Jaji Sinde Warioba kanishangaza

Jaji Sinde Warioba kanishangaza

Umoja Kamili wa Wapumbavu = UKAWA oyooooooooooooooooooooooooo Wapumbavuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu (in Mkapa's Voice)
 
Ikumbukwe kuwa Jaji Warioba alikuwa akizunguka kutoa elimu ya uraia pamoja na kueleza wananchi jinsi maoni yao yalivyotupwa kwenye rasimu ya katiba jambo ambalo lilifanya atukanwe, adhihakiwe, adharauliwe na hata kudaiwa kupigwa.

Kilichonishangaza ni yeye kusimama jana na kupiga kampeni kwa wagombea, wakati kwanza chama hicho ndo kilihusika kusigina maoni ya wananchi, pili mmoja wa wagombea alikuwa makamu mwenyekiti bunge la katiba sasa Mh. Warioba ulikuwa unazunguka kufanya nini kwa wananchi ikiwa leo una wanadi waliosigina maoni ya wananchi?

Sikutegemea kwa kweli, sasa vipi ile rasimu ya wananchi ndo huitetei tena? Nimewaza kwa sauti wajamaeni.

Ndugu kwenye siasa kuna unafiki na ulielewe hilo, Unakumbuka walivyokuwa wanasema wakina Mbowe, Msigwa, Mdee, na wapinzani wengine kuhusu Mh. Lowassa wakati yupo CCM?
Unakumbuka alichokisema Sumaye kwenye mchakato wa kuchukua forms za kuteuliwa na CCM juu ya Lowassa?
Ndio maana huwa nasema mwanasiasa mwenye maono angalau ni Dr. Slaa hawa wengine wote ni wachumia tumbo tu na wanaojali zaidi maslahi yao binafsi.
 
Warioba ni mwana ccm sasa tunataka asimame jukwaa lipi? Mambo mabaya alifanyiwa na wana ccm sio ccm kwahyo ye anaumia anapoona ccm inaharibu misingi yake
Ana imani na huyu anaetarajiwa ndo maana kajitokeza.
 
Ukiona hivyo ndio ujue hata magufuli hatakuwa na jipya
 
We unafikiri ule mtama mchezo??ukitaka wazee wasikufuate fuate mpige mtama wa nyumanyuma hawezi rudia tena.
 
Politicians are alive ONLY because it is illegal to kill them!

Nimeamini kuwa mwanasiasa anachokisema kwa ukweli ni jina lake tu!
 
Hii ndio ajira yako wengi tunalijua hilo. Hivi kama tukiamua wote humu ndani kussupport cCM kwa kila Jambo utalipwaje?
Umepena kuyasema hayo! mimi si ccm kamwe na sijawai kuwa ccm wala cdm ispokuwa natambua mtamsema vibaya yeyote yule atakae wakosoa, siasa ni kukosoana sasa mnapo panic mkosolewapo hamjui siasa mnafuata mkumbo
 
Huyu Huyu Mzee Warioba Ndiye Alipigwa Na MaCCM Wenzake Kwa Sababu ya Kushaabikia rasimu yake ya Katiba. Leo Ni

Kimbembele wa Kuishaabikia CCM. Kweli CCM Ni Ile Ile..Do Hata Dr. Magufuli Hawezi Lolote Kwa MiCCM.

hushangai kuona waliomponda lowassa na kumchafua leo ndo mgombea urais wa saccos yao umeona la warioba tu.... zinduka toka usingzn na kutumia akili za mgando kufikilia....
 
Alicho fanya mzee warioba nisahihi kwakuwa hakuna chama cha upinzani ndio maana amepanda ktk jukwa la ccm A kama alivyo sema mzee mwinyi.
Laiti wapinzani wasinge uza vyama vyao kwa maccm B mzee warioba asingeweza kufanya alivyo fanya.

Naona uko sahihi kwa 100% kwani hakuna aliyekanusha kuwa wao sio ccm b,badala yake wanafurahia.
 
