UWT yasimama kidete kumsaidia ndugu. Maria ngoda katika kesi inayomkabili

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
UWT YASIMAMA KIDETE KUMSAIDIA NDUGU. MARIA NGODA KATIKA KESI INAYOMKABILI

RUFAA YA MARIA NGODA YASIKILIZWA

IRINGA
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu. Mary Chatanda (MCC) imeendelea kusimama kidete katika kuhakikisha inamsaidia Mwanamama Maria Ngoda ambapo jan Tarehe 01 Februari, 2024, Mahakama Kuu ya Mkoa Wa iringa Chini ya Jaji Mfawidhi Mgetta imesikiliza kesi ya Rufaa Namba 84101/2023 kati ya Ndg Maria Ngoda (almaarufu Mama wa Nyama wa Swala) Dhidi ya Jamhuri.

Akiongoza jopo la Mawakili nane (8) upande wa mrufani wakili Moses Ambwindile wakishirikiana na Mwanasheria Kutoka Umoja wa wanawake (UWT) Amesema, wametetea Sababu zao za Rufaa 14 mbele ya Jaji Mfawidhi , Aidha Jaji Mgetta ameahirisha Shauri hilo mpaka hapo tarehe 2 Februari, 2024 (leo).

Mfungwa Maria Ngoda (mkata rufaa) alihukumiwa kifungo cha miaka 22 kwa kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala mnamo tarehe 3 Novemba, 2023.

#UWTImaraJeshiLaMamaSamia
IMG-20240202-WA0242(2).jpg
IMG-20240202-WA0240(2).jpg
IMG-20240201-WA1797(2).jpg
IMG-20240202-WA0246(2).jpg
 
Sawa licha tunajuwa wanatafuta kik za kisiasa lakini wamsaidie huyo dad's

Ova
 
Walikuwa wapi wakati kesi inaendelea mwanzo?naungana na Mrangi ...ni Kiki za kisisasa
 
Na mwendesha mashitaka aithibitishie mahakama kuwa hiyo nyama ni ya swala, nchi imejaa uonevu sana, kuna tajiri mkubwa hapo iringa kaua sana tembo kule selous na Ruaha na wapumbavu wengine walishauri upewe ubunge wa iringa mjini, kesi hii ni matumizi mabaya ya kodi yangu
 
Back
Top Bottom