Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

WILIIAM jOHN MALECHELA.....MSANII UNAYEJIITA LE MUTUZ....

NAOMBA NIKUAMBIE NA TENA NIKUHAKIKISHIE KUWA HAUNA MORAL AUTHORITY YA KUFANYA MAJADILIANO NA MZEE WARIOBA SEMBUSE HILI LA KUJIBIZANA NA MZEE WARIOBA.......

WEWE KAZANA NA BIASHARA ZAKO NA TENA NAKUSHAURI UACHANE NA SIASA...WATU WANAOIPENDA TANZANIA WANAWEZA KUKUANGUSHIA KIBANO SAA YOYOTE...

NI VIZURI UKAJIFUNZA TABIA NJEMA..MZEE WARIOBA ANAWEZA PIA KUWA BABA YAKO...

- Wewe hamna baba hapa, tunajadili Taifa wachana na mambo ya baba, Sheria ipo wazi sana unataka niirudie tena?

Le Mutuz
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz

Kweli ww ndio "Le matuzi"

Kwani nani asiejua kuwa anachosema bosi wako Bulembo ni wazi huwezi pingana nae? Hata kama akij..ba wewe si unapiga makofi tu?! Kubwa jinga wewe kabisa! Hivi wewe kaka hukui?
 
Kweli ww ndio "Le matuzi"

Kwani nani asiejua kuwa anachosema bosi wako Bulembo ni wazi huwezi pingana nae? Hata kama akij..ba wewe si unapiga makofi tu?! Kubwa jinga wewe kabisa! Hivi wewe kaka hukui?

- ha! ha! okeeeee!! eti kukua kuna anything to do na Katiba mpya? really?

Le Mutuz
 
- ha! ha! la msingi ni marekebisho ya katiba mpya na si Warioba wala Chadema wenye nguvu nayo ila CCM, sheria ipo wazi sana!! ila tu umenivunja mbavu na matusi yako ya kizamani sana!! ha! ha1

LE Mutuz
Hapa hatujadili CCM wala CHADEMA, tunajadili muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba!
 
Hapa hatujadili CCM wala CHADEMA, tunajadili muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba!

- Tunajadili namana ya kutengeneza katiba mpya kisheria, CCM ndio tuna hiyo haki ni ukweli mbaya na unaouma sana lakini ndio ukweli wenyewe mtuwanguz.

Le Mutuz
 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema baadhi ya wanasiasa wameacha kujadili rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume yake badala yake wamejikita katika kuijadili Tume yake na Wajumbe.

Kauli ya Jaji Warioba imekuja kufuatia tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abdallah Bulembo mkoani Tanga zilizonukuliwa na ITV na baadhi ya magazeti leo.

Katika taarifa hizo, Bulembo anaelezwa kusema kuwa Tume ya Warioba imekuwa ikiingilia uhuru wa wananchi kutoa maoni katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya badala ya kukusanya maoni ya wananchi hao na kuongeza ikiwa Tume au Jaji Warioba anataka kufanya kazi hiyo, basi ajiuzulu kwanza katika Tume.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Warioba, ambaye ameshawahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri Mkuu, amesema kauli hizo ni upotoshaji na kuwa Tume yake ina jukumu la msingi la kutoa elimu kwa umma.

“Moja ya kazi za kisheria za Tume ni kutoa elimu kwa umma, na ni kazi ya wakati wote,” anaelezwa kusema Jaji Warioba wakati akijibu swali la mwandishi mmoja kutoka Star TV aliyeongozana na baadhi ya waandishi wengine kutoka ITV, Channel Ten na Clouds FM.

Kwa mujibu wa Warioba, katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, wananchi ambao walikuwa ni wajumbe wa Mabaraza hayo walikuwa na fursa ya kuuliza maswali na Wajumbe wa Tume walitoa elimu kuhusu hoja na maswali yaliyoulizwa kwa mujibu wa sheria.

“Sasa anaona (Bw. Bulembo) kuwa kutoa elimu ni dhambi,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Bulembo kutoa kauli kama hizo.

“Nilimsikia Mbeya, Moshi na sasa Tanga akitoa matamshi hayo… kwa kawaida huwa sizungumzii mambo haya, huwa tunayaacha yapite,” alisema na kufafanua kuwa kauli kama hizo zimekuwa zikiwafanya wajumbe wa Tume kufanya kazi katika mazingira magumu.