Sote ni mashuhuda, kilichotokea siku ya Tarehe 23, katika viwanja vya jangwani kulipofanyika uzinduzi wa kampeni ya CCM kuelekea Uchaguzi wa oktoba 25.

Walikuwepo manguli wote wa siasa za Tanzania, akiwemo Jaji Mstaafu Warioba, ambaye alikua mwenyekiti wa Tume ya kuratibu maoni ya wananchi katika mchakato wa kupata katiba mpya.

Uwepo wake umekua wa faraja na umehitimisha safari ya uhalali wa vyama vinne vya upinzani vilivyounda umoja wao na kuuita UKAWA.

Dhana nzima ya Muunganiko huo kama wanavyotaka tuwaamini ilikua ni kupigania matakwa ya wananchi yaliyoratibiwa na tume, kabla ya kufanyiwa marekebisho na bunge na kutoa rasimu ambayo itapigiwa kura na kuamuliwa na wananchi.

Jaji mstaafu warioba, pamoja na kuzungumzia mengine, aliutaarifu uma kwamba atakuwepo kuipigia kampeni CCM katika uchaguzi wa oktoba 25.

Kauli hiyo ni nzito, na inamaana kubwa katika uhalali wa muunganiko wa Ukawa, kauli ya muasisi wa madai ya Ukawa, inatoa picha moja kubwa kwamba, watu hao hawaaminiki, na si watu sahihi katika kuhakikisha wananchi wanapata wanachokihitaji.

Ukawa ingepata Uhalali kama ingepata support ya nguli huyu wa siasa,lakini kwa kua amewakataa kwa kutojihusisha nao, sidhani kwanini sisi wananchi wa kawaida ambao hatupo karibu na hao watu tuwakubali.

Kifupi ni kwamba UKAWA imekufa na imepoteza uhalali wake kimantiki tokea siku ile ilipoanza kukumbatia watu wenye tuhuma mbali mbali kama watu wake wa karibu. Jambo hili si dogo na limemfanya mwasisi wa madai yao kuwakana hadharani.

Ni jambo la heri mno kwa Mh. jaji Mstaafu kuona kua kikundi hicho ni cha wababaishaji, na watumiaji wa uelewa mdogo wa wananchi katika mambo flani kujinufaisha kisiasa kwa malengo binafsi.

Ukawa haina pakusimamia, imekufa kabla hata ya Oktoba kufikia, tunashukuru kuona wazee kama hawa wakijitokeza na kuwaumbua hadharani hawa watu.
 
Huyu mzee hajitambui, hao ccm walituma mtu ampige, na baada ya yy kupigwa mwenzake kazawadiwa madaraka, warioba alizunguka kuisema ccm na ubaya wake juu ya kuhodhi maoni ya watanzania, eti leo anatuambia hao hao ccm wni wa maana, ha, hii ccm imejaa wachawi kwa nini wazee tu nido wanaopewa nydifa? Kama kale kazee ka NEC kana karibia 80 yrs, eti bado ni mfanyakazi wa serikali, nchi ina vituko hii sijapata kuona.
 
Mimi pia namheshimu sana Jaji Waryoba pamoja na UCCM wake. Lakini katika hili la kampeini, kapiga nje kabisa, heli angekaa kimya kabisa tu
 
S

Kifupi ni kwamba UKAWA imekufa na imepoteza uhalali wake kimantiki tokea siku ile ilipoanza kukumbatia watu wenye tuhuma mbali mbali kama watu wake wa karibu. Jambo hili si dogo na limemfanya mwasisi wa madai yao kuwakana hadharani.

Ni jambo la heri mno kwa Mh. jaji Mstaafu kuona kua kikundi hicho ni cha wababaishaji, na watumiaji wa uelewa mdogo wa wananchi katika mambo flani kujinufaisha kisiasa kwa malengo binafsi.

