Jakaya Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon UN?

Jakaya Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon UN?

Yote yanawezekana na kwa kuwa ni jambo jema sisi tunaomba MUNGU alipe uzito wa aina yake

Nyambaf!
Hivi nyie Mafisi wa Lumumba hamweshi vituko?
Juzi tu mmegushi kuwa JPM kachaguliwa kuwa Africa person of year kumbe ni UONGO! Leo mnakuja na porojo ya JK kuwa UN Secretary General. Hakika hizo ni ndoto za Alinacha!
Yaani dunia nzima UN wakose watu waje mpaka Tanzania kutafuta candidate na mtu mwenyewe ni JK...!!!!!!
 
Kutokana na sifa nzuri ya JK kimataifa zipo tetesi anaweza kumrithi katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana Ban Ki-Mooon muda wake ukiisha. JK ni kiongozi pekee kutoka nchi za dunia ya tatu mwenye mahusiano mazuri, ni rafiki mzuri wa china, marekani, ujeruman uingereza na ufaransa ambao ni watu wenye ushawishi mkubwa katika baraza la umoja wa kimataifa.

Wakati wa utawala wake viongozi wakuu wa Marekani walitumia muda wa kutosha kupumzika Tanzania ikiwemo Rais George Bush kukaa zaidi ya siku tatu Tanzania jambo ambalo halijawahi kutokea. Pia wakati wa mkutano wa kibiashara wa dunia marais watatu wa marekani walikutana Tanzania kwa mpigo jambo ambalo si la kawaida.

Katika mkutano wa china na afrika JK alionekana akitaniana na rais wa China kana kwamba anaongea na swahiba wake wa karibu huku akiwatambulisha watu mbalimbali kwa mkuu huyo wa uchina.

Kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa mambo ya nje balozi Augustine Mahiga ambaye ni rafiki wa karibu wa Ban ni dhahiri Mahiga atalichomeka jina la JK kwa Ban Ki-Moon watakapokutana katika masuala ya kimataifa.
Nahisi 1.4 imezudi
 
Uzi mwingine wa JK, naona JK akipata nafasi hiyo atakwenda mwezini kama space tourist kwa jinsi anavyopenda safari. Wakimuuliza kwa nini unapenda sana safari za anga za mbali atajibu naenda kutafuta misaada ya dunia yetu

Ume gonga ndipo .....
 
Kwa udalali alioufanya wa kuuza Rasilimali zetu anaweza kuzawadiwa hiyo nafasi.Jambo pekee linaloweza kuwa kikwazo kwake katika kupata nafasi hiyo ni tabia yake ya kuishi angani kama popo.Labda UN wamjengee ofisi mwezini,lakini kama ofisi zitabaki kuwa ardhini hawezi kukubali huo uteuzi.

Mbavu zangu jamani ....
 
Nyie mnaishi wapi.. Saksesa wa ban tayari yupo anatoka south america
 
Aise kila siku huwa nawambia tuache kupost habari ambazo hatuna uhakika nazo mrithi wa katibu mkuu UN atatokea ureno sass wewe habari za JK unazitoa wapi? Muacheni mzee wa watu apumzike.
 
Back
Top Bottom