“Nilisema katika mkutano wangu na waandishi wa habari mwishoni mwa mwezi uliopita kuwa Tume yake imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kauli za wanasiasa, zikiwemo zake (Bulembo),” alisema na kuongeza kuwa, pamoja na kauli hizo, Tume yake inafarijika na kauli za kutia moyo wanazozipata kutoka kwa wananchi wa kawaida.

“Matamshi mengine yalilenga Tume na wakati mwingine yalinilenga mimi binafsi au wajumbe wa Tume badala ya kuzungumzia rasimu,” anaelezwa kusema.

Jaji Warioba alisema Tume yake siku zote imekubali kukosolewa kwa kuamini kuwa kukosolewa ni jambo la kawaida lakini akaongeza kuwa ni vema wananchi na wanasiasa wakajadili rasimu ya katiba iliyotolewa badala ya watu au Tume.

“Nadhani wangezungumzia rasimu wangetusaidia sana, badala ya kuzungumzia Tume na watu,” amesema Jaji Warioba.

Kuhusu kujiuzulu, Jaji Warioba anaelezwa kusema kuwa haamini kuwa kauli zinazotolewa na Bulembo ni kauli za CCM kwa kuwa CCM haijawahi kuitaka Tume ijiuzulu.

“Sina hakika kama anazungumza kwa niaba ya CCM kwani CCM haijasema tujiuzulu,” anadaiwa kusema.

Imeandikwa na mwandishi wa JF

Tatizo wa tz kila kitu mlaleta siasa.mnatualibia nchi
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz
Wewe ---- kweli. Baba yako mwenyewe alikuwa anataka Serikali tatu halafu unambeza Warioba? Kweli katapila limezaa crusher
 
Katiba sio ya kuamuliwa na sisiem wala kikundi chochote kile, inatakiwa iamuliwe na wananchi at large Wile unachemka (imaomesha kukaa kwako marekani unaona ni dili sana kilaukihojiwa unataja marekani Duh!! Wewe ni reduced mind kinoma.
- tunaishi kwa Sheria sio kanuni, Sheria ipo wazi Warioba hana mamalaka ya kuwaamulia wananchi Katiba, ila anayo mamalaka ya kukusanya maoni yao na kuyaandika chini, Warioba hana mamlaka yoyote kikattiba ya kuwaambia eti Viongozi wa Saisa wakae chini kujadili tena Rasimu, Rasimu imeshaenda Bungeni imepitishwa na Wabunge wa Chadema na CCM, sasa inasubiri saini ya Rais iwe Muswaada na kujadiliwa na Wabunge,

- Labda nikukumbushe historia kidogo, kule USA ni Republicans ndio walioamua kupunguza mafao ya Marais wao kwa sababu ya wingi wao bungeni, na ni wao ndio walioamua kupunguza malipo ya welfare ya wananchi wao bila kujali uchache wa Democrats bungeni kwa sababu Sheria inasema ni majority ndio wenye uamuzi wa mwisho wa marekebisho ya sheria, CCM ndio wenye mamlaka ya mwisho kisheria ya jamhuri kuamua katiba mpya iweje sio Warioba na Chadema.

Le Mutuz
 
- Tunajadili namana ya kutengeneza katiba mpya kisheria, CCM ndio tuna hiyo haki ni ukweli mbaya na unaouma sana lakini ndio ukweli wenyewe mtuwanguz.

Le Mutuz

ccm kama nani? Wananch wengine wasio na vyama hawana hiyo haki kubwa jinga wewe! Unaja mb a jamba tu ! Hapa jukwani kila post yako imejaa ushabiki stop!
 
Tunataka serikali tatu! Tanganyika yenye mamlaka and zanzibari yenye mamlaka kamili nyie manyinyimu mtaka nini?
 
kuna sentensi moja niliikuta humu JF ndo ilinishawishi kusoma na kuanza kuingia humu JF. hiyo sentence ilikuwa inasema " Kuitetea CCM hadharani unatakiwa uwe na Akili za Maiti" Leo nimeamini LEMUTUZ NI WALKING COURPSE
 
1. Kwenye Siasa kama kwenye Sheria na Uchumi kuna kitu kinaitwa the bottom line, ambayo katika ishu nzima ya Tume ya Warioba na Tume zingine zote zilizopita kazi yao ilikuwa ni kukusanya tu maoni ya wananchi na kutoa mapendekezo, ambao sio lazima yakubaliwe na waliounda kamati, ndio maana kuna Tume ilisema Wananchi wa Tanzania 80% hawataki vyama vingi vya siasa, lakini Serikali ya CCM ikaapuuza na kuruhusu Wapinzani. Narudia tena kazi ya Tume ya Warioba ni kukusanya tu maoni ya wananchi na kuyaweka pamoja na mapendekezo, lakini sio kutuamulia CCM kuhusu nini cha kufanya na katiba mpya.

