Carlos Valderrama
JF-Expert Member
- Dec 27, 2014
- 664
- 240
Umuelewi kivipi wakati Warioba ni kada wa CCM muda mrefu wewe ulidhani yupo Ukawa?Nashindwa kumuelewa jaji Warioba kuhusu katiba yeye kasimamia wapi maana anaowanadi sasa hivi walimtukana mpaka kumpiga kisa alikuwa na msimamo juu ya katiba ya wananchi.
Ebu tujadili; je, na yeye kakubali katiba pendekezwa?
Unachoshindwa kumuelewa ni kipi hasa?
Msimamo wake kuhusu katiba kabadilisha?
Hawezi kukiunga mkono chama chake katika kampeni za urais kama anatofautiana nacho kuhusu katiba?
Mbona anamnadi tibaijuka chenge mhongo etc mafisadi waliokiri na midomo yao walilamba
Nashindwa kumuelewa jaji Warioba kuhusu katiba yeye kasimamia wapi maana anaowanadi sasa hivi walimtukana mpaka kumpiga kisa alikuwa na msimamo juu ya katiba ya wananchi.
Ebu tujadili; je, na yeye kakubali katiba pendekezwa?
Chadema ndiyo wamewasaliti upinzani na kuungana na mafisadiWamesaliti kazi yao iliyo bora,Wamewasaliti wananchi Maskini NA sasa hawazungumzii tena katiba mpya zaidi ya kupambana NA LOWASSA. Magufuli akishinda Urais hawezi kubadilisha msimamo WA bunge maalum LA katiba lililo pitisha katiba pendekezi zaid ya kufanya referendum.WARIOBA NA POLEPOLE wametuacha kwenye mataa sisi wakulima maskini.hawatakua NA jipya kwa wananchi tena zaidi ya sisi kuwaona wasaliti.
Wasalaam
Abel sere from Moshi
Hata Saed kubenea, waliomwagia tindikali ndio hao sasa anawaandika vizuri, kwahiyo ushishangae ya Warioba anza kwanza na ya kubenea. hii ndio tz kama huijui
Namuheshimu sana Jaji Warioba, lakini kwa hili la kukubali kutumika pamoja na kutukanwa sana na kupigwa kwa baraka ya chama hicho hicho, na bado akasimama nao jana linampunguzia sana heshima kwangu.. Nakumbuka Bulembo alivyomtukana huyu mzee and yet jana wakawa jukwaa moja..!
Amefnya hivyo kwa sababu gamba tayari limevuka, Fisadi hayupo tena CCM, Nachama kimebaki salama
pochi imebadilisha upepo!
Sio Siri..Jaji Warioba ameingia chaka.Ni dhahiri huyu bwana ni kigeugeu.Bora angekaa kimya kama mawiri wakuu wastaafu wenzake kama Salim Ahmed Salim,Msuya na Malecela.
#Hapa Kazi tu..kula kwenu.
Hujaeleza ameingia chaka kivipi na kwa nini ni kigeu geu.
Inawezekana unashindwa kumuelewa kwa kukosa uchambuzi wa kina utakaoweza kuelewa kwamba mtu anaweza kutokubaliana na chama chake kwenye masuala fulani lakini pia akaona hakijapata mbadala na hivyo kuamua kukiunga mkono katika kampeni na kubaki kama chachu ya mabadiliko kutoka ndani ya chama hicho.
Usichoelewa hapo ni nini?
Au wewe kumuelewa mtu ni lazima afikiri kama wewe na kuunga mkono fikra unazounga mkono wewe?
Fisadi gani huyo? Ni yule/wale waliohusishwa na ESCROW scandal; maana hao bado wamo ndani ya chama kilichochoka. Gamba ambalo "tayari limevuka" halikushiri escrow hivyo mchawi anayeiua CCM bado yungalimo ndani ya CCM.
Mbona Hujamshangaa Mbowe Kupokea Makapi Kutoka Ccm Wakati Yalisigina Katiba Pia Mpaka Ukawa Ukaundwa?
Mlidgani warioba ni mpumbavu na lofa kama nyinyi?
Fisadi gani huyo? Ni yule/wale waliohusishwa na ESCROW scandal; maana hao bado wamo ndani ya chama kilichochoka. Gamba ambalo "tayari limevuka" halikushiri escrow hivyo mchawi anayeiua CCM bado yungalimo ndani ya CCM.