais ni mtu mwenye nguvu sana na hili mtu yoyote asijidanganye!
Watu waliobaki nae wanajua fika mtaani hawawezi kushinda na wameweka matumaini yao yote kwenye nguvu za rais.
Siko sana karibu na Lowassa lakini naamini kuna watu wa karibu na yeye wanapita huku.
Kuamini kwamba Kikwete atakaa asimame jukwaani kusema Rais ni Lowassa ni ndoto za mchana!
Kuwaweka wananchi mbele wakabiliane na nguvu ya rais, japo ndilo jambo linalofanywa sehemu nyingi duniani, ni kuwaumiza na japo haki haiombwi lakini ni busara tu kuwapunguzia wananchi mzigo huu.
Najua kuna watu wazima huko juu, so please, think of a strategy ili kama inafaa wananchi kikombe hiki tukiepuke, ila kama haifai, basi, mapenzi ya Mungu yatimizwe!
 
Kiongozi, Vasco da gama alikuwa explorer na ndie aliefungua njia ya kuanza kwa uchumi wa kinyonyaji na umiliki wa maeneo makubwa duniani.Aliisaidia Ureno kuanzisha Utawala wa kikoloni uliodumu kwa muda mrefu.

Je, Kikwete amegundua nini?
Je, ameisaidia Tanzania nini ambacho kitakumbukwa?

Amegundua Escrow,EPA,RICHMOND NA BRN
 
Kikwete ndo rais bora kabisa tanzania kuwahi kupata.

kabisa Abunuas binafs huwa nasema kila siku.Nalithibitisha hili kwa mifano kadhaa
-Rekod yake ya safar za nje ya nchi
-Kuwasamehe watu waliokwapua pesa BoT zile za EPA
-Chini ya utawala wake ndo twiga tumeskia wamesafirishwa kwa ndege
-Ndio tumeskia watu wamepiga mishindo mikubwa ya pesa
-Ndio tumeshuhudia kiwango cha elim kuongezeka
-Ndo tumeskia baadhi ya mawaziri wake wakiuchanganua muungano wa Zimbabwe na Tanganyika
-Ndo tumeshuhudia vijana wakiwakosea heshima wazee(Warioba)
-Ndo tumeshuhudia waandish wakipoteza maisha kwa kushambuliwa na polisi (rejea)Mwangosi
-Ndo tumesikia vuguvugu la kidini
 
Last edited by a moderator:
Mh. Dr. J. M. Kikwete ni Rais aliyejitahidi kuleta uhuru wa vyombo vya habari ambao mtu ana uhuru wa kukosoa atakavyo, ingawa uhuru huu umechangia uvunjaji wa haki za binadamu (Mwangosi). Pia ni pongezi kwake kwa sababu amejitahidi na miundo mbinu hasa barabara (ingawa barabara sio za viwango) na viwanja vya ndege, ingawa miundo mbinu hii huenda imechangia kuongezeka kwa deni la taifa.

Pia, Rais wetu amejitahidi kusaidia uhifadhi wa mali asili ktk kipindi chake, lakini kwa bahati mbaya ni kipindi ambacho wanyama wamejangiliwa kwa kiasi kikubwa sawa na miaka ya 1960s hadi 1989 (Miaka 29), na Rais wetu labda kwa upendo au staha amehifadhi majina ya majangili ingawa alidai anayo kibindoni (nahisi hii ilikuwa njia tu ya kudai anawajua majangili ili kutisha majangili wasuiendelee na biashara yao chafu).

Sifa kuubwa ambayo nampongeza nayo Mh. Rais ni mvumilivu na mtu mwenye kupuuza maneno ya wakosoaji wake. He is a real smart shock absorber kitu ambacho ni muhimu sana kwenye maisha ya mtu yeyote. Ni vizuri sana kutoruhusu maneno au matendo ya mtu kukuyumbisha au kuusumbua moyo wako. Heko JK.

Ni imani yangu kuwa JK alikuwa na mapenzi mema sana na hii nchi, ila kuna kundi la watu waliomzunguka ndilo limefanya sehemu ya muda wake wa uongozi kuonekana mbaya kiutendaji. Kuna watu wamekuwa washauri wabaya kwa Mh. Rais. Lakini pia ikumbukwe kuwa kwa ujumla si Tanzania tu bali mataifa mengi yanayoendelea na yaliyoendela yanapita kwenye wakati mgumu, na maisha ya wananchi ni magumu, mna ushahidi wa maandamano ktk nchi mbalimbali duniani.

HIVYO BASI, WATANZANIA TUSITEGEMEE MIUJIZA KWA RAIS ATAKAYECHAGULIWA KWA AWAMU YA TANO, IWE MAGUFULI AU LOWASSA, NOTHING NEW KIVILE KWA KWELI.

hapa ndo mnaponichosha watanzania wenzangu,yaani sababu hii ni ya kipuuz sana na huwa sioni kama inamashiko.Kwa miaka 10 wewe unaendelea kuteua washaur wabovu tu halafu ukae kando na ubovu wao?katiba ya JMT inampa mamlaka makubwa rais ya uteuz,haya hebu niambie Gambo ameteuliwa na nani kuwa DC???na ni nani alimtoa u-DC???ondoa sababu za kitoto bhana.,Yaani sifa nzuri ziende kwa jk sifa mbaya ziende kwa washaur wake,,,,,how????unatumia vigezo gani hapo????
 
Back
Top Bottom