2. Great kwamba umetaja vyeo vingi vilivyowahi kushikwa na Warioba katika Serikali yetu, nashangaa akiwa kwenye nafasi zote hizo ni nini kilimshinda kufanya haya ya Serikali tatu anayoyalilia sana sasa hivi wakati akiwa kwenye Tume ambayo haina nguvu yoyote kisheria ya kubadili Sheria? I mean ni kichekesho kikubwa sana, MWalimu alipokuwepo sikuwahi kusikia Warioba anataka Serikali tatu, sasa leo ameibukia wapi na hizi habari za Serikali tatu? Tunayemjua ni Kasaka Njelu peke yake ndiye aliyesimama kidete na kutaka Serikali tatu lakini sio Warioba, ni bora anyamaze na asubiri muda wake kwenye kamati ukiisha au ajiuzulu sasa na kutoa maoni yake kama sisi wananchi wengine.Le Mutuz
William, Ukikaa kimya inaweza kukusadia maana kila ukiandika unajipaka samadi sijui ni ya wanayama au ya binadamu.
Nenda kasome hadidu rejea za tume ya warioba alizopewa na serikali ya JK halafu urudi hapa.
Pili, lazima uelewe tume ya Warioba ipo kisheria,ilianzishwa kwa mswada uliosainiwa na kuwa sheria.
Kusema tume haina nguvu za kisheria ni ishara nzuri hujui hata tume imeundwaje.

Pili, pamoja na ukweli kuwa uandikaji wa katiba ya sasa haukufuata kanuni za kuandika katiba, William lazima aelewe kuwa tume si kikundi cha makarani cha kukusanya maoni. Hata kwa mtindo anaofikiria haelewi kuwa waliotoa maoni ni wananchi na tume haina sababu za kusikiliza maoni ya CCM bali wananchi.
Kusema kazi ya tume ni kukusanya maoni ni umbu mbu wa hali ya juu sana.

Tume ya Warioba haipo kubadili katiba, ipo kutengeneza mazingira ya kuandika katiba kama ilivyotakiwa na sheria ya bunge lenye CCM wengi na kusainiwa na mwenyekiti wa CCM ambaye ni rais mbona ni vitu rahisi sana kuelewa.

Tume ya kukusanya maoni ya vyama vingi ilikuwa ya rais hikuwa na nguvu za kisheria.
Hata ilipotoa maoni bado busara zilitumika,halikuwa suala la wengi wanasema nini.

Kuhusu tuhuma kwa Warioba, Njelu Kasaka alikuwa kiongozi wa G55 baba yako mzee J.S alikuwa kiongozi wa serikali hakuweza kuonekana ndani ya G55 ingawa aliunga mkono hoja ya G55.

J.S waziri mkuu aliruhusu hoja ya watu 55 iingie bungeni ili kubdaili katiba bila kuzingatia maoni ya wananchi. Nyerere akasema kama hiyo haikuwa sera ya CCM na wale wanaoitaka waondoke ndani ya chama wakaitetee wakiwa nje.
Nyerere akasema ' Wahuni' wamemshauri rais vibaya Malecela akapigwa chini na kuanguka kisiasa kukaanzia hapo hadi sasa ambapo watoto ndio hawa tunawasoma.

Baba yako mzee J.S.Malecela alikuwa kiongozi wa G55 kwa kujificha nyuma ya Njelu Kasaka.
Hakutaka seriakli 3 kwa faida ya nchi alitaka awe rais wa Tanganyika tu.

Hivyo mwasisi wa serikali 3 katika miaka ya karibuni ni baba yako. Warioba ana rekodi zake lakini ya baba yako ndiyo inakutesa wewe na CCM.

Laana ya Nyerere ndio imepelekea baba kutokuwa rais wa nchi hii hata siku moja.
Hilo linakukera unaamua kumaliza hasira kwa Warioba. Kwa mwendo ulivyo sidhani kama familia ya Malecela itatoa kiongozi tena maana kama mwanae ni wewe ipo kazi ya miaka mingi.

