Jaji Warioba aishangaa Tume ya Uchaguzi kwa kitendo cha kuengua Wagombea wa Vyama mbalimbali vya upinzani bila kufuata utaratibu

Mkuu mimi ni uvccm taifa, lakni hata hivyo nafaham umuhim wa upinzani katika serikali, so kiukweli wapinzani wananafasi yao katika serikali na taifa kwa ujumla
Mnawapataje sasa?Turudie uchaguzi maana tumejifunza kwa gharama kubwa mno.Tufanyeni kuwa kuna kasiro kubwa zimejiri,lipelekwe azimio bungeni kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya then tufanye Uchaguzi Mkuu upya kwa Katiba hiyo Mpya.
Kufikia hilo,tuanzie na Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Warioba,liundwe Bunge Huru la Katiba bila kuwahusisha wanasiasa/itikadi za vyama vya siasa.Tusipofanya hivyo tunaparaganyika zaidi na kugawanyika(Ukosefu wa Uhuru na Umoja) ni kidonda.
 
Jamani huyu Mzee amepiga kelele sana tangu kwenye Rasimu yake ya Katiba! Nadhani moja ya maeneo ambayo yaliguswa na Rasimu yake ni marekebisho ya Tume ya Uchaguzi.Tusisahau jinsi mzee alivyoshambuliwa na genge lililoongozwa na Bashite!
Mimi nadahani si kwamba Wazee wa nchi hawayaoni haya ambayo yanaendelea katika Taifa letu chini ya utawala huu,wanayaona lakini kwa umri wao lazima waogope kwa sababu ya kulinda mkate wao.
Kama wanathubutu kulinda mkate wao basi wametusaliti.Misingi ya Taifa inayosiginwa leo ni hao Wazee/waasisi ndiyo waliiweka.Je,wanapovumilia inapovurugwa tuwape jina gani?Hao wanaoharibu na kuivunja Katiba wapo juu ya sheria.Tuwape na jina wanalostahili kuitwa.
 
Hahahhaaa yani upinzani mtazalauriwa na kukejeliwa mpaka lini??😂😂 yani warioba ndo ameona jana vitendo hivi??
Hii inaonyesha ni jinsi gani mnavyokejeliwa na serikali 😂😂😂
Uislam unasema ukiona jambo baya liondoe kwa mkono wako, kama huwezi liondoe kwa mdomo wako na pia kwa mdomo kama ni gumu lichukie moyoni, mzee wa watu ametimiza wajibu wake mwacheni, ndugai alipiga biti vyombo vya habari viache kuwafuata wastaafu eti mambo yamebadilika
 
Jaji Joseph Sinde Warioba ameishangaa tume ya uchaguzi ya Tanzania kwa kitendo chake cha kuengua wagombea wa vyama mbalimbali vya upinzani bila kufwata utaratibu.

Ameishangaa kuengua wagombea wa vyama mbalimbali bila kuzingatia katiba badala yake kutumia vigezo dhaifu ktk kumuengua mgombea.

Ameishauri tume kufwata utaratibu mpya badala utaratibu huu Usiokua wa haki.

Pamoja na hayo ameshangaa kuona viongozi wa kisiasa wanashindwa kukaa pamoja kwa ajili ya Taifa badala yake wametanguliza ubinafsi, tamaa ya madaraka na itikadi.

Amewashauri kuachana na itikadi za vyama vyao badala yake waliangalie Taifa.

Ameyasema hayo ktk maadhimisho ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Huyu ni Kiongozi wa kwanza mstaafu ambae ameishaanza kuona madhaifu yetu kama nchi ambayo yanaweza kutupeleka kubaya kama nchi na hivyo kutoa tahadhari.

Amevunja ukimya na kujionesha utofauti wake na wengine ambao ni wazalendo maslahi ambao kazi yao kubwa ni kusifu na kuabudu ili kulinda matumbo yao na familia zao.
Huyu mzee sijui ataacha lini kumaliza kuvuta bunda za sigara
 
Hayawezi kubadilika kivipi, kwani huu Uchaguzi ni wa mwisho,kwani Rais Magufuli ni wa milele, kwani Tanzania ndio inaisha baada ya huu utawala....Mzee ameongea maneno ambayo yataishi vizazi na vizazi..hajawaza tumbo lake amewaza hatma ya Taifa letu.
Yeye ni miongoni mwa watu muhimu anatakiwa akemee kabla ya kuleta madhara hizo ni hadithi.
Mfano wakati tume inajiaanda kuiba kura kwa kutoa tamko kuwa hakuna nakala watayopewa mawakala .angechukuwa hatua ya kukemea.sasa Kuna raia wapo ndani,Mali zimeteketezwa na maisha kupotea.kisha wanaleta unafiki.aongelee lililopo
 
Asante mzee Warioba, natamani wazee wenye hekima walisemee taifa.Bado tuna nafasi kurekebisha tulipo jikwaa.
Mzee Mwinyi anatia aibu, HANA kabisa uwezo kulisemea taifa. Na hivi keshakamilisha biashara ya mwanae, ndio basi tena.
 
