Jaji Werema akipona katika hili la IPTL natembea uchi

Jaji Werema akipona katika hili la IPTL natembea uchi

Itakuwa na nguvu kwa kuwa baada ya Werema kulazimika kuandika barua ya kujiuzulu kwa Rais na kujiuzulu huko kukubalika, tafsiri yake ni kuwa mkuu tpaul amenusurika kutembea uchi toka Pugu hadi Kivukoni, iwapo tu Jaji Werema angegoma kabisa kujiuzulu na bosi wake angeshindwa kumtimua kazi!

asante , hata hivyo nililenga ile post niliyoi quote , sikulenga thread hii .
 
Naapa kwamba ikiwa Jaji Werema atanusurika kuangukiwa na rungu kufuatia skandali ya UFISADI wa ESCROW, nitatembea uchi barabarani kutoka nyumbani kwangu Pugu hadi Kivukoni.

Nimemkamia sana Werema kuliko wahusika wengine kwa sababu ya kiburi chake na kwa kuwa ameisababishia serikali hasara kubwa zaidi ukilinganisha na mafisadi wenzake waliohusika katika skandali nzima.

Sababu ya pili ya kumkamia huyu MWIZI inatokana na jinsi alivyokuwa akimkomalia Mh Kafulila na kumuita TUMBILI hadi mishipa inamtoka na macho kuwa mekundu huku akijua kwamba ameiibia serikali mabilioni ya shilingi.

Yaani wananchi wanakufa kama nzige mahospitalini kwa sababu serikali haina fedha za kununulia dawa wakati tumbili huyu ameipotezea serikali mabilioni ya shilingi!

Ndugu watanzania, endapo bunge halitamuwajibisha Werema na baadaye Profesa Kikwete kumfuta kazi na serikali kumfunga jela, sote tuandamane uchi kwenda Dodoma tukalichome moto jengo la bunge. Hakuna haja ya kuwepo kwake ikiwa haliwezi kumuwajibisha huyu MWIZI.

:israel:
Mkuu umepona kumwaga radhi...ila ungeahidi Tibaijuka walah ungetembea!!
 
Hongera tpaul kwa mafanikio makubwa uloyapata nami nadiriki kusema kuwa hatuna budi Mimi na wewe tpaul tuchukue maamuzi hayohsyo endapo JK asipowasurubisha wahusika J3
 
Hongera tpaul kwa mafanikio makubwa uloyapata nami nadiriki kusema kuwa hatuna budi Mimi na wewe tpaul tuchukue maamuzi hayohsyo endapo JK asipowasurubisha wahusika J3

Anza na home kwako......!!!!
 
Hongera tpaul kwa mafanikio makubwa uloyapata nami nadiriki kusema kuwa hatuna budi Mimi na wewe tpaul tuchukue maamuzi hayohsyo endapo JK asipowasurubisha wahusika J3

Pamoja sana mkuu. Kwa jinsi hali ilivyo, kuna kila dalili kwamba hata PM huenda akaenda na maji...hali ni mnaya sana kule Lumumba. Ukimuuliza MwanaLumumba yeyote kati ya hawa Mingoi, MwanaDiwani, MSALANI, East African Eagle, Ritz, mjepo, Mamndenyi, laki si pesa, Agogwe, lusungo, Queen P, gsu, Simiyu Yetu, thatha, Nape Nnauye atakuambia kwamba hali ya Lumumba kwa sasa hivi ni tete sana. Baada ya TUMBILI mmoja kuachia tawi na kuuaga msitu, tumbili waliosalia hawalali usingizi.
 
Last edited by a moderator:
tpaul hajawahi kumung'unya maneno na anajiamini sana , namwamini .

umeona eeh? tunawasubiri wale Misukule wa Lumumba waliokuwa wakitamba kwamba hakuna tumbili atakayeachia tawi waje wabatilishe kauli zao.
 
IPTL wanafanya kazi ya kuzalisha umeme na kuwauzia TANESCO ni lazima walipwe.

Mpaka sasa ripoti ya CAG na PCCB sijaziona, kwanini nianze kuonyooshea watu vidole?

Hiyo ripoti sasa umeiona au bado?
 
kwa sababu gani?

Hapo mkuu mada inasema Werema akipona. .... bahati nzuri hajapona! Angepona kweli ingewezekana kutembea uchi? Imagine kweli ikawa hivyo jamii itakuchukuliaje? That was my concern. Sina maana zaidi ya hiyo. Kama nimekukwaza sorry!
 
na mimi Muhongo asipojiuzulu ntatembea uchi kuanzia Arusha mpaka dar ikulu kwa JK bila kuogopa chochote huyu Muhongo ana kiburi kama Werema
 
Usiombe uwe shabiki LA yanga tena mwanaume halafu utoe ahadi kama hii kwenye game ya mtani jembe.........wanaume watakusubiria mlangoni kwako wakiwa na ky zao
 
Back
Top Bottom