Ninachoogopa ni kumuona William akitoa maamuzi yanayogusa maisha yetu sehemu X.
Kidogo angekuwa mbunge wa EAC, na bado hatujapona anaweza kuwa mkuu wa Wilaya, mkoa au balozi.
Eeeh Mola tusaidie kutuepusha na mabalaa

 
William, Ukikaa kimya inaweza kukusadia maana kila ukiandika unajipaka samadi sijui ni ya wanayama au ya binadamu.
Nenda kasome hadidu rejea za tume ya warioba alizopewa na serikali ya JK halafu urudi hapa.
Pili, lazima uelewe kuwa tume ya Warioba ipo kisheria ndio maana ilianzishwa kwa mswada uliosainiwa na kuwa sheria.Kusema tume haina nguvu za kisheria ni ishara nzuri hujui hata tume imeundwaje.

Pili, pamoja na kuwa uandikaji wa katiba ya sasa haukufuata kanuni za kuandika katiba William lazima aelewe kuwa tume si kikundi cha makarani cha kukusanya maoni. Hata kwa mtindo huo bado haelewi kuwa waliotoa maoni ni wananchi na tume haina sababu za kusikiliza maoni ya CCM bali wananchi. Kusema kazi ya tume ni kukusanya maoni ni umbu mbu wa hali ya juu sana.

Tume ya Warioba haipo kubadili katiba, ipo kutengeneza mazingira ya kuandika katiba kama ilivyotakiwa na sheria ya bunge lenye CCM wengi na kusainiwa na mwenyekiti wa CCM ambaye ni rais. Hii si tume ya kubadili katiba Mwana wa Malecela, mbona no vitu rahisi sana kuelewa.

Tume ya kukusanya maoni ya vyama vingi ilikuwa ya rais hikuwa na nguvu za kisheria. Hata ilipotoa maoni bado busara zilitumika . Halikuwa suala la wengi wanasema nini.

Kuhusu tuhuma kwa Warioba, kwanza nikuambie Njelu Kasaka alikuwa kiongozi wa G55 baba yako mzee J.S alikuwa kiongozi wa serikali lakini kutokana na wadhifa wake hakuweza kuonekana ndani ya G55 ingawa aliunga mkono hoja ya G55.

J.S akiwa waziri mkuu aliruhusu hoja ya watu 55 iingie bungeni ili kubdaili katiba bila kuzingatia maoni ya wananchi. Nyerere akasema kama hiyo haikuwa sera ya CCM na wale wanaoitaka waondoke ndani ya chama wakaitetee wakiwa nje. Nyerere akasema ' Wahuni' wamimshauri rais vibaya ndiyo Malecela akapigwa chini na kuanguka kisiasa kukaanzia hapo hadi sasa ambapo watoto ndio hawa tunawasoma.

Babay yako mzee J.S.Malecela ndiye alikuwa kiongozi wa G55 kwa kujificha nyuma ya Njelu Kasaka. Hakutaka seriakli 3 kwa fiada ya nchi alitaka awe rais wa Tanganyika. Hivyo mwasisi wa serikali 3 katika miaka ya karibuni ni baba yako. Warioba ana rekodi zake lakini ya baba yako ndiyo inakutesa wewe na CCM.

Laana ya Nyerere ndio imelekea baba yako kutokuwa rais wa nchi hii hata siku moja. Hilo linakukera sana na unaamua kumaliza hasira kwa Warioba. Kwa mwendo ulivyo sidhani kama familia ya Malecela itatoa kiongozi tena maana kama mwanae ni wewe bipo kazi ya miaka mingi.

Ninachoogopa ni kumuona William akitoa maamuzi yanayogusa maisha yetu. Kidogo angekuwa mbunge wa EAC, na bado hatujapona anaweza kuwa mkuu wa Wilaya, mkoa au balozi. Eeeh Mola tusaidie kutuepusha na mabalaa


- ha! ha! Childish, Nyerere, mara baba yako, what do have anything to do na this mess Warioba has put himself in? Aliombwa kuandika maoni ya katiba mpya kutoka kwa wananchi that is all hakuombwa maoni yake binafsi, ingawa anao uhuru wa kufanya hivyo ila tu akiwa nje ya tume,

- Mkuu sana umelia sana lakini nje ya topic fungua thread inayonihusu na inayomuhusu baba yangu na wako, hapa tunajadili Taifa, kwamba Sheria inasema nini kuhusu maamuzi ya kurekebisha katiba, inasema CCM yenye majority bungeni na ambao ndio watawala, wana haki ya kuamua katiba iweje sio Chadema, CUF, Warioba au wewe na matusi yako haya ya kitoto sana, pole sana sio mimi ni Sheria ya jamhuri!! ha1 ha1 ha!

