"Jaji Mwenzangu Luvanda" Machozi ya samaki majini hayatakufikia wewe na kizazi chako mpaka cha nne, tekeleza maagizo

Kwanini ‘Jaji wa Kimkakati’ Elinaza Luvanda anasikiliza kesi ya Mbowe?

Hana hatia, huenda anatekeleza maagizo toka juu kama ilivyo kwa Msajili /Registrar Simba wa Mahakama kuu amewekwa Kisutu kwa mikakati maalum.

Juzi Jaji Elinaza Luvanda alitupilia mbali pingamizi la awali ambalo lilikuwa limewekwa na mawakili wa upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema.

Uamuzi wa Jaji Luvanda, umesababisha baadhi ya watu kutaka kumjua yeye ni nani, na imekuwaje akawa msimamizi wa Mahakama Kuu Division ya Uhujumu Uchumi na Rushwa. SAUTI KUBWAi imefuatilia na inayo machache ya kueleza kuhusu wasifu wa Jaji Luvanda katika kesi za aina hii – “kesi za kimkakati” zinazofunguliwa na dola.

Kwa kifupi, huyu ndiye Jaji Elinaza Luvanda:

Mwaka 2017, Elinaza Luvanda alikuwa katibu wa Kaimu Jaji Mkuu, Jaji Ferdinand Wambari.
Mwaka 2018, aliteuliwa kuwa mjumbe kwenye Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania hadi Rais John Magufuli alipomteua kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Mwaka 2021, Jaji Luvanda aliwahukumu kifungo cha maisha Shamim Mwasha na mkewe kwa makosa ya mihadarati.

Mwaka 2020, alikuwa miongoni mwa jopo la majaji watatu ambao walikuwa na kesi ya Addo Shaibu dhidi ya Jamhuri kuhusu kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adelardus Kilangi.

Mwaka 2021, alikuwa miongoni mwa jopo la majaji watatu waliosikiliza kesi ya Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) – kesi ya kikatiba dhidi ya Kamishina Jenerali wa Magereza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mwaka 2019, alikuwa miongoni mwa jopo la majaji watatu katika kesi ya Zitto Kabwe dhidi ya Spika Job Ndugai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali – kesi ya sakata la CAG Assad kuhojiwa na Kamati ya maadili ya Bunge.

asante hisani Ngurumo

Mwaka 2019, kesi ya madai ya sh.bilioni 10 ya Bernard Membe dhidi ya Musiba, ilianzia kwa Jaji Luvanda kabla hajahamishiwa Mahakama ya Ardhi na hivyo kesi ikapangwa Jaji De Melo.
Mwaka 2020, Jaji Luvanda aliwahukumu Anitha Oswald (mfanyakazi wa PPF Moshi) na Frank Moshi (dereva wa teksi) kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la mihadarati.

Mwaka 2020, Jaji Luvanda alitoa uamuzi wa kutaifisha Tsh.16.7 bilioni kuwa mali ya Serikali baada ya DPP Biswalo Mganga kuwasilisha ombi mahakamani kuwa washitakiwa waliokuwa na kosa la UPATU hawakuwahi kufika mahakamani tangu kesi ilipoanza. Washitakiwa walikuwa ni kampuni ya IMS Marketing Tanzania.

Ukiunganisha matukio haya na hukumu ambazo Jaji Luvanda ametoa, hatua kwa hatua, unaweza kuona kuwa huyu ni “jaji wa kimkakati” ambaye amekuwa anapewa kusikiliza kesi za kimkakati. Sasa anasikiliza kesi nyingine ya kimkakati inayomkabili Mbowe na wenzake watatu.

Wachambuzi na wachunguzi wetu wanaendelea kumulika mwenendo wa kesi hii na Jaji Luvanda.
Sawa. Mwache aendelee kumtumikia kafri. Ipo siku atalipa.
 
Duuuh kumbe wewe ni jaji kweli ?!!

Basi huko mahakamani utakuwa unawaonea watu sana wasio wa imani yako.....

Maandiko yako humu ndani yanaonesha hayo.....

Waafrika tuna safari ndefu sana ya kwenda....mmmh yaani Jaji huwa unajaa ubaguzi juu ya wengine hatari sana.....

Kizazi kijacho hakitakuwa na mihemko ya ubaguzi wa kidini ya hizo dini zilizokuja kutoka ughaibuni....

#AgainstHate
#AgainstBigotry
#AgainstRacism
#AgainstRadicalism
#AgainstAntiSemitism

#NchiKwanza
#SiempreJMT
nasimamia haki, sipendi uonevu, siku ya kiama tutaulizwa damu za watu.
Kufunga mwanaume gerezani miaka 20 unaacha mke ndio kaolewa tu , anamegwa na wengine nyumbani inauma,watu kupewa kesi za kubumba na maelekezo toka juu hapana.
 
Mkuuu huwezi kutoka nje na moyo na mwelekeo yako. Uko very biased and that’s an intellectual suicide. Na mimi nisiyekujua naweza kuwa prejudiced na kukuona kuwa wewe Ni CHadema au pro Mbowe egal Where truth lies.

Mko wengi sana humu JF na Sasa huwezi tofautisha JF na vikundi vya vyama vya siasa. Hakuna kati yenu anayependa kutoka nje ya mlengo Wake na kuwa objective. We have the Know all.
you are totaly wrong, i stand with justice and not hate, an not a politician .
 
Babu yangu alikuwa na usemi "pamoja na kunitolea mimacho yako kama bulb bado umeshindwa kuniona".... Ulinichukua muda mrefu sana Kumuelewa...
Babu yako alikuwa ni mtu mwenye busara sana. Sijui kama nawe umerithi angalao kiasi kidogo cha 'genes' zake kuhusu busara zake!
 
Mkuuu huwezi kutoka nje na moyo na mwelekeo yako. Uko very biased and that’s an intellectual suicide. Na mimi nisiyekujua naweza kuwa prejudiced na kukuona kuwa wewe Ni CHadema au pro Mbowe egal Where truth lies.

Mko wengi sana humu JF na Sasa huwezi tofautisha JF na vikundi vya vyama vya siasa. Hakuna kati yenu anayependa kutoka nje ya mlengo Wake na kuwa objective. We have the Know all.
Unabwabwaja na vitu usivyovijuwa, ili mradi tu uonyeshe ujuaji. "...intellectual suicide" unayoiandikia hapo inahusu nini?

Wewe unajiita 'unprejudiced', halafu hapa unalaani vikundi ambavyo vinatofautiana na vikundi unavyovishabikia wewe!

Hebu tuonyeshe bandiko lolote ulilowahi kuweka humu JF ambalo unajivunia kwamba ulionyesha "objectivity' juu yake.
 
Back
Top Bottom