Ukawa haina pakusimamia, imekufa kabla hata ya Oktoba kufikia, tunashukuru kuona wazee kama hawa wakijitokeza na kuwaumbua hadharani hawa watu.
Jaji Warioba aliongoza tume kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa rasimu kwa kuzingatia maoni hayo. Kazi ambayo aliifanya kwa umakini na uaminifu mkubwa na ameingia katika vitabu vya historia ya Tanzania kwa mchango wake huo mkubwa na uliotukuka, na ndio maana rasimu hiyo itaendelea kurejelewa kama 'Rasimu ya Warioba' hata baada ya miaka mia. Lakini hiyo haina maana kuwa ni mali yake au yaliyomo ni mawazo ya Warioba au ya mwanaTume ye yote, bali ni maoni ya wananchi wa Tanzania. Kwa hivyo hata akihama nchi au kuchukua uraia wa Rwanda (kwa mfano), hayo maoni yataendelea kuwa ya wananchi wa Tanzania na mali ya Wananchi. Kwa hivyo basi kujiunga kwake tena na timu ya kutetea mafisadi wa CCM (kumbuka na yeye hajawahi kuikana CCM), haihalalishi UKAWA waache kutetea maoni ya wananchi. Ni mtu mwenye uelewa wa kiwango cha chini anayeweza kunena kuwa "Ukawa haina pakusimamia, imekufa kabla hata ya Oktoba kufikia, tunashukuru kuona wazee kama hawa wakijitokeza na kuwaumbua hadharani hawa watu." Na mtu mwenye fikira kama hizi si kosa lake, bali ni matokeo kuntu ya elimu za kata (sekondari na vyuo). Mzee Warioba ni haki yake kupigia kampeni CCM kama UKAWA walivyo na haki yao kutetea na kupigania maoni ya Wananchi kuzingatiwa katika Katiba mpya.
 
Kupuuzwa na kupigwa koote eti Warioba bado ana guts za kusimama kuiombea ccm kura? Au Kip kamtuma babake ku-sacrifise heshima yake kwa ajili ya kanafasi ka ubunge?
Hebu mawzaziri wakuu wastaafu acheni kujidhalilisha kwa wananchi waliowaamini na kujiheshimu. Igeni wa nchi nyingine wanaokosoa wanapoona kasoro na wanaoisimamia maneno yao na sio ninyi waganga njaa.
Nakushangaa Warioba kwa usaliti wako kwetu sisi wapenda mabadiliko. Hii dhambi ya usaliti itakutafuna wewe na jamaa zako milele!
 
Huyu mzee angeachana na siasa za jukwaani abaki kuwa mshauri wa chama, ingawa ni kitu ambacho wameshashindwa ndiyo maana chama kimefika hapo. Ndiuo maana tuliowatarajia kuwa na busara wamejitoa ufahamu na kumwaga matusi.
 
Amefnya hivyo kwa sababu gamba tayari limevuka, Fisadi hayupo tena CCM, Nachama kimebaki salama
Fisadi gani huyo? Ni yule/wale waliohusishwa na ESCROW scandal; maana hao bado wamo ndani ya chama kilichochoka. Gamba ambalo "tayari limevuka" halikushiri escrow hivyo mchawi anayeiua CCM bado yungalimo ndani ya CCM.
 
Wamesaliti kazi yao iliyo bora,Wamewasaliti wananchi Maskini NA sasa hawazungumzii tena katiba mpya zaidi ya kupambana NA LOWASSA. Magufuli akishinda Urais hawezi kubadilisha msimamo WA bunge maalum LA katiba lililo pitisha katiba pendekezi zaid ya kufanya referendum.WARIOBA NA POLEPOLE wametuacha kwenye mataa sisi wakulima maskini.hawatakua NA jipya kwa wananchi tena zaidi ya sisi kuwaona wasaliti.

Wasalaam
Abel sere from Moshi
 
Back
Top Bottom