Hapo Mkapa nae angekuwepo angeongeza maneno yake mazito,ila Warioba,Malecela,Butiku n.k wakipumzika hatutakuwa na wenye hekima na msimamo ktk taifa letu
 
Jaji Joseph Sinde Warioba ameishangaa tume ya uchaguzi ya Tanzania kwa kitendo chake cha kuengua wagombea wa vyama mbalimbali vya upinzani bila kufwata utaratibu.

Ameishangaa kuengua wagombea wa vyama mbalimbali bila kuzingatia katiba badala yake kutumia vigezo dhaifu ktk kumuengua mgombea.

Ameishauri tume kufwata utaratibu mpya badala utaratibu huu Usiokua wa haki.

Pamoja na hayo ameshangaa kuona viongozi wa kisiasa wanashindwa kukaa pamoja kwa ajili ya Taifa badala yake wametanguliza ubinafsi, tamaa ya madaraka na itikadi.

Amewashauri kuachana na itikadi za vyama vyao badala yake waliangalie Taifa.

Ameyasema hayo ktk maadhimisho ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Huyu ni Kiongozi wa kwanza mstaafu ambae ameishaanza kuona madhaifu yetu kama nchi ambayo yanaweza kutupeleka kubaya kama nchi na hivyo kutoa tahadhari.

Amevunja ukimya na kujionesha utofauti wake na wengine ambao ni wazalendo maslahi ambao kazi yao kubwa ni kusifu na kuabudu ili kulinda matumbo yao na familia zao.
Alikuwa wapi siku zote?
 
Maneno yanasaidia nini?...chaguzi zipo hawataongea mpaka uchaguzi upite so maneno yao ni useless

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
At last amejitokeza kiongozi mwenye ujasiri wa kuuambia uongozi uliopo ukweli kuhusu mambo yanavyoenda hovyo kama gari inayoendeshwa na mlevi. NEC imejaa watu waliobobea kwenye sheria lakini vitendo na maamuzi hayakuonyesha hubobezi huo.
 
Alikuwa wapi muda wote hayo maneno angesema mwezi wa tisa.
Labda kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa uchaguzi mkuu ulikuwa bado. Huenda alijipa matumaini kuwa yasingejirudia kwenye uchaguzi mkuu kutokana na jinsi ulivyosheheni wanasheria
 
Huo ndio ukweli tusiangalie matokeo sisi tuendelee kupiga kelele kwani maisha hayajasimama
Haswa kwa kila anayetoa kauli ya kupinga kupelekwa kwenye nchi isiyofuata sheria tumuongezee kauli zetu ili asijione yupo peke yake.
Prof Safari naye kwanza Maji Warioba na wengine. Dikteta atatoa shingo tu ili jambia lipite
 
  • Thanks
Reactions: bne

Jaji Joseph Sinde Warioba ameishangaa tume ya uchaguzi ya Tanzania kwa kitendo chake cha kuengua wagombea wa vyama mbalimbali vya upinzani bila kufwata utaratibu.

Ameishangaa kuengua wagombea wa vyama mbalimbali bila kuzingatia katiba badala yake kutumia vigezo dhaifu ktk kumuengua mgombea.

Ameishauri tume kufwata utaratibu mpya badala utaratibu huu Usiokua wa haki.

Pamoja na hayo ameshangaa kuona viongozi wa kisiasa wanashindwa kukaa pamoja kwa ajili ya Taifa badala yake wametanguliza ubinafsi, tamaa ya madaraka na itikadi.

Amewashauri kuachana na itikadi za vyama vyao badala yake waliangalie Taifa.

Ameyasema hayo ktk maadhimisho ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Huyu ni Kiongozi wa kwanza mstaafu ambae ameishaanza kuona madhaifu yetu kama nchi ambayo yanaweza kutupeleka kubaya kama nchi na hivyo kutoa tahadhari.

Amevunja ukimya na kujionesha utofauti wake na wengine ambao ni wazalendo maslahi ambao kazi yao kubwa ni kusifu na kuabudu ili kulinda matumbo yao na familia zao.
Mwambieni aendelee kushangaa.
Watakapokata mafao yake ndio ataacha kushangaa
 
Huyu naye asituchoshe. Katiba yake imegeuzwa karatasi ya chooni na ngwala juu. Hakufanya lolote
 
Ulikuwa wapi wakati uenguaji unaendelea.na hii ni tabia ya wastaafu wengi wenye hadhi yako +.nyie wastaafu mliokuwa mnaamua hatima ya maisha yetu ongeeni tukio likiwa linaweza kusahihishwa kabla ya madhara.hawezekani kaeni kimya kuhifadhi heshima kiasi iliyopo.
 
Tatizo unafiki si mkweii hakusema hivi mapema aijua mwanaye anapewa madaraka sasa ameona hamna kitu anajitokeza utazana anatupenda kweii. Katiba ya nchi inavunja wako kimya ii watoto wao wapewe vyeo.
Ukumbuke yeye ndie alieandaa mchakato wa katiba mpya eti.

Kwa hiyo usitumie hisia saana kumhukumu huyu mzee
 
Back
Top Bottom