Jaji Warioba aishangaa Tume ya Uchaguzi kwa kitendo cha kuengua Wagombea wa Vyama mbalimbali vya upinzani bila kufuata utaratibu

bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,657
1,992
Warioba.jpg

Jaji Joseph Sinde Warioba ameishangaa tume ya uchaguzi ya Tanzania kwa kitendo chake cha kuengua wagombea wa vyama mbalimbali vya upinzani bila kufwata utaratibu.

Ameishangaa kuengua wagombea wa vyama mbalimbali bila kuzingatia katiba badala yake kutumia vigezo dhaifu ktk kumuengua mgombea.

Ameishauri tume kufwata utaratibu mpya badala utaratibu huu Usiokua wa haki.

Pamoja na hayo ameshangaa kuona viongozi wa kisiasa wanashindwa kukaa pamoja kwa ajili ya Taifa badala yake wametanguliza ubinafsi, tamaa ya madaraka na itikadi.

Amewashauri kuachana na itikadi za vyama vyao badala yake waliangalie Taifa.

Ameyasema hayo ktk maadhimisho ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Huyu ni Kiongozi wa kwanza mstaafu ambae ameishaanza kuona madhaifu yetu kama nchi ambayo yanaweza kutupeleka kubaya kama nchi na hivyo kutoa tahadhari.

Amevunja ukimya na kujionesha utofauti wake na wengine ambao ni wazalendo maslahi ambao kazi yao kubwa ni kusifu na kuabudu ili kulinda matumbo yao na familia zao.
 
Hahahhaaa yani upinzani mtazalauriwa na kukejeliwa mpaka lini? 😂😂 yani warioba ndo ameona jana vitendo hivi??
Hii inaonyesha ni jinsi gani mnavyokejeliwa na serikali 😂😂😂
 
Jaji Joseph sinde waryoba ameishangaa tume ya uchaguzi ya TANZANIA kwa kitendo chake cha kuengua wagombea wa vyama mbalimbali vya upinzani bila kufwata utaratibu. Ameishangaa kuengua wagombea wa vyama mbalimbali bila kuzingatia katiba badala yake kutumia vigezo dhaifu ktk kumuengua mgombea. Ameishauri tume kufwata utaratibu mpya badala utaratibu huu Usiokua wa haki...

Ngoja tuone kama magazeti yanayotarajiwa kufa yataandika hii kitu kesho
 
Jaji Joseph sinde waryoba ameishangaa tume ya uchaguzi ya TANZANIA kwa kitendo chake cha kuengua wagombea wa vyama mbalimbali vya upinzani bila kufwata utaratibu.
Kila mtu anaishangaa tume sio Warioba pekw yake, labda mazuzu tu ndio wanaoweza kuona sawa lakini wenye akili timamu wanajiuliza hawa viongozi wa tume wana akili gani maana mambo wanayofanya hata mtu wa la saba b hawezi kufanta
 
Hahahhaaa yani upinzani mtazalauriwa na kukejeliwa mpaka lini??😂😂 yani warioba ndo ameona jana vitendo hivi??
Hii inaonyesha ni jinsi gani mnavyokejeliwa na serikali 😂😂😂
Hapana sio Hivyo Ila nikwamba wamegundua makosa makubwa yaliyofanyika na sasa wanaona umuhimu WA wapinzani nchini
 
Utasikia kauli hii kutoka kutoka kwny mamlaka ya juu 'waandishi wa habari msiwasumbue wazee wetu waliolitumikia taifa hili kwa uadilifu na weledi waacheni wapumzike wazee wetu'.
Hahahaha Kwakweli tulipofika ni mungu tu ndio wakutuokoa la hatutafika salama
 
Jaji Joseph sinde waryoba ameishangaa tume ya uchaguzi ya TANZANIA kwa kitendo chake cha kuengua wagombea wa vyama mbalimbali vya upinzani bila kufwata utaratibu...

Na yeye ajishangae kwa nini katiba yake kashindwa kuitetea kufa na kupona
 
Back
Top Bottom