Jakaya Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon UN?

Jakaya Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon UN?

quinine umenichekesha sana. kwa hiyo sisi tupo top 10 ya nchi zenye watu wenye IQ ndogo duniani? du!


Tanzania ni kati ya nchi 10 zenye IQ ndogo kabisa duniani.

Wenye dunia yao sio wajinga kiasi hicho huwa wanaangalia IQ ya mtu na IQ ya nchi yenyewe.
 
pamoja na sifa nyingine nyingi cheo hicho kinahitaji mtu makini na mwenye busara !
 
Kutokana na sifa nzuri ya JK kimataifa zipo tetesi anaweza kumrithi katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana Ban Ki-Mooon muda wake ukiisha. JK ni kiongozi pekee kutoka nchi za dunia ya tatu mwenye mahusiano mazuri, ni rafiki mzuri wa china, marekani, ujeruman uingereza na ufaransa ambao ni watu wenye ushawishi mkubwa katika baraza la umoja wa kimataifa.

Wakati wa utawala wake viongozi wakuu wa Marekani walitumia muda wa kutosha kupumzika Tanzania ikiwemo Rais George Bush kukaa zaidi ya siku tatu Tanzania jambo ambalo halijawahi kutokea. Pia wakati wa mkutano wa kibiashara wa dunia marais watatu wa marekani walikutana Tanzania kwa mpigo jambo ambalo si la kawaida.

Katika mkutano wa china na afrika JK alionekana akitaniana na rais wa China kana kwamba anaongea na swahiba wake wa karibu huku akiwatambulisha watu mbalimbali kwa mkuu huyo wa uchina.

Kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa mambo ya nje balozi Augustine Mahiga ambaye ni rafiki wa karibu wa Ban ni dhahiri Mahiga atalichomeka jina la JK kwa Ban Ki-Moon watakapokutana katika masuala ya kimataifa.

Yakheeee!!!!! unaburudisha nafasi yako tu; "raha jipe mwenyewe".
 
china na marekani kuizonga Tanzania Ni sababu ya Maliasili uliyoikalia hawana urafiki na mtu yoyote,rafiki Yao Ni gesi,tembo,twiga,uranium,coal,iron ore,gold,diamond,tanzanite nk
America does not have permanent friend or permanent enemy sera Yao hapendwi mtu Bali utajiri
bush,Obama na mchina wana urafiki na Mali ya tanzania Tu na sio vinginevyo.
hata putin(Russia)amewekeza kwenye uranium.

Wewe umesema kweli. Ni mjinga tu anayefikiri Mataifa yalliyendelea yanaipenda Tanzania. Walimuweza jk tu. sasa wanatafjta mbinu kumpata magufuli.
 
Kutokana na sifa nzuri ya JK kimataifa zipo tetesi anaweza kumrithi katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana Ban Ki-Mooon muda wake ukiisha. JK ni kiongozi pekee kutoka nchi za dunia ya tatu mwenye mahusiano mazuri, ni rafiki mzuri wa china, marekani, ujeruman uingereza na ufaransa ambao ni watu wenye ushawishi mkubwa katika baraza la umoja wa kimataifa.

Wakati wa utawala wake viongozi wakuu wa Marekani walitumia muda wa kutosha kupumzika Tanzania ikiwemo Rais George Bush kukaa zaidi ya siku tatu Tanzania jambo ambalo halijawahi kutokea. Pia wakati wa mkutano wa kibiashara wa dunia marais watatu wa marekani walikutana Tanzania kwa mpigo jambo ambalo si la kawaida.

Katika mkutano wa china na afrika JK alionekana akitaniana na rais wa China kana kwamba anaongea na swahiba wake wa karibu huku akiwatambulisha watu mbalimbali kwa mkuu huyo wa uchina.

Kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa mambo ya nje balozi Augustine Mahiga ambaye ni rafiki wa karibu wa Ban ni dhahiri Mahiga atalichomeka jina la JK kwa Ban Ki-Moon watakapokutana katika masuala ya kimataifa.
Jamani, JF ilikuwa home ya great thinkers. Sasa naona small thinkers wametuzidi mizani. Kabla ya kuleta uzi huku afadhali kwanza ufanye utafiti kidogo na si kusukumwa na mhemko wa ushabiki. Kikwete hawezi katu kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika karne hii.
 
Mh hizo ndoto kashindwa mgogoro wa Zanzibar na kila kitu kipo wazi kua ccm wameshindwa hakuutatua ataweza kutatua migogoro mikubwa
 
Safari hii ni zamu ya bara la ulaya

Great Thinker, hakuna kits Kama hicho. Katika historian ya UN alianza Norwegian akaja Swedish, Burma, kisha Misri/Afrika, Ghana/Afrikana sasa Bak. Google list of UN secretary generals mkuu
 
Achana Nalo Hilo Halijielewi.Ban Alimrithi Anan Toka Afrika,kwa Maana Nyingine Hiki Cheo Kurudi Afrika Ni Labda 2045,sijui Huyo Kichwa Nazi Wa Msoga Atakuwa Na Umri Gani!!

Naona Mmemsahau Butros Butros Ghali huyo alikuwa anatokea Africa pia Egypt na haikupita hiyo Miaka 45 akaja Koffi Anan
 
Mkuu Elli hupaswi kupitwa na Uzi huu uliosheheni sifa za kijinga
 
Last edited by a moderator:
in ilipoanzishwa zilikua nchi 5,china, urussi,marekani,ufaransa na uingiteza,hao ndio wakubwa wa umoja huo, na ndio wenye uwamuzi wa kuamua nini kifanyike kwenye dunia hii,kiuchumi, vita, nk. na ndio wanaokaa kikao cha kuteua kiongozi wanaeona anafaa kutoka kwenye maeneo tofauti duniani.na malanyingi hawazunguki kwa bara ila wanachukua ukanda fulani mfano:,kipindi kilichopita kilikua ni zamu ya uraya ya mashariki na kutokana na migogoro ya ukreini wameona wasiteue mtu kutoka huko na wameamua kumuacha ban kngmoon aendelee kwa kipindi kingine na ikawa hivyo.kwa mpango huu wakubwa Hawa kumbe wanauwezo wa kuamua yeyote awe mwenyekiti. kwa kipindi hiki kinachokuja inatakiwa atoke ukanda wa ratini amerika kamavile (Mexico) . kwa sheria zao hua wanateua wanaemuona anafaa na hasa wanaeona anafuata matakwa yao na maslahi yao.
 
acheni kudhalilisha ofisi ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa!
 
Hii thread inanipa mashaka makubwa

Hasa chanzo chake.
Mleta uzi inaonekana analipwa kwa post za mtindo huu.

Swali. Mlipaji ni nani??
 
Bora apate icho cheo akaishi huko huko ulaya alipokua anaenda kila kukicha nadhani safari atazokua amebakisha ni kwenda mwezini tu
 
Back
Top Bottom