Le Mutuz
 
ccm kama nani? Wananch wengine wasio na vyama hawana hiyo haki kubwa jinga wewe! Unaja mb a jamba tu ! Hapa jukwani kila post yako imejaa ushabiki stop!

- ha! ha! ha! yaani wewe sasa ndio kabisa umenivunja mbavu zangu, eti unauliza CCM ni nani hujui? ha1 ha! ha!, halafu unasema nini eti ni makosa ya CCM kuwa tuna wananchi wasio na Vyama? ha! ha!

Le Mutuz
 
- tunaishi kwa Sheria sio kanuni, Sheria ipo wazi Warioba hana mamalaka ya kuwaamulia wananchi Katiba, ila anayo mamalaka ya kukusanya maoni yao na kuyaandika chini, Warioba hana mamlaka yoyote kikattiba ya kuwaambia eti Viongozi wa Saisa wakae chini kujadili tena Rasimu, Rasimu imeshaenda Bungeni imepitishwa na Wabunge wa Chadema na CCM, sasa inasubiri saini ya Rais iwe Muswaada na kujadiliwa na Wabunge ,

- Labda nikukumbushe historia kidogo, kule USA ni Republicans ndio walioamua kupunguza mafao ya Marais wao kwa sababu ya wingi wao bungeni, na ni wao ndio walioamua kupunguza malipo ya welfare ya wananchi wao bila kujali uchache wa Democrats bungeni kwa sababu Sheria inasema ni majority ndio wenye uamuzi wa mwisho wa marekebisho ya sheria, CCM ndio wenye mamlaka ya mwisho kisheria ya jamhuri kuamua katiba mpya iweje sio Warioba na Chadema.

Le Mutuz
Siku zote nilikuwa najiuliza kwanini wabunge hawakukuchagua kuingia Bunge la EAC, sasa nimepata majibu walishajua wewe ni kilaza wa kutupwa. Mkuu unazungumzia rasimu gani ambayo imepitishwa na bunge na inasubiriwa kusainiwa na rais? au mwenzetu uko kuzimu. Kinachosubioriwa kusainiwa na Rais siyo rasimu aliyokuwa anaizungumzia Jaji Warioba ni sharia inayohusu utaratibu kwa majadiriano katiba Bunge la Katiba.
 
- Sijui kitu really? Muswaada wa sasa umepitishwa bungeni na nani kama sio CCM, tuliza boli mkuu maana hujui kinachoendelea ni kwamba CCM tu ndio wenye haki ya kuamua katiba mpya iwe vipi, na habari ndio iyoooooo!! ha! ha1

Le Mutuz


Ha haha ha haaa!! Kweli kua uyaone!!! Wanao amua Katiba ni Wananchi siyo CCM! Wewe vipi??
 
Siku zote nilikuwa najiuliza kwanini wabunge hawakukuchagua kuingia Bunge la EAC, sasa nimepata majibu walishajua wewe ni kilaza wa kutupwa. Mkuu unazungumzia rasimu gani ambayo imepitishwa na bunge na inasubiriwa kusainiwa na rais? au mwenzetu uko kuzimu. Kinachosubioriwa kusainiwa na Rais siyo rasimu aliyokuwa anaizungumzia Jaji Warioba ni sharia inayohusu utaratibu kwa majadiriano katiba Bunge la Katiba.

Mkuu huyu jamaa nilijaribu kumuelimisha toka jana kuhusu anavyochanganya mambo mawili tofauti, lakini akaweka pamba masikioni. Labda sasa tumshauri akasome hotuba ya mwisho wa mwezi aliyoitoa JK, kwenye kipengele kinachohusu katiba mpya, labda ataelewa mchakato mzima ulianzaje, uko wapi kwa sasa, na nini kitafuata. Yani hata hajui anaongea nini. Kakazania ooh Warioba kamaliza kazi, wakati hata rasimu ya pili haijatolewa bado na Tume.
 
Back
